Vita kati ya Seif na Hamad Rashid yaibukia Manzese

Tanganyika hatuhitji siasa za vyama viwili kama kule Zanzibar, huku Tanganyika tunahitaji Demokrasia ya kweli na sio Chadema na CCM peke yao wahodhi siasa za Tanganyika. Big no!

bora umeliona na kuliongea hili mkuu
 
Maalim seif sio mwenzao tena,siku hz anatembea na ving'ora mwenzao anapata huduma swafi.Ya nn aanze kujihangaisha na kuzunguka majukwaani wakati yuko kwenye kiti cha juu.Wakimsumbua sana atahamia airtel-ccm na hapo ndo mwisho wa cuf
 
Haka kamgogoro kamepikwa na ccm na baadhi ya mashabiki wa cdm wanashangilia, jamani mnafurahia upinzani unapodhoofika?
CUF ni chama tawala mkuu acha kupotosha watu hapa JF, na ndio maana siku zote wao wanacheza mdundiko na CCM kama pale walipopitisha muswada wa katiba mpya kesho yake wanataka kumuona JK ikulu.
Ni vigumu kujuwa CUF sasa hivi wanacheza sindimba gani, yaani kwishney!!
 
Mtatiro anatumia akili, anafaidi yale marupurupu yao, ikifika 2014 watapata taarifa redioni na Tv kuwa yuko Chadema. Subiri uone.
 

hivi julius mtatiro bado hajui kwamba huu ni muafaka wa kujikweza katika medani ya siasa ndani ya cuf kwa huku bara?

huu ugomvi mkali kati ya wapemba wawili -- yaani maalim seif na hamad rashid mohamed ni muafaka mzuri sana kwa mtatiro kunyakuwa nafasi na kujipambanua katika cuf kukitetea chama kutokana na jinsi kinavyodidimia upande wa bara.

anachotakiwa kufanya ni mara moja kutoa tamko la kumuunga mkono hamad rashi mohamed, hasa katika kauli yake kwamba cuf imepoteza mvuto bara na kinatakiwa kifanye mabadiliko makubwa kiuongozi.

mimi nadhani hata prof lipumba hatimaye angemuunga mkono mtatiro – na hapo ndiyo ingekuwa mwisho wa seif.

au mnasemaje wadau?

angalizo: Mimi si mfuasi wa cuf – natoa tu ushauri.

laiti huyu mtatiro maneno haya labda angeambiwa na mama yake angeelewa!!nashindwa kumuelewa huyu jamaa!!
 
Wewe huijui CUF na Maalim Seif vizuri.
Seif aliweza kumtimua muasisi mwenza wa CUF Bw. James Mapalala, sembuse Rashid.
Yaani kwa Seif hata Lipumba mwenye hapindui, so usimchuuze Mtatiro bure.
Wazo la kumsaidia Mtatiro labda ungemshauri aje Chadema tuimarishe upinzani!!
 
Ktk gazeti la Leo la Nipashe nimesoma habari ya mapambano ya wazi kati ya Maalim Seif na Hamad Rashid. Mapambano hayo yalisababisha Hamad Rashid kuahirisha kikao chake Manzese baada ya mkutano wake kuvunjwa na mabaunsa. Mabaunsa hao hawajulikani walikotoka. Mtatiro alipoulizwa alisema hajui kama Hamad Rashid yuko Manzese, na hana taarifa ya mkutano wake. Halafu akasema Kiongozi mkubwa kama Hamada Rashid hawezi kwenda Manzese bila kutoa taarifa.
Kwa maoni yangu Mtatiro amekosea. Heri angemuunga mkono Hamad Rashid. Nadhani CUF inaenda kubaya.
 
mtatiro hawezi mtihani ulikuwa igunga amepoteza kura 9,000 ,,,,,,,hoja yako haina tija jadili issues za maendeleo wacha kuleta hoja za mtu binafsi
 
Ktk gazeti la Leo la Nipashe nimesoma habari ya mapambano ya wazi kati ya Maalim Seif na Hamad Rashid. Mapambano hayo yalisababisha Hamad Rashid kuahirisha kikao chake Manzese baada ya mkutano wake kuvunjwa na mabaunsa. Mabaunsa hao hawajulikani walikotoka. Mtatiro alipoulizwa alisema hajui kama Hamad Rashid yuko Manzese, na hana taarifa ya mkutano wake. Halafu akasema Kiongozi mkubwa kama Hamada Rashid hawezi kwenda Manzese bila kutoa taarifa.
Kwa maoni yangu Mtatiro amekosea. Heri angemuunga mkono Hamad Rashid. Nadhani CUF inaenda kubaya.

Hamad ataungwa mkono pale v atakapotubu kwa tundu Lissu
 
Hii ndoa ilikuwa na walakini toka mwanzo!!! Huu si muelekeo mzuri. Naungana na mdau mmoja aliyeomba kwa Mungu ainusuru nyumba ya jirani yake hata kama ni mchawi!!
 
Hamadi rashidi kama namuon vile.....huyoooooooooooooooo aanakatiza chalinze,segera,mombo,same,njia panda ya hima,moshi,machame.........antua hai kuchukua kadi ya chama cha kususa na kuandamana,hamna lia,yeye si alikua anachekelea prof safari alivyokuwa anadhalilishwa kwa kujaribu kutumia haki yake kugombe uenyekiti?sema chadema hamad rashid bonge la mtaji,atawasaidia kufuta ile propaganda ya wapinzani wenu jamaa wa magamba kwamabchama chenu ni cha kanisa,ikiungana na profesa safari na mzee said arfi na toto lenu tundu zitto kabwe,magamba kimyaaaaaaa!

Hamad ana uchu wa madaraka,CDM hatumtaki kabisaaaaaaaaaaaa
 
kiongozi wa cuf juma duni anasema huyo hamadi rashidi anayesema kuwa malimu seif amechoka kiafya eti anavyuma vingi mwilini!mbona yeye rashidi anavyo vingi zaidi?na kama ni uzee mbona yeye ndio mzee zaidi?kwa hali hii tutegemee mengi.
 
Mabaunsa hao hawajulikani walikotoka.
Kwa maoni yangu Mtatiro amekosea. Heri angemuunga mkono Hamad Rashid.

Hao ni Blue Guards.

Mie namuunga mkono Mtatiro hasa hii reply yake:
NANUKUU:
“tuna utaratibu wa ziara za viongozi wetu waandamizi ndani ya chama, yaani wabunge, wawakilishi, wajumbe wa baraza kuu na kwamba wanapofanya ziara yoyote iliyo nje ya maeneo yao, hupaswa watoe taarifa kwenye Ofisi ya Katibu Mkuu. Utaratibu huu, hata mheshimiwa Rashid anaufahamu. Ofisi ya Katibu Mkuu haikuwa na taarifa ya ziara hiyo,”

Mie simuungi mkono Hamad kwa sababu hajafata utaratibu wa chama chake.
 
Back
Top Bottom