Viongozi waoga ndiyo kikwazo kwa CHADEMA na ndiyo wameiponza!

jmushi1

Platinum Member
Nov 2, 2007
24,990
22,523
Naskia Dr. Slaa AKA muzeiya mihogo, anadai kuwa uncle jiwe hana mpinzani 2020 na hata ccm haina mpinzani. Kwahiyo kumbe Dr. Mihogo yuko full ccm sasa hivi. Nilidhani alishalipa fadhila kwa usaliti kuachana na siasa za upinzani, ili apewe ubalozi. This is sad manake imeonyesha #Mayala, ama njaa kwa kisukuma ndiyo sababu kuu ya usaliti.

On the other side, kiukweli Slaa na madhaifu yake mengi, hakuwa kiongozi muoga ama mvivu kama viongozi wengine waliobakia. Huyo Mashinji(huyu hata sauti yake sijui inafananaje), ndo kama hakuna katibu kabisa. Ila nadhani aliwekwa tu li ku counter nguvu za ccm kanda ya ziwa(my guess tho), lakini toka chadema waje na ile operation UKUTA, uncle jiwe aliwaambia wasithubutu kumjaribu, wakabakia kama mbwa koko anayeingiza mkia makalioni kwa woga.

Kiukweli naona wako very out of touch, yani wanashindwa kuwaelewa wananchi, and in return, wananchi nao wameshindwa kuwaelewa, na hivyo kupelekea huu mgogoro, sintofahamu(uncertainity), ama mtafuruku unaoendelea.

Viongozi hawa ni waoga na ndiyo maana wananchi wengi wanamkumbuka Slaa hadi sasa hivi, wananchi wanataka wasikie sauti ya kiongozi, si tu ya kuwapa matumaini, bali ya kuwaongoza na kuwaambia hatua za kuchukua. Dr. Slaa huwa alikuwa anaenda mstari wa mbele, hata kwenye maandamano mengi tu walikosakosa, mfano kule Nyamongo alikouwawa yule mwandishi kwa bomu mchana kweupe na camera zikiwa on! Ile siku kuna fununu kuwa ni Dr Slaa walitaka kumuuwa.

Sasa hivi kuna wale wanaosema na kujiuliza kama Lowassa ni asset au liability, mimi kwa maoni yangu, huu uoga umechagizwa sana na Lowassa na ndiyo maana hata mkuu wa nchi alimuita ikulu na kumsifia kuwa hajawahi kumtukana, na yeye Lowassa alirudisha sifa kemkem kwa jiwe.

Jiwe kesharudia zaidi ya mara moja kuhusu kile alichokiita "ustaarabu wa Lowassa", kwa mantiki hii, kama kuna ukweli kuwa makali ya chadema yamepunguzwa na siasa za Lowasa, basi ni wazi he is a liability. Mahesabu yamekataa, lakini hakuna maamuzi yanayochukuliwa kukabiliana na hali hiyo.

Mahesabu ya kuimegua ama kuidhoofisha ccm kwa kumchukuwa Lowassa hayakufaya kazi. Lakini chadema nayo haitaki kufanya adjustments. Maana siasa zimebadilika, lakini uoga wenu wa kutokubadilika ili kuweza kuendana na hali halisi, ndiyo umekiponza chama chenu. Mmeshaona kama vile ni business as usual, na miaka inapita tu bila ya malengo kujulikana. Ama mlitaka kusubiri hadi uncle jiwe atoke madarakani? Hiyo si ndiyo inaonyesha upinzani feki?

Maana jiwe ameamuwa kuwaangamiza na hivyo hakuna cha kusubiri. Hivyo ni bora mnekubali kufa mkipambana kuliko mkiwa mmepiga magoti.

Sisi ni binadamu ambao tunaoongozwa na saikolojia, hakuna binadamu anayependa kuwepo kwenye timu inayoshindwa tuu na yenye matatizo chungu nzima kila kukicha ambayo hayashughulikiwi.

Mnapofanyiwa unyama na kutishwa na kutotendewa haki kwa mujibu wa katiba, halafu wanachama wenu wakisikiliza kauli zenu kutaka muongozo, mko kimya, sauti inayosikika ni ya jiwe na yule Polepole, hamdai haki zenu, halafu mnategemea kitu gani?

Hakuna kitu ambacho kimekuwa fair, labda hiyo ruzuku ambayo naona ilishakuwa kama miwani ya mbao kabisa. Ndicho ambacho ccm waliamuwa kuendelea kuwapa(pengine kwa nia ya kuwapumbaza, kuwagawa, na kuwaletea migogoro). Sasahivi kaja rais ambaye ana nia ya kukifuta ama kukiuwa chama chenu na kuuwa upinzani kwa ujumla, mtakapokosa wabunge na madiwani, labda mtapata akili muanze upya, muanze kwa kuwaongoza wananchi kiukweli na siyo blah blah tu.

Maandamano yenyewe hamthubutu halafu mnawadangaya wananchi kuwa mnapigania uhuru wao.

Pengine hamuuthamini huo uhuru kama ilivyo kwa wananchi. Uoga hauwafikishi mahali, mnaharibu vijana,(wengi walikuwa wakisubiri tu kauli), ni heri muachane na hii maneno mumuunge mkono jiwe tujue moja.

LIBERTY IS ALWAYS WORTHY FIGHTING FOR!
 
Sio Kiongozi muoga,anastahili pongeza kubwa,option no.1 ilikuwa Kiongozi afike bei,tunajua masibu yake kiuchumi nk, kisha watesi kukidhi kiu ya mfalme wakaanza biashara ngumu option 2 kudhofisha chama kununua madiwani,wabunge na sasa wenyeviti.
 
Sio Kiongozi muoga,anastahili pongeza kubwa,option no.1 ilikuwa Kiongozi afike bei,tunajua masibu yake kiuchumi nk, kisha watesi kukidhi kiu ya mfalme wakaanza biashara ngumu option 2 kudhofisha chama kununua madiwani,wabunge na sasa wenyeviti.
Master Plan nzima ya jiwe ilikuwa inaonekana hata na asiye na uelewa wa kutosha kuhusu siasa zetu. Haki ngapi zimeshakanyagwa na ni unyama kiasi gani wameshafanyiwa, lakini hawajathubutu hata kuandamana. Watu wanasema watanzania waoga sijui nini. Hao viongozi walishaitisha maandamano kupinga chochote ambacho ni kinyume na katiba?

Toka ile operesheni ukuta ilipochimbwa biti na jiwe, wote walitulia kabisa kama maji ya mtungini. Wananchi mwishowe wanaona kama ni usanii tuu! Maana wao wana uchungu kuliko viongozi, na hilo baada ya muda, lina negative impact kwa wananchi. Wananchi wanahisi kama wanapotezewa muda au wanadanganywa.

Wananchi walikuwa "pumped up", lakini wakakosa uongozi wa kuwaonyesha direction, hadi yule Mange Kimambi ambaye yuko nje ya nchi akawa maarufu mara mia kushinda hao viongozi wa chadema(ilionyesha wananchi wana kiu), na wafuasi kibao wa yule dada ambao nadhani wangeitikia mwito kama kungekuwa na ground organization ya ukweli. Lakini uoga wa viongozi wa chadema ndo ulisababisha! Wakajikausha as if ni suala linaloendelea marekani alipokuwa Mange. As if siyo suala linalowahusu hata kidogo!
 
Naskia Dr. Slaa AKA muzee ya mihogo, anadai kuwa uncle jiwe hana mpinzani 2020 na hata ccm haina mpinzani. Kwahiyo kumbe Dr. Mihogo yuko full ccm sasa hivi. Nilidhani alishalipa fadhila kwa usaliti kuutema upinzani na kuhamia ccm ili apewe ubalozi. This is sad manake imeonyesha #Mayala ama njaa kwa kisukuma.

Kiukweli Slaa na madhaifu yake mengi, hakuwa muoga ama mvivu kama viongozi wengine waliobakia. Huyo Mashinji(huyu hata sauti yake sijui inafananaje), ndo kama hakuna katibu kabisa, ila nadhani aliwekwa li ku counter nguvu za ccm kanda ya ziwa(my guess), lakini toka chadema waje na ile operation ukuta, uncle jiwe anawaambia wasithubutu kumjaribu, walibakia kama mbwa koko anayeingizi mkia makalioni kwa woga.

Kiukweli naona wako very out of touch, yani wanashindwa kuwaelewa wananchi, and in return, wananchi nao wameshindwa kuwaelewa, na hivyo kupelekea huu mgogoro ama mtafuruku unaoendelea.

Viongozi hawa ni waoga na ndiyo maana wananchi wengi wanamkumbuka Slaa hadi sasa hivi, wananchi wanataka wasikie sauti ya kiongozi, si tu ya kuwapa matumaini, bali ya kuwaongoza na kuwaambia hatua za kuchukua. Dr. Slaa huwa alikuwa anaenda mstari wa mbele.

Sasa hivi kuna wale wanaosema na kujiuliza kama Lowassa ni asset au liability, mimi kwa maoni yangu, huu uoga umechagizwa sana na Lowassa na ndiyo maana hata mkuu wa nchi alimuita ikulu na kumsifia kuwa hajawahi kumtukana, na yeye Lowassa alirudisha sifa kemkem kwa jiwe.

Jiwe kesharudia zaidi ya mara moja kuhusu kile alichokiita "ustaarabu wa Lowassa", kwa mantiki hii, kama kuna ukweli kuwa makali ya chadema yamepunguzwa na siasa za Lowasa, basi ni wazi he is a liability. Mahesabu yamekataa, lakini hakuna maamuzi yanayochukuliwa kukabiliana na hali hiyo.

Mahesabu ya kuimegua ama kuidhoofisha ccm kwa kumchukuwa Lowassa hayakufaya kazi. Lakini chadema nayo haitaki kufanya adjustments. Maana siasa zimebadilika, lakini uoga wenu wa kubadilika ili kuweza kuendana na hali halisi ndo umekiponza chama chenu. Mmeshaona kama vile ni business as usual, na miaka inapita tu bila ya malengo kujulikana. Ama mlitaka kusubiri hadi uncle jiwe atoke madarakani? Hiyo si ndiyo inaonyesha upinzani feki?

Maana jiwe ameamuwa kuwaangamiza na hivyo hakuna cha kusubiri.

Sisi ni binadamu tunaoongozwa na saikolojia, hakuna binadamu anayependa kuwepo kwenye timu inayoshindwa tuu na yenye matatizo chungu nzima kila kukicha ambayo hayashughulikiwi.

Mnapofanyiwa unyama na kutishwa na kutotendewa haki kwa mujinu wa katiba, halafu wanachama wenu wakisikiliza kauli zenu, mko kimya, sauti inayosikika ni ya jiwe na yule Polepole, hamdai haki zenu, halafu mnategemea kitu gani?

Hakuna kitu ambacho kimekuwa fair, labda hiyo ruzuku ambayo naona ilishakuwa kama miwani ya mbao kabisa. Ndicho ambacho ccm waliamuwa kuendelea kuwapa(pengine kwa nia ya kuwapumbaza, kuwagawa, na kuwaletea migogoro), sasa kaja rais ambaye ana nia ya kukifuta chama chenu na kuuwa upinzani kwa ujumla, mtakapokosa wabunge na madiwani, labda mtapata akili muanze upya, muanze kwa kuwaongoza wananchi kiukweli na siyo blah blah tu.

Maandamano yenyewe hamthubutu halafu mnawadangaya wananchi kuwa mnapigania uhuru wao.

Pengine hamuuthamini huo uhuru kama ilivyo kwa wananchi. Uoga hauwafikishi mahali, mnaharibu vijana,(wengi walikuwa wakisubiri tu kauli), ni heri muachane na hii maneno mumuunge mkono jiwe tujue moja.
Rubbish!,leave alone the Dr, blame yourselfs for changing the gear on air, nothing else ,we warning you before, nd this are outcome of your madness decision s
 
kwa yaliyofanyika juzi kweli hana mpinzani. maana mawakala wote swaga nje wa upinzani. wasimamizi ndani ya vituo uvccm. huku wakipewa semina na afisa wa bwana mkubwa akiwaita mawakala wa upinzani kenge.
Nawashangaa sana! Nadhani mbinu yao wao, ni kusubiri jiwe aondoke, sasa hao ni watu wanataka kukomboa nchi kiukweli? Na sababu kubwa ya kusubiri jiwe aondoke,

Moja ni uoga, wanamuogopa jiwe toka siku achimbe ile biti kuhusiana na opersheni ukuta. Sasa ukiongeza na issue ya Lissu ndo kabisaa!

Kwanza nina Imani kuwa kama wangedili na issue ya kuhakikisha haki inatendeka na katiba inafuatwa toka mwanzoni wakati ule walipochimbwa biti kuhusu ukuta, nina imani hata Lissu asingeshambuliwa. Pengine wananchi wangeteseka na kumwaga damu, lakini kamwe isingefikia Lissu kutaka kuuwawa. Na kama ingefikia huko, tayari tungekuwa tunafahamu hatma na kama ni mbaya ni mbaya, lakini kunakuwepo na heshima kwenye ujenzi wa Taifa.
 
Rubbish!,leave alone the Dr, blame yourselfs for changing the gear on air, nothing else ,we warning you before, nd this are outcome of your madness decision s
It was a political tactic, and so therefore I can not blame them on such a move. Ama umesahau kama siyo JK na mizengwe yake, Lowassa ilikuwa apite na Jiwe angekuwa anapasikia tu ikulu!

Ama umesahahu hadi Kassim Majaliwa alikuwa akiimbia "Tuna Imani na Lowassa"? Acha kutuongopea, bifu la JK na Lowassa ndo limesababisha Jiwe kuwa ikulu na Lowassa kuwa chadema.
 
Mbowe aliuza nafasi ya kukataa kuonewa aliporoll back operation UKUTA!, Alishindwa kuprovide uongozi katika critical time!

Waoga hufa vifo vingi sana kabla ya vifo vyao halisi, lakini wabishi hufa mara moja tu!

Pamoja na hayo, ni udhalimu kupora haki ya mwananchi kumchagua kiongozi amtakaye!
Wewe unaona mbali mkuu! Pale ndipo walipo "boogey step"! It was the most critical time in the recent history of our multiparty system.

Wananchi walikosa muongozo, wananchi walikuwa pumped up!Lakini kumbe viongozi wa chadema shida yao kubwa ni a lack of empathy, yani wao hawawezi kujiweka kwenye nafasi ya wananchi na kuhisi kama wanavyohisi wao. Niliona kabisa wakipoteza watu kwenye ile issue.
 
Mbowe aliuza nafasi ya kukataa kuonewa aliporoll back operation UKUTA!, Alishindwa kuprovide uongozi katika critical time!

Waoga hufa vifo vingi sana kabla ya vifo vyao halisi, lakini wabishi hufa mara moja tu!

Pamoja na hayo, ni udhalimu kupora haki ya mwananchi kumchagua kiongozi amtakaye!
haa haa alidanganywa na viongozi wa dini. na ambao kwa sasa nao wameufyata
 
Am confused about our nation!! Economy is declining no one is able to rescue our nation, neither leading nor opposing party. Kiukweli watanzania wote tumepoteza
Mwenye akili hili analiona
Very well said bro, kumbe tuko wengi tunaohisi na kuona hayo.
 
Back
Top Bottom