Vituko ulivyowahi kutana navyo stand.

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
34,910
41,467
Nakumbuka miaka hiyo naenda sana mikoa kwa bus.

Sikuhiyo nikiwa ndani ya basi jamaa kasubiria basi likiwa linaondoka ndio kanikimbizia gazeti kwakua lilikua na kichwa cha habari kilichovutia basi nikamrushia hela jamaa akanipa gazeti.

Ile nalifungua aisee ni gazeti la wiki moja iliyopita.

Yule jamaa kwakweli alifanya jambo la kishujaa mno.
 
huyo jamaa ni mimi 😂
 
Nilikuwa natafuta kabila la kuongopea wachumba nikaamua kwenda stendi ya mkoa pale Ubungo zamani,zoezi lilifanikiwa kwa Asilimia 100 mpaka leo watu wanajua mi kabila fulani.
 
Nilienda Ubungo kuchukua parcel miaka hiyo, nikiwa na bint flani hivi sasa wale wapiga debe wakadhani tunasafiri, kila tunaekutana nae anatuzonga, sisi tunawaambia hatusafiri ni parcel tunafuata, wanang’ang’aniza tuwaambie ni ofisi za gari gani ili watupeleke hatukuwaambia, sasa wakawa wameungana kama 10 hivi wanatufuata nyuma, basi ikabidi niwape jibu kwamba sisi ni kweli tunasafiri hatufuati parcel bali tunaelekea Zanzibar, ofisi za kikatia tiketi ni wapi?
Aisee, tulioga matusi stendi nzima iligeuka uwanja wa matusi, watu wengine wakabaki wanashangaa na kucheka!
 
Sasa mkuu sijaona tatizo hapo,wewe ulivutiwa na moja ya heading kwenye hilo gazeti tafsiri nyepesi ni yakuwa hukuwa umeisoma hiyo habari,sasa kuwa gazeti hilo ni toleo la lini unashangaza kudogo.
 
Back
Top Bottom