Elections 2010 Vituko vya uchaguzi

Anfaal

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
1,154
113
Baada ya harakati za uchaguzi, mambo mbalimbali yamekuwa yakijitokeza, hapa tutakuwa tunaweka hints ya vituko mbalimbali vilivyojitokeza na vinavyojitokeza kuelekea Uchaguzi Mkuu wa October 31.
Naanza kwa kuorodhesha baadhi:
  • Mgombea wa Urais kupitia CHADEMA aanguka huko Mwanza wakati akienda kuomba kudhaminiwa na wananchi.
  • CHADEMA yampitisha mgombea Urais bila hata kuthibitishwa na Mkutano Mkuu.
  • Wagombea walioshindwa CCM wajiunga na vyama vya upinzani.
  • NEC yamuibulia tuhuma nzito za Uraia kada wao maarufu na kutoa maelezo yasiyojitosheleza.
  • Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM aanguka wakati wa kufungua mkutano wa Kampeni, jangwani jijini Dar es Salaam.
  • Katika hali ya kushangaza, ni wagombea wa CCM tu mpaka sasa ndiyo wanaoshinda pingamizi na kupita bila kupingwa huku zile pingamizi za wagombea wa upinzani karibu zoote zikitupiliwa pembeni na hivyo kuleta hali ya mashaka kwa wale wenye mamlaka ya kusikiliza pingamizi hizo.
 
Hiyo Ya mwisho ndio inashangaza wengi, hasa lile pingamizi la Mashaka aka Masha
 
Hiyo Ya mwisho ndio inashangaza wengi, hasa lile pingamizi la Mashaka aka Masha
Mambo ya kushangaza yatakuwa mengi sana mwaka huu. Kwanza, mtu anaishi nchini na kupewa kibali cha kuchagua ( kuwa mpiga kura) lakini baada ya muda yeye mwenyewe akiomba kuchaguliwa anaambiwa si raia. Kitu cha kushangaza ni kuwa hakuna ufafanuzi mtu anaposema kuwa mwenzake si raia bila kuelewa kwanini si raia na ili awe raia inatakiwa aweje, hivi ni vitu vya kushangaza sana. Wengine wanatetewa kuwa ni raia bila ufafanuzi vile vile. Kazi ipo
 
Usisahau pingamizi la Dewji pia huko Singida !
ANGALIZO: Nivema account za Mabenki za hawa wasimamizi wa Uchaguzi kama huyu wa Singida zikaangaliwa na Takukuru, maana ghafla unaweza kukuta mafweza ya ghafla yasiyo na maelezo. Ndio TZ hii.
 
Tunaendelea;
  • Habari zisizo rasmi zinasema CHADEMA ilikuwa ikiwaomba wagombea ubunge wake walioshinda katika kura za maoni wawapishe watu wengine ambao CHAMA kinaona wanaushawishi zaidi.
  • CCM yawaengua baadhi ya wagombea ubunge kwa chama hicho kwa tuhuma za maadili huku wengine wenye tuhuma kama hizo wakiachwa waendelee na kugombea nafasi zao.
  • Harakati za CUF zimekuwa hazisikiki kabisa kwa upande wa Bara.
 
Back
Top Bottom