Vita ya Chalamila dhidi ya madanguro Dar ina viashiria vya ubaguzi

Ukahaba mkoani Dar es Salaam na nchi hii kwa ujumla unafanyika kila mahali, sio katika madanguro ya Mwananyamala tu. Ukahaba unafanyika katika Lodges, Hoteli kubwa, maofisini kwa watu, katika magari na hadi nyumbani kwa watu.

Kwanini vita vya ukahaba hapa Dar vimelenga madanguro tu ya aina ya Mwananyamala ambayo yanaonekana ni ya masikini hoehahe wa kipato badala haya maeneo yote kwa ujumla?

Usawa katika kudhibiti ukahaba ulipasawa kujumuisha kutaka nyumba zote za kulala wageni hata hotel kubwa zisiruhusu mwanaume na mwanamke wasio na cheti cha ndoa kulala chumba kimoja, kupiga marufuku wanaume kuhonga katika mapenzi au kutoa pesa kwa wanawake wasio wake wa ndoa baada ya kufanya mapenzi.
Kwa ufupi unatetea madanguro
 
Kuna baadhi ya watanzania ni kama mapopoma!! Jitu zima linatetea madanguro na ukahaba, maeneo hayo yalikuwa ni hatarishi kwa usalama wa afya za akili na mwili kwa wakazi wa maeneo hayo.

Imagine mazingira ya hapo yanavyo onekana ni machafu na pia watu hao makahaba yalikuwa hayachagui rika la kuuza miili yao, watoto wadogo na wanafunzi,nao walikuwa ni wateja wao wakubwa.

Mitaa hio ilikuwa imegeuka jehanamu kwa matendo machafu yaliyokuwa yakifanyika hapo.

Tufike hatua tuunge mkono angalau juhudi kidogo serikali inayofanya, hivi ni namna gani watoto walikuwa wanaona watu wazima wakiuza miili yao mbele ya mazingira yao?

Serikali itunge sheria mmiliki yeyote wa nyumba au ardhi aliyegeuza nyumba yake au ardhi yake kufanyia biashara ya ukahaba na madanguro nyumba yake au ardhi yake itaifishwe iwe mali ya umma na eneo lijengwe bustani za michezo ya watoto au sehemu za kupumzikia wananchi.
 
MWALIMU NYERERE ALIMZUIA BALOZI JOSEPH RWEGASIRA KUWAONDOA MAKAHABA JIJINI DAR:

Tanzania imepitia simulizi nyingi zenye kusisismua lakini nyingi zikiwa hazisemwi sana kwenye vyombo vya habari na hivyo kupelekea vizazi vya sasa na vijavyo kutokujua mengi yaliyowahi kutokea na kuleta changamoto kubwa kwa baadhi ya viongozi serikalini, sambamba na kutekeleza mambo yao mbalimbali.

Mnamo mwaka 1980, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar wakati huo, Balozi Joseph Rwegasira alianzisha Operesheni maalum ya kuhakikisha Makahaba wote waliokuwa wakifanya biashara ya kuuza miili ndani ya Jiji hilo kuondoka haraka, sambamba na kutumia nguvu kuwaondoa wale wote ambao wangekaidi amri hiyo.

Operesheni hiyo ilikuwa imelenga kuwarudisha Makahaba waliopo Dar makwao, ili wakaendeleze kazi ya kulijenga taifa kupitia shughuli zao nyingine kama kilimo, ufugaji nk, na hivyo kuweza kusaidia kuimarisha vijiji vya ujamaa wakati wa Mpango wa Taifa wa kuiimarisha na kuendeleza Vijiji vya Ujamaa maarufu kama "Operesheni Vijiji".

Kufuatia uamuzi huo wa Balozi Rwegasira, aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alimuita Ikulu Balozi Rwegasira, akitaka aende akamfafanulie kuhusu utaratibu na madhumuni ya Operesheni ile.

Alipofika Ikulu, kauli ya kwanza ya Mwalimu ilimtumainisha kuwa huenda Operesheni yake iliungwa mkono pale alipohoji, “Nasikia umeamua kuwahamisha mama zangu warudi makwao wakalime maharagwe!” Rwegasira alijibu haraka kwa kusema, “Unajua Mwalimu, hatua yangu hii ni kutekeleza kaulimbiu yetu ya "Kilimo ni Uti wa Mgongo wa Taifa Letu", na Operesheni ya "Kilimo cha Kufa na Kupona" pengine hata kaulimbiu ya awali tuliyoiita, "Siasa ni Kilimo", ndipo nikaiona ni muafaka kabisa.

Hapo ndipo hoja ya Mwalimu iliyofuatia ilimshtua Rwegasira, pale aliposema, “Nimekuita unieleweshe ni watu wa aina gani ulioteua warudishwe makwao kwa utekelezaji huo, pia nataka kujua utaratibu unaotumika”.

Ndipo Baba wa Taifa aliishia kuhoji, “Kwa hiyo umewahukumu kwa ukahaba wao, au kuna sababu nyingine?” Hapo, Rwegasira alikaa kimya kwa kutokuwa na jibu muafaka! Hata hivyo, Baba wa Taifa aliendelea kudadisi kwa kuhoji, “Ikiwa umeamua kuwatimua makahaba, je, mazingira ya kule utakakowahamisha, umeyaandaaje?”

Kwa kuwa hoja ya Baba wa Taifa ilikuja kinyume na matarajio ya Rwegasira, isitoshe hakuelewa mwelekeo wa hoja ile, alibaki kimya, ndipo Mwalimu alimuamuru kwa kusema, “Ukiweza kutimiza hilo, njoo unieleze nibariki Operesheni yako!”

Aliongeza kwa kusema, “Kama usingekuwa mtani wangu wito wangu ungeishia hapa, lakini hebu nikufafanulie chanzo cha ukahaba, ndipo aliuliza iwapo Rwegasira anafahamu wateja wa makahaba ni kina nani, akawa amejibu kuwa ni wanaume! Mwalimu alicheka akamuuliza, “Wewe si mwanaume, je, huko waliko makahaba unakwenda?” Rwegasira alijibu, “Hapana!”

Mwalimu akahoji tena, “Mimi si mwanaume, je, huko naenda?” Rwegasira alijibu, “Hapana Mwalimu!” Ndipo alianza kumchambulia kuanzia wanaume wasiojua kumtaka mapenzi mwanamke, wasiotaka bughudha ya kutunza familia hivyo hawaoi, hata waliobarikiwa nguvu nyingi za mwili wakienda huko kuzipunguza ili wasisumbue wake zao.

Na hapo ndipo Mwalimu alifafanua hoja yake kwa Rwegasira akisema, “Nilipotaka nijue mazingira ya huko utakakowaondoa umeyaandaje, nilijua hao wateja wao wasipowakuta, matokeo ni kubakwa mama zetu, wake zetu, wanafunzi wetu, vilema wetu, hata vichaa wetu! Ndiyo maana katika miji yote duniani makahaba wapo!“

Mwalimu alimalizia kwa kumwambia Rwegasira ya kuwa, hata mataifa yaliyojigamba kuwa na utawala bora na wa sheria, yalishindwa kubuni sheria ya kutawala miili ya watu hususani wanawake hivyo kudhibiti ukahaba, pia michezo hatari kama ndondi na kareti, ikaishia kuhalalisha biashara zinazohusisha ukahaba kwa namna moja au nyingine, tena zikitozwa kodi ya mapato kwa Serikali.

Hatimaye Mwalimu alitaja kuhusishwa kwa ukahaba katika Maandiko Matakatifu, ambapo makahaba hawakuhukumiwa kwa ukahaba wao, isipokuwa walihimizwa wawe na matendo mema, sawa na walivyohimizwa watu wengine.

Alitoa mfano wa kahaba aliyemkimbilia Yesu alipokimbizwa na umati uliotaka wamponde mawe mpaka afe kama mila yao inavyoruhusu. Yesu aliuambia ule umati akisema, “Ikiwa miongoni mwenu kuna asiyepata kutenda mnalomtuhumu nalo, na awe wa kwanza kumtupia jiwe.

”Yesu alishusha macho kuendelea kuchora kielelezo chake, na alipoinua macho sekunde kadhaa baadaye, hakuona mtu hata mmoja! Ndipo alimuamuru yule kahaba akisema, “Inuka uende zako, kawe na matendo mema.“

Mwalimu alimhoji Rwegasira akisema, “Kwani Yesu alishindwa kumtamkia kahaba aache ukahaba?” Hapo ndipo Mwalimu alimtaja kahaba mwingine aliyemkuta Yesu mahali akifanyiwa karamu akamuangukia akilia, mpaka alimlowesha miguu na kumpangusa kwa nywele zake, akampaka manukato! Yesu alimuambia mwenyeji wake akisema: “Huyu mwanamke amekuzidi, kwa kuniosha miguu kama ilivyo desturi yetu, ambapo wewe hukufanya vile.“

Kwa msingi huu, Mwalimu alimtamkia Balozi Joseph Rwegasira akisema: “Kwa kupewa akili na Mwenyezi Mungu, mwanadamu hatahukumiwa kwa dhambi ya mwenziwe, ndipo kwa hali hiyo, litatimilika agizo la Mwenyezi Mungu kuwa, "Usihukumu mwenzio, ndipo nawe hutahukumiwa."

Nini maoni yako juu ya mtazamo huu wa baba wa Taifa, Mwalim Nyerere dhidi ya biashara hii kongwe??
 
Dah!mkuu umeandika hadi asiejua anapata kujua itoshe kusema tuuh
MWENYE KUSIKIA NA ASIKIE
Big up mkuu💪🏿
 
Nimesikitika pale aliposema watoto wadogo wa shule wanaenda huko pia, na lingine ni uchafu uliopo hapo unatisha naona wanaishi na kila aina ya uchafu na panya wamejaa

Tatizo letu tunamshambulia mtu badala ya kuangalia hali yenyewe
Ukahaba upo duniani kote watu wanaenda mpaka Spain na Brazil kote kutafuta Malaya

Lakini wanatofautiana hawa wa kwetu ni bora ya wanyama
Hawa ni kuwafunda na akionekana na mtoto fine 1m
Kerb crawler wakamatwe tena hao ndio wabaya ila wenye anuani sawa
 
MWALIMU NYERERE ALIMZUIA BALOZI JOSEPH RWEGASIRA KUWAONDOA MAKAHABA JIJINI DAR:

Tanzania imepitia simulizi nyingi zenye kusisismua lakini nyingi zikiwa hazisemwi sana kwenye vyombo vya habari na hivyo kupelekea vizazi vya sasa na vijavyo kutokujua mengi yaliyowahi kutokea na kuleta changamoto kubwa kwa baadhi ya viongozi serikalini, sambamba na kutekeleza mambo yao mbalimbali.

Mnamo mwaka 1980, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar wakati huo, Balozi Joseph Rwegasira alianzisha Operesheni maalum ya kuhakikisha Makahaba wote waliokuwa wakifanya biashara ya kuuza miili ndani ya Jiji hilo kuondoka haraka, sambamba na kutumia nguvu kuwaondoa wale wote ambao wangekaidi amri hiyo.

Operesheni hiyo ilikuwa imelenga kuwarudisha Makahaba waliopo Dar makwao, ili wakaendeleze kazi ya kulijenga taifa kupitia shughuli zao nyingine kama kilimo, ufugaji nk, na hivyo kuweza kusaidia kuimarisha vijiji vya ujamaa wakati wa Mpango wa Taifa wa kuiimarisha na kuendeleza Vijiji vya Ujamaa maarufu kama "Operesheni Vijiji".

Kufuatia uamuzi huo wa Balozi Rwegasira, aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alimuita Ikulu Balozi Rwegasira, akitaka aende akamfafanulie kuhusu utaratibu na madhumuni ya Operesheni ile.

Alipofika Ikulu, kauli ya kwanza ya Mwalimu ilimtumainisha kuwa huenda Operesheni yake iliungwa mkono pale alipohoji, “Nasikia umeamua kuwahamisha mama zangu warudi makwao wakalime maharagwe!” Rwegasira alijibu haraka kwa kusema, “Unajua Mwalimu, hatua yangu hii ni kutekeleza kaulimbiu yetu ya "Kilimo ni Uti wa Mgongo wa Taifa Letu", na Operesheni ya "Kilimo cha Kufa na Kupona" pengine hata kaulimbiu ya awali tuliyoiita, "Siasa ni Kilimo", ndipo nikaiona ni muafaka kabisa.

Hapo ndipo hoja ya Mwalimu iliyofuatia ilimshtua Rwegasira, pale aliposema, “Nimekuita unieleweshe ni watu wa aina gani ulioteua warudishwe makwao kwa utekelezaji huo, pia nataka kujua utaratibu unaotumika”.

Ndipo Baba wa Taifa aliishia kuhoji, “Kwa hiyo umewahukumu kwa ukahaba wao, au kuna sababu nyingine?” Hapo, Rwegasira alikaa kimya kwa kutokuwa na jibu muafaka! Hata hivyo, Baba wa Taifa aliendelea kudadisi kwa kuhoji, “Ikiwa umeamua kuwatimua makahaba, je, mazingira ya kule utakakowahamisha, umeyaandaaje?”

Kwa kuwa hoja ya Baba wa Taifa ilikuja kinyume na matarajio ya Rwegasira, isitoshe hakuelewa mwelekeo wa hoja ile, alibaki kimya, ndipo Mwalimu alimuamuru kwa kusema, “Ukiweza kutimiza hilo, njoo unieleze nibariki Operesheni yako!”

Aliongeza kwa kusema, “Kama usingekuwa mtani wangu wito wangu ungeishia hapa, lakini hebu nikufafanulie chanzo cha ukahaba, ndipo aliuliza iwapo Rwegasira anafahamu wateja wa makahaba ni kina nani, akawa amejibu kuwa ni wanaume! Mwalimu alicheka akamuuliza, “Wewe si mwanaume, je, huko waliko makahaba unakwenda?” Rwegasira alijibu, “Hapana!”

Mwalimu akahoji tena, “Mimi si mwanaume, je, huko naenda?” Rwegasira alijibu, “Hapana Mwalimu!” Ndipo alianza kumchambulia kuanzia wanaume wasiojua kumtaka mapenzi mwanamke, wasiotaka bughudha ya kutunza familia hivyo hawaoi, hata waliobarikiwa nguvu nyingi za mwili wakienda huko kuzipunguza ili wasisumbue wake zao.

Na hapo ndipo Mwalimu alifafanua hoja yake kwa Rwegasira akisema, “Nilipotaka nijue mazingira ya huko utakakowaondoa umeyaandaje, nilijua hao wateja wao wasipowakuta, matokeo ni kubakwa mama zetu, wake zetu, wanafunzi wetu, vilema wetu, hata vichaa wetu! Ndiyo maana katika miji yote duniani makahaba wapo!“

Mwalimu alimalizia kwa kumwambia Rwegasira ya kuwa, hata mataifa yaliyojigamba kuwa na utawala bora na wa sheria, yalishindwa kubuni sheria ya kutawala miili ya watu hususani wanawake hivyo kudhibiti ukahaba, pia michezo hatari kama ndondi na kareti, ikaishia kuhalalisha biashara zinazohusisha ukahaba kwa namna moja au nyingine, tena zikitozwa kodi ya mapato kwa Serikali.

Hatimaye Mwalimu alitaja kuhusishwa kwa ukahaba katika Maandiko Matakatifu, ambapo makahaba hawakuhukumiwa kwa ukahaba wao, isipokuwa walihimizwa wawe na matendo mema, sawa na walivyohimizwa watu wengine.

Alitoa mfano wa kahaba aliyemkimbilia Yesu alipokimbizwa na umati uliotaka wamponde mawe mpaka afe kama mila yao inavyoruhusu. Yesu aliuambia ule umati akisema, “Ikiwa miongoni mwenu kuna asiyepata kutenda mnalomtuhumu nalo, na awe wa kwanza kumtupia jiwe.

”Yesu alishusha macho kuendelea kuchora kielelezo chake, na alipoinua macho sekunde kadhaa baadaye, hakuona mtu hata mmoja! Ndipo alimuamuru yule kahaba akisema, “Inuka uende zako, kawe na matendo mema.“

Mwalimu alimhoji Rwegasira akisema, “Kwani Yesu alishindwa kumtamkia kahaba aache ukahaba?” Hapo ndipo Mwalimu alimtaja kahaba mwingine aliyemkuta Yesu mahali akifanyiwa karamu akamuangukia akilia, mpaka alimlowesha miguu na kumpangusa kwa nywele zake, akampaka manukato! Yesu alimuambia mwenyeji wake akisema: “Huyu mwanamke amekuzidi, kwa kuniosha miguu kama ilivyo desturi yetu, ambapo wewe hukufanya vile.“

Kwa msingi huu, Mwalimu alimtamkia Balozi Joseph Rwegasira akisema: “Kwa kupewa akili na Mwenyezi Mungu, mwanadamu hatahukumiwa kwa dhambi ya mwenziwe, ndipo kwa hali hiyo, litatimilika agizo la Mwenyezi Mungu kuwa, "Usihukumu mwenzio, ndipo nawe hutahukumiwa."

Nini maoni yako juu ya mtazamo huu wa baba wa Taifa, Mwalim Nyerere dhidi ya biashara hii kongwe??
Nyerere alikuwa mtu pragmatic na rational sana.
 
Ukahaba mkoani Dar es Salaam na nchi hii kwa ujumla unafanyika kila mahali, sio katika madanguro ya Mwananyamala tu. Ukahaba unafanyika katika Lodges, Hoteli kubwa, maofisini kwa watu, katika magari na hadi nyumbani kwa watu.

Kwanini vita vya ukahaba hapa Dar vimelenga madanguro tu ya aina ya Mwananyamala ambayo yanaonekana ni ya masikini hoehahe wa kipato badala haya maeneo yote kwa ujumla?

Usawa katika kudhibiti ukahaba ulipasawa kujumuisha kutaka nyumba zote za kulala wageni hata hotel kubwa zisiruhusu mwanaume na mwanamke wasio na cheti cha ndoa kulala chumba kimoja, kupiga marufuku wanaume kuhonga katika mapenzi au kutoa pesa kwa wanawake wasio wake wa ndoa baada ya kufanya mapenzi.
Umeanza kukosa wateja hapo kwa manyanya mkuu?
 
Yaan umeharibu hapo maswala ya Chet cha Ndoa.

Ukitaka vita ipiganwe hapa Mjini waweke huo utaratibu.
Naona umehamaki!!!

Nenda hotel za kikatoliki au Lutheran kama utaingia na mwanamke bila kuwa na cheti Cha NDOA😀😀

Tendo la NDOA ni Kwa wanandoa pekee!!

Mwaka huu wote wenye kukataa NDOA mtaoa HAKIKA!!
 
Ukahaba mkoani Dar es Salaam na nchi hii kwa ujumla unafanyika kila mahali, sio katika madanguro ya Mwananyamala tu. Ukahaba unafanyika katika Lodges, Hoteli kubwa, maofisini kwa watu, katika magari na hadi nyumbani kwa watu.

Kwanini vita vya ukahaba hapa Dar vimelenga madanguro tu ya aina ya Mwananyamala ambayo yanaonekana ni ya masikini hoehahe wa kipato badala haya maeneo yote kwa ujumla?

Usawa katika kudhibiti ukahaba ulipasawa kujumuisha kutaka nyumba zote za kulala wageni hata hotel kubwa zisiruhusu mwanaume na mwanamke wasio na cheti cha ndoa kulala chumba kimoja, kupiga marufuku wanaume kuhonga katika mapenzi au kutoa pesa kwa wanawake wasio wake wa ndoa baada ya kufanya mapenzi.
Jamaa wewe unakali nyingi sana ...wote wanakumpinga hawana logic ..sijapaona popote unatetea madanguro au ukahaba ila unasema kuwe usawa...mfano ukamataja wa wazurulaji mida ya usiku wakati polisi wana deal watembea kwa miguu wakati wa kwenye magari wana wacha tuu...No fairness at all.Tz vijana wengi akili ime eroded.
 
Kuna baadhi ya watanzania ni kama mapopoma!! Jitu zima linatetea madanguro na ukahaba, maeneo hayo yalikuwa ni hatarishi kwa usalama wa afya za akili na mwili kwa wakazi wa maeneo hayo.

Imagine mazingira ya hapo yanavyo onekana ni machafu na pia watu hao makahaba yalikuwa hayachagui rika la kuuza miili yao, watoto wadogo na wanafunzi,nao walikuwa ni wateja wao wakubwa.

Mitaa hio ilikuwa imegeuka jehanamu kwa matendo machafu yaliyokuwa yakifanyika hapo.

Tufike hatua tuunge mkono angalau juhudi kidogo serikali inayofanya, hivi ni namna gani watoto walikuwa wanaona watu wazima wakiuza miili yao mbele ya mazingira yao?

Serikali itunge sheria mmiliki yeyote wa nyumba au ardhi aliyegeuza nyumba yake au ardhi yake kufanyia biashara ya ukahaba na madanguro nyumba yake au ardhi yake itaifishwe iwe mali ya umma na eneo lijengwe bustani za michezo ya watoto au sehemu za kupumzikia wananchi.
Kweli mkuu wa mkoa anakanyaga milango akisaka madanguro kweli, hii kazi si ingefanywa na mtendaji wa kata na wdc yake, hata dc na meya hiyo kazi imemshinda kweli? Hao waandishi walilipwa shs ngapi kwa hiyo movie? Walikuwepo akina detopile chipungahero makamba sr wote walihangaika na hayo makahaba na hawajafanikiwa sasa yeye anakuja na muujiza gani?

kuna rpc aliwapiga risasi ya makalio wasasambuaji na hawakuacha.

Rc anapaswa ashughulikie maandalizi ya madarasa na madawati ya form one watakao anza januari,
 
Back
Top Bottom