msnajo
JF-Expert Member
- Jan 20, 2011
- 3,067
- 1,136
Kwa wale waliofuatia ule mdahalo, tuliona mengi kwa kweli. Miongoni ni kuhusu kupindishwa kwa kanuni pamoja na wabunge wetu kukosa staha na uvumilivu kwa wenzao! Mama mmoja mchangiaji alimshauri Ndugai asipende kushindana na wabunge hasa pale wanapokuja juu dhidi ya jambo fulani, so Ndugai awe mpole. Ushauri ulikuwa mzuri ila wa upendeleo! Lissu nae alitakiwa awe mpole anapochangia hoja. Yeye naye asipende kushindana na wakuu wake, hii italeta ukomavu kiakili na kuokoa upotevu wa muda na hela kama tulivyoshuhudia kikao kilichopita ambapo kikao kiliahirishwa mara kadhaa kutokana na watu kutokuwa wavumilivu. Wao wanafurahi tu, ila sisi tuliowatuma tunateseka kutokana na matendo yao!!