MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 10,090
- 22,340
RC Mtaka ni kiongozi mzuri lakini naona huwa anavuka kabisa mipaka labda kwa kujua au kutokujua ila mwishoni huonekana ni kama vile maamuzi binafsi ya kujijenga kisiasa. Mara kadhaa ameshawahi kuleta misuguano hadi na waziri wa elimu kutokana na maamuzi yake ambayo huwa hataki kabisa yapingwe.
Hii sio sawa kwasababu serikali haifanyi kazi kwa kufuata busara za mtu bali sheria zilizowekwa. Hata kama ni busara lazima iendane na sheria.
Leo nimeona tena RC akisema hata wanafunzi wa mkoa wake wasio na uniforms wakaripoti shuleni. Huu uamuzi unashangiliwa sana na wananchi wa huo mkoa lakini uko kinyume kabisa na utaratibu wa serikali. Kama serikali inatoa elimu bure iweje wazazi/walezi washindwe hata kununua sare za shule? Kwanini RC anataka kuondoa wajibu wa mzazi/mlezi na kuibebesha Serikali lawama?
Mimi naona ni kuwaletea tu matatizo watendaji wanaohusika na elimu kwa huu uamuzi wake wa kisiasa. RC Mtaka anachofanya ni kujijenga yeye binafsi huku akipandikiza chuki kwa wananchi dhidi ya serikali. Iko wazi kuna watendaji wanaweza kuwakataa wanafunzi watakaoripoti bila sare na matokeo yako ukawa tu mvurugano kati ya wananchi na serikali. Halafu huu uamuzi ni sawa na kurudi nyuma kabisa kimaendeleo.