Vita ya Chalamila dhidi ya madanguro Dar ina viashiria vya ubaguzi

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,620
46,261
Ukahaba mkoani Dar es Salaam na nchi hii kwa ujumla unafanyika kila mahali, sio katika madanguro ya Mwananyamala tu. Ukahaba unafanyika katika Lodges, Hoteli kubwa, maofisini kwa watu, katika magari na hadi nyumbani kwa watu.

Kwanini vita vya ukahaba hapa Dar vimelenga madanguro tu ya aina ya Mwananyamala ambayo yanaonekana ni ya masikini hoehahe wa kipato badala haya maeneo yote kwa ujumla?

Usawa katika kudhibiti ukahaba ulipasawa kujumuisha kutaka nyumba zote za kulala wageni hata hotel kubwa zisiruhusu mwanaume na mwanamke wasio na cheti cha ndoa kulala chumba kimoja, kupiga marufuku wanaume kuhonga katika mapenzi au kutoa pesa kwa wanawake wasio wake wa ndoa baada ya kufanya mapenzi.
 
Hilo la Mwananyamala ni suala la muda tu linahamishiwa kwingine au hapohapo maana hizo ni nyumba za watu na hivyo vyumba hao madada wanalipa kodi.

Labda mwenye eneo aamue kuliuza au kubadili matumizi kabisa.
 
Mwambieni Chalamila asiwaonee maskini wanaochukua buku tatu kwa raundi ya kawaida na tano huko kwingine.

Kama yeye mlume kweli a deal na wanaofanya kwenye mtandao na wa barabarani wanaouzia kwenye chocho au kwa babu.
 
Back
Top Bottom