Viongozi wa Dini Wakoshwa na Bwawa la Nyerere

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Wakati mradi wa kufua umeme wa Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP) ukifikia asilimia 90 ya ujenzi wake, viongozi wa dini wamesema watakwenda kuwaelezea waumini wao umuhimu wa kutunza mazingira ili mradi huo uwe endelevu.

Viongozi hao kutoka Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), jana walifanya ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa bwawa hilo, wakiongozwa na Waziri wa Nishati, January Makamba.

Mradi wa JNHPP unaogharimu takribani Sh6.5 trilioni unatarajia kuanza majaribio ya kufua umeme Februari mwakani, baada ya shughuli ya kufunga mitambo inayoendelea kukamilika.

Akizungumza kwa niaba ya CCT, Asko-fu Maimbo Mndolwa alisema wjumbe walioubeba ni kuwahamasisha waumini. kuchukua hatua za kuhifadhi na kulinda mazingira ili kuwezesha maji yanayotoka katika vyanzo mbalimbali kutitirika kwa ufanisi katika bwawa hilo.

"Sasa hivi ukipita katika vijiji kuna nuru ya umeme iliyowezesha watu kuutumia katika shughuli za ujasiriamali ili kujikwamua kiuchumi.

"Tunarudi kutoka JNHPP tukiwa na moyo na ari mpya ya kuhamasisha wananchi kutunza mazingira," alisema Mndolwa, ambaye ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania. Mwakilishi wa TEC, Askofu Lazarus Msimbe wa Jimbo Katoliki la Morogoro, alishukuru Serikali kutoa wazo la viongozi wa dini kutembelea mradi huo mikubwa wa kitaifa, akisema wametambua thamani ya viongozi katika shughuli za mendeleo ya nchi.

Alisema wanaamini mradi huo ukikamilika na kuanza uzalishaji wa nishati hiyo utakuwa mwarobaini wa kukatika umeme kunakojitokeza mara kwa mara. "Baada ya kutembelea mradi na maelezo tuliyoyapata kutoka kwa wataalamu, tunadhani tatizo la kukatika umeme litakwisha, kwa sababu wame-tueleza tutapata umeme wa kutosha na mwingine wa zaida," alisema Askofu Msimbe

Askofu Msimbe alisema watahakikisha wanaendelea kumuomba Mungu ili miradi yote ya kimkakati ikamilike, uki-wamo wa JNHPP utakaozalisha megawati 2,115 ukamilike kwa wakati.

"Kanisa Katoliki tuna nyaraka kutoka kwa Baba Mtakatifu kuhusu utunzaji wa mazingira. Tulivyotembea hapa na kupata maelezo ya wataalamu kwa kiasi kikubwa mazingira yameheshimiwa na kuna umuhimu mkubwa wa wananchi kuendelea kuyatunza.

Kwa upande wake, Waziri Makamba alisema kazi ya kufunga mitambo ya kufua umeme inaendelea, huku nyumba inayotumika kusuka mashine, mchakato wake ukiwa umefikia asilimia 70. Alisisitiza kuwa Februari mwakani wanatarajia kuanza majaribio ya kuzungusha mitambo hiyo. Kazi inaendelea kufanyika usiku na mchana, tunamshukuru Mungu tuliku-Wa na msimu mzuri wa mvua uliowezesha kupatikana kina cha maji yaliyovuka kiwango," alisema.

Mhandisi Mkazi wa mradi wa JNHPP, Lutenzano Mwandambo alisema mita za ujazo wa maji katika bwawa hilo zimefikia 163.7 kutoka usawa wa bahari.
 
Huu ni mfano halisi wa umuhimu wa kutenganisha dini na serikali. Hawa viongozi wa dini wana utaalamu gani wa kuzungumzia suala hili? Huyo anayesema kuwa wananyaraka kuhusu utunzaji wa mazingira kutoka kwa Baba Mtakatifu, aliuliza miti mingapi imekatwa katika ujenzi wa bwawa hilo? Ameulizia impact ya bwawa hilo katika Rufiji Delta? Aliomba hata ripoti ya EIA ili aisome? Na ni nani amelipia ziara hiyo?

Amandla...
 
Back
Top Bottom