Viongozi wetu wanapofanya makosa ya wazi waishie tu kuomba msamaha kisha 'life as usual', au tujenge utamaduni wa kuwajibika kama enzi za Nyerere?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,504
113,620
Wanabodi,

Kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", ambazo huwa na swali, kisha hoja, halafu jibu utajibu wewe msomaji.

Naomba kuanza kwa Declaration of Interest.

Kwa vile mimi ni mmoja wa waandishi wa habari, tuliwahi kuitwa mbele ya Kamati ya Bunge na kusulubiwa, naomba bandiko hili, lisichukuliwe kuwa ni hit back. Mimi nimewahi kuandika sana kuhusu uwajibikaji na mambo ya watu kuombana misamaha batili Psychoanalysis ya Waomba Msamaha Kwa Rais, Makamba Snr is the Next, Membe Will Never for Pride, Kiburi na Jeuri, Kinana Will Never for Integrity

Hili ni bandiko la swali.

Kwa kadri ya siku zinavyokwenda, wale watu wa Nyerere wanazidi kupungua, katika generation hii iliyopo, waliokuwa wanaujua utawala wa Mwalimu Nyerere ni wachache, wengi ni new generation ya utawala wa Mwinyi, Mkapa, JK, na JPM, hivyo inawezekana kabisa, wengi wasielewe kuwa enzi za Nyerere, viongozi wetu, walipofanya makosa ya wazi, sio tuu waliomba msamaha, bali msamaha huo uliandamana na barua ya kuwajibika, hivyo nauliza, kwa viongozi wetu hawa wa sasa, pale wanapofanya makosa ya wazi kabisa, tuwaache waombe tuu msamaha na life kuendelea as usual, au sasa tujenge utamaduni wa viongozi kuwajibika kwa makosa yao, na wasiishie kuomba tuu msamaha, tena misamaha mingine ni misamaha batili kwa kutoa visingizio, vya eti nilinukuliwa vibaya!, bali msamaha uandamane na barua ya kuwajibika, kama enzi za Nyerere?.

Naomba kwanza niwaonyeshe msamaha wa enzi za Nyerere,
Barua ya Mwinyi Kujiuzulu.jpeg

Na kwa msiofahamu kisa hiki, sio Waziri Mwinyi pekee alijiuzulu, Rashidi Kawawa aliondolewa kwenye umakamo wa pili wa rais. Waziri wa Usalama wa Taifa, Peter Siyovelwa alijiuzulu.
Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Emelio Mzena Alistaafishwa, IGP, Samuel Pundugu Alistaafishwa, Kamisha Mkuu wa Magereza Alistaafishwa. Kisha ngoma ikahamia Mwanza, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Peter Kisumo, alimwaga unga. RPC, RSO, OCD na DSO wa Mwanza sio tuu walimwaga unga, bali walifikishwa kwa Pilato na wote wakala mvua nyingi, isipokuwa mshitakiwa mmoja tuu, aliyekuwa anatetewa na wakili mahiri, Murtaza Lakha, ndie alinusurika.

Hivyo jee mnaonaje, huu msamaha ulioombwa leo live kwenye TV, pia uandamane na barua rasmi ya kuomba msamaha wa kweli, ukiandamana na kuwajibika?, au msamaha tuu unatosha?.

Hii Video Clip Inayosambaa

Mimi ni mtu wa Audio Visual, hivyo nikiangalia tuu a video clip, naweza kujua kama imefanyiwa makeke au laa. Hii video clip ni Bonafide Genuine, toka kwa a trusted source, haijafanyiwa makeke yoyote!.

Kwa msiojua mambo ya Audio/Video. Kila ukirekodi video, unapobonyeza kitufe cha record na kuanza ukirekodi, kile unachorekodi kinaitwa shots. Kila ukirekodi pose au ku stop, halafu inaendelea kurekodi unakuwa una change shots. Hivyo mtu ukiitazama video iliofanyiwa makeke, utanotice ama ina kitu kinachoitwa jump cuts, ama inawekewa cuts aways ili kuziba jump cuts. Video yetu hii imepigwa kwa single shot, maana yake anayerekodi alibonyeza record mara moja tuu, hakuchange shot yoyote wala kuingiza cut aways zozote, the video is smooth, simless , hivyo alichozungumza mzungumzaji hayo aliyozungumza ni maneno yake mwenyewe halisi. Hajalishwa maneno yoyote wala hii video, haijafanyiwa makeke yoyote!.

Jee Wajua Kuna Msamaha Batili, Msamaha Batilifu na Msamaha wa Kweli ?.
Sii wengi wanaojua kuna msamaha ya kweli, batili na misamaha batilifu.
Msamaha wa kweli ni pale mtu unakosa, kwanza kwa kukubali kosa, pili kujutia kosa, tatu kuomba msamaha wa dhati na mwisho ku take responsibility kwa kuwajibika kwa kubeba the consequences ya matokeo ya makosa yako, kwa kupisha ofisi ya umma kupunguza embarasment caused.

Msamaha batili ni pale mtu umekosa, badala ya kukiri kosa, unatafuta visingizio kwa kutafuta the scapegoat to shift the blame kwa wengine kwa kudai au umenukuliwa vibaya au video clip imefanyiwa maujanja!.
Msamaha Batilifu ni msamaha batili ambao ule ubatili unaweza kuondosheka na kugeuka ni msamaha wa kweli. Ule msamaha uliombwa na Spika, ni msamaha batilifu, wenye ubatili wa kusingizia kuwa Ile video inayosaamba, imetengenezwa kwa kuunga unga, kitu ambacho sio kweli!.
Ile video ni bonafide genuine, haijafanyiwa maujanja yoyote, hivyo hayo matamshi, ni matamshi halisi ya mhusika. Kuomba msamaha kwa kutafuta kusingizio chochote, ni kuomba msamaha batili wenye ubatilifu.

Ubatili kwenye msamaha huu unaweza kuondosheka kwa Spika kuchutama tuu na kukiri ni kweli ni yeye na aliyasema hayo kwa kughafilika tuu, na asitafute visingizio.

Kwa mlioisikiliza hiyo video, jee kuomba tuu msamaha kunatosha, au pia awajibike?.

Paskali
 
Hakuna kosa lolote alilofanya Ndugai kila mwananchi anahoji hela ya tozo inaenda wapi?

Selling point ya tozo wakati inaletwa na waziri Nchemba ilikuwa hizo hela zinaenda kujenga madarasa na zahanati, je imekuwaje tena tukakopa trillion 1.3 kujenga madarasa?
 
Hilo ndilo tatizo lake kubwa. Ndugai hana mshipa wa kuchuja pumba na mchele. Kwa waliowahi kuface one on one na Ndugai wanajua ninachosema.

Ukiona profile ya Speaker tuliyenaye, unaanza kujiuliza kuwa hawa watu wanapatikanaje? Je kweli hakukuwa na mtanzania mwingine mwenye credibility, maturity na wisdom zaidi ya Ndugai?

#KatibaMpyaNiMuhimu
 
Shida ni kwamba ndani ya CCM hakuna aliye msafi wa kumnyooshea kidole mwenzake hivyo huu utamaduni wa kujiuzuru kwa kuwajibika usitegemee utaendelea kuwepo.

Ni wazi kwamba spika alikosea sana, Rais amevaa kofia mbili na hii ndio tumekuwa tukilalamikia pia, amevaa kama Mwenyekiti wa chama na pia boss mkuu wa nchi.

Sasa spika kwa namna yeyote hawezi kumsema Rais sababu akienda kwenye chama ni boss wake na akirudi kwenye serikali ni boss wake.

Back to the point ni kwamba, ndani ya CCM hakuna wa kumuita mwenzake na kumwambia ajiuzuru sababu wote hawana moral authority ya kumsema mwenzake.

Unaweza kuona kabisa msimamo wa spika upo wapi hata kama ameomba msamaha wa kinafiki, dhamira na ujasiri uliomtuma kuongea vile haviwezi kuondoka, tatizo ni nani sio mnafiki ndani ya CCM???

Hata Samia alijinafikisha kwa Magufuli, sisemi Magufuli alikuwa mtu wa maana sana Ila nakazia hoja ya nani amfunge chui kengele??? Wote wanafiki na wanaishi kwa huo unafiki na ndio maana spika amejikuta anaropoka na yakamfika mwenyewe.

Hata akina nape walijinafikisha Ila mwishowe wakaumbuka, sasa Magufuli alikuwa mtemi ndio maana aliwanyoosha sio kwamba alikuwa msafi maana nae alijinafikisha kwa Kikwete.

So mwisho wasiku unakuja kutambua kwamba maisha ya wanasiasa wa Tanzania yamekaa unafiki ndio maana hakuna wa kumwajibisha mwenzie.
 
Wanabodi,
Hili ni bandiko la swali.

Kwa kadri ya siku zinavyokwenda, wale watu wa Nyerere wanazidi kupungua, katika generation hii iliyopo, waliokuwa wanaujua utawala wa Mwalimu Nyerere ni wachache, wengi ni new generation ya utawala wa Mwinyi, Mkapa, JK, na JPM, hivyo inawezekana kabisa, wengi wasielewe kuwa enzi za Nyerere, viongozi wetu, walipofanya makosa ya wazi, sio tuu waliomba msamaha, bali msamaha huo uliandamana na barua ya kuwajibika, hivyo nauliza, kwa viongozi wetu hawa wa sasa, pale wanapofanya makosa ya wazi kabisa, tuwaache waombe tuu msamaha na life kuendelea as usual, au sasa tujenge utamaduni wa viongozi kuwajibika kwa makosa yao, na wasiishie kuomba tuu msamaha, tena misamaha mingine ni misamaha batili kwa kutoa visingizio, vya eti nilinukuliwa vibaya!, bali msamaha uandamane na barua ya kuwajibika, kama enzi za Nyerere?.
Inaendelea...
Paskali
Kwa kuomba radhi Spika amejishusha sana.
Na tunafahamu Ndugai anavyo penda pride.
Kwenye hili swala pride yake imekuwa shaken, maana Mama Samia zaidi ya kukanusha allegations kwenye clip yake , hitmen were going for the kill!
Kwa kuomba radhi ameondoa kiwingu.
 
Wanabodi,
Hili ni bandiko la swali.

Kwa kadri ya siku zinavyokwenda, wale watu wa Nyerere wanazidi kupungua, katika generation hii iliyopo, waliokuwa wanaujua utawala wa Mwalimu Nyerere ni wachache, wengi ni new generation ya utawala wa Mwinyi, Mkapa, JK, na JPM, hivyo inawezekana kabisa, wengi wasielewe kuwa enzi za Nyerere, viongozi wetu, walipofanya makosa ya wazi, sio tuu waliomba msamaha, bali msamaha huo uliandamana na barua ya kuwajibika, hivyo nauliza, kwa viongozi wetu hawa wa sasa, pale wanapofanya makosa ya wazi kabisa, tuwaache waombe tuu msamaha na life kuendelea as usual, au sasa tujenge utamaduni wa viongozi kuwajibika kwa makosa yao, na wasiishie kuomba tuu msamaha, tena misamaha mingine ni misamaha batili kwa kutoa visingizio, vya eti nilinukuliwa vibaya!, bali msamaha uandamane na barua ya kuwajibika, kama enzi za Nyerere?.
Inaendelea...
Paskali
Mimi nadhani kiongozi anapofanya kosa la wazi aombe msamaha na pia barua ya kuwajibika ifuate hii italeta nidhamu kwa Viongozi.
 
Wanasiasa wa Tz ni ngumu kujiuzulu, ndiyo maana hawana misimamo, leo anaamini hiki kesho anaamini kile ilimradi tu kitumbua chake hakiingii mchanga.......
 
Uwajibikaji?? Ulizikwa enzi za Mwalimu na sio sasa, kwasasa ni nyenyekea, jipendekeze, tubu, sifu, abudu ili tu mkono wako uende kinywani na si vinginevyo. Yaaan!
Wanabodi,
Hili ni bandiko la swali.

Kwa kadri ya siku zinavyokwenda, wale watu wa Nyerere wanazidi kupungua, katika generation hii iliyopo, waliokuwa wanaujua utawala wa Mwalimu Nyerere ni wachache, wengi ni new generation ya utawala wa Mwinyi, Mkapa, JK, na JPM, hivyo inawezekana kabisa, wengi wasielewe kuwa enzi za Nyerere, viongozi wetu, walipofanya makosa ya wazi, sio tuu waliomba msamaha, bali msamaha huo uliandamana na barua ya kuwajibika, hivyo nauliza, kwa viongozi wetu hawa wa sasa, pale wanapofanya makosa ya wazi kabisa, tuwaache waombe tuu msamaha na life kuendelea as usual, au sasa tujenge utamaduni wa viongozi kuwajibika kwa makosa yao, na wasiishie kuomba tuu msamaha, tena misamaha mingine ni misamaha batili kwa kutoa visingizio, vya eti nilinukuliwa vibaya!, bali msamaha uandamane na barua ya kuwajibika, kama enzi za Nyerere?.
Inaendelea...
Paskali

IMG_20211029_105959.jpg
 
Back
Top Bottom