Viongozi wastaafu achaneni na Siasa...!

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,725
Wakuu,
Je hapa tunaweza kujifunza kitu?

Nilikuwa namsikiliza Mzee Butiku kwenye kipindi cha This Week In Perspective juzi, alisema kuwa mtu yeyote mstaafu aliyekuwa Kiongozi Mwandamizi Serikalini asiingizwe kwenye NEC na Halmashauri Kuu Ya CCM, hapo akimaanisha akina Mwinyi, Mkapa, Lowassa, Warioba, Msuya, Malecela na wengineo.

Alisema watu wa aina hii wametoa michango yao tayari kwa serikali na wamechoka, hivyo wawachie wengine wenye mawazo mapya ili waingie na mawazo mapya ya kukikwamua chama, wao wabaki kama 'wazee' tu, na wataheshimiwa na kuombwa ushauri.

Kwa Mtazamo tu, je hawa wazee watakubaliana na wazo la Butiku?
Na je wazo la namna hii ni 'viable' kwa uhai wa chama chochote, mbali ya ccm?

My Take:
Mzee huyu yuko sahihi. Ku'maintain wazee waliotumikia kwa miongo kwenye nafasi za maamuzi ya juu ya vyama kunaziba uwezekano wa mabadiliko na maamuzi magumu.
 
Kuunda baraza la wazee (viongozi wastaafu) ni strategy ya kuwanyamazisha maana siku za karibuni imeonekana viongozi wastaafu wakipata ujasiri wa kukosoa baadhi ya maamuzi ya serikali (kuongea nje ya utaratibu wa chama). Wakiundiwa baraza lao, itawalazimu (watalazimika) kuongea mambo hayo behind closed doors, na hivyo hakuna atakayejua maoni yao, isipokuwa viongozi wa juu wa chama tu. Kwasasa serikali haiwezi kuvumilia makombora yanayoruka kutoka kila upande.
 
Mkuu,
Aksante!
Hii approach ya kuwaundia baraza unayoongelea sidhani kama inaweza kuwa effective kwa 'era' hii...si umeona Umoja Wa Vijana (CCM)jinsi wanavyoibuka katika muda usiotarajiwa na kumwaga sumu ndani na nje ya chama?..The same is bound to happen kutoka Baraza la Wazee!
 
Namuunga mkono Butiku kuwa hawa wazee waliokuwa viongozi wa juu wa chama na serikali si busara kuendelea kuwa wajumbe wa vikao vya chama vinavyotoa maamuzi kwani wakati mwingine wanakuwa na personal interests zao zinazowafanya wajumbe wasijadili kwa uwazi kwa sababu ya uwepo wao; mfano ni wakati wa uteuzi wa majina ya kugombea nafasi za uongozi kama vile urais hapo ndipo huweza kutumia influence zao ili watoto wao wapate nafasi za uongozi!! Kuwapo kwao kwenye vikao vya maamuzi vya chama kunaashiria kulea tabia za kisultani/kimangi!! Waundiwe baraza lao la ushauri na huko ndio watoe madukuduku yao kama yapo!!
 
Butiku anasema mambo hayo sababu ajapewa CHEO. Na akipewa Cheo basi kila kitu lala.
 
Butiku anasema mambo hayo sababu ajapewa CHEO. Na akipewa Cheo basi kila kitu lala.

At least Butiku has got guts kutoa adharani yale yanayomkera kwa manufaa ya taifa Kwani ni wangapi hawajapata vyeo na wako kimya si kwamba hawaoni kuwa mambo yanaenda halijojo. Kwa sababu ya woga wanasema bora liende.
 
Back
Top Bottom