Anfaal
JF-Expert Member
- Jan 19, 2010
- 1,154
- 113
Baada ya harakati za uchaguzi, mambo mbalimbali yamekuwa yakijitokeza, hapa tutakuwa tunaweka hints ya vituko mbalimbali vilivyojitokeza na vinavyojitokeza kuelekea Uchaguzi Mkuu wa October 31.
Naanza kwa kuorodhesha baadhi:
Naanza kwa kuorodhesha baadhi:
- Mgombea wa Urais kupitia CHADEMA aanguka huko Mwanza wakati akienda kuomba kudhaminiwa na wananchi.
- CHADEMA yampitisha mgombea Urais bila hata kuthibitishwa na Mkutano Mkuu.
- Wagombea walioshindwa CCM wajiunga na vyama vya upinzani.
- NEC yamuibulia tuhuma nzito za Uraia kada wao maarufu na kutoa maelezo yasiyojitosheleza.
- Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM aanguka wakati wa kufungua mkutano wa Kampeni, jangwani jijini Dar es Salaam.
- Katika hali ya kushangaza, ni wagombea wa CCM tu mpaka sasa ndiyo wanaoshinda pingamizi na kupita bila kupingwa huku zile pingamizi za wagombea wa upinzani karibu zoote zikitupiliwa pembeni na hivyo kuleta hali ya mashaka kwa wale wenye mamlaka ya kusikiliza pingamizi hizo.