Viongozi wa TikTok, X, Meta, Snap na Discord wakaangwa vilivyo kushindwa kulinda watoto mtandaoni

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993
Wakuu wa baadhi ya makampuni makubwa ya mitandao ya kijamii duniani wamehojiwa na wanasiasa katika Seneti ya Marekani na kukaangwa vilivyo kuhusu ulinzi wa watoto mtandaoni.

Wameulaumu uongozi wa Meta, TikTok, X, Snap, na Discord kwa kutochukua hatua za kutosha kulinda watoto dhidi ya madhara yanayotokea mtandaoni ikiwemo vitendo vya unyanyasaji wa kingono pamoja na matukio yaloyopelekea watoto kujitoa uhai.

Hii inaendelea sasa hivi katika Senate hearing ambapo akina Mike Zuckerberg(CEO wa Facebook) na wengine wanalaumiwa na senatores kwamba vijana hawapati protection wanapokuwa katika mitandao ya kijamii.

Kwa mfano, watu wanaweza kuoneshwa picha za ngono ambazo walikuwa hawazitafuti, na mawazo yao yalikuwa mbali na ngono: au wanaona messages ambazo zinawashawishi watu kujiua( to commit suicide).

Yule CEO wa Tik Tok anashutumiwa kuwa kibaraka wa Communist China.

Mitandao ya kijamii inaulizwa kwanini haikuripoti habari za massacre ys Tienamen Square.

Kwa hiyo Senate inajadili kupitisha muswada wa Sheria ya kuwalinda vijana katika mtandao.

Hasa Instagram inalaumiwa sana kwa kuharibu vijana.
 
Wakuu wa baadhi ya makampuni makubwa ya mitandao ya kijamii duniani wamehojiwa na wanasiasa katika Seneti ya Marekani na kukaangwa vilivyo kuhusu ulinzi wa watoto mtandaoni.

Wameulaumu uongozi wa Meta, TikTok, X, Snap, na Discord kwa kutochukua hatua za kutosha kulinda watoto dhidi ya madhara yanayotokea mtandaoni ikiwemo vitendo vya unyanyasaji wa kingono pamoja na matukio yaloyopelekea watoto kujitoa uhai.

View attachment 2890868
Dah, nimeona wenzetu wako serious sana, wale wajumbe wa seneti ni kama walipanga kumuadhibu tajiri Zuckberg.

Tutarajie mabadiliko makubwa kwenye baadhi ya apps zinazosimamiwa na hao ma CEO's walio hojiwa.
 
Back
Top Bottom