Viongozi wa CHADEMA makao makuu: Msimtelekeze Joseph Ludovick Rwekeza mahabusu

Kiongozi!

Mbona una shingo ngumu kiasi hicho?

Ludovick alishatumika kisiasa na MAGAMBA kwa muda mrefu. Sio kwamba ataanza baada ya kuwekewa dhamana na CCM! Pamoja na kutumika huko ni wapi umeona CHADEMA imepwaya? Zaidi ilipata mbinu mbadala za kuhakikisha kwamba waTanganyika wanaona michezo michafu inayo fanywa na CCM.

Si umesikia kwamba huko MAGAMBANI hakukaliki kwa sababu ya hii issue ya Lwakatare?!! Kwamba CCM inazidi kujijengea uhalali wa kuchukiwa na waTanganyika kwa siasa za Kizandiki kiasi kwamba ngoma inamuelemea director wa hii movie!!

Kwa taarifa yako ni kwamba hata MAGAMBA wanajuwa wazi kwamba kwa hili wamebugi na ndio maana unamuona Mwigulu anaomba huruma ya waTanzania kupitia mitandao baada ya kusoma upepo unavyo wavumia vibaya.

Kama una huruma kwa Kudovick nenda kamtoe, vinginevyo wewe ni ndugu yake na umeshajua kwamba MAGAMBA wamesha mtosa na hivyo ataozea lupango.
 
Wasaliti siku zote hukataliwa na Pande zote.Hawezi kuaminika na Mtu yoyote.Kwa kuwa Mchuma Janga hula na wa kwao,Watu pekee wa Kumwekea Dhamana ni ndugu zake maana ndio walishindwa kutimiza majukumu yao ya Malezi Bora kwa Kijana wao.

Mkuu Farudume kwa hizo nondo ulizodondosha hapo juu unastahili like yangu kabisa,sema natumia simu muda huu,acha hilo janga ale na nduguze kwasababu aliye kinyume chetu si mwenzetu.
 
Last edited by a moderator:
Wasaliti siku zote hukataliwa na Pande zote.Hawezi kuaminika na Mtu yoyote.Kwa kuwa Mchuma Janga hula na wa kwao,Watu pekee wa Kumwekea Dhamana ni ndugu zake maana ndio walishindwa kutimiza majukumu yao ya Malezi Bora kwa Kijana wao.

Mkuu Farudume kwa hizo nondo ulizodondosha hapo juu unastahili like yangu kabisa,sema natumia simu muda huu,acha hilo janga ale na nduguze kwasababu aliye kinyume chetu si mwenzetu.
 
Last edited by a moderator:
LODU kuwa nje ni mtihani mkubwa sana Kwake kimaisha kutokana na kitendo chake cha usaliti amejiongezea maadui wengi sana.Ikiwa ni pamoja na ndani ya familia ya Lwakatare,ukoo wa Lwakatare na kwa wanachama wa CHADEMA pia ambao walichukizwa na kitendo chake cha usaliti wake.wanaweza kumfanyia kitendo chochote kisicho cha kawaida ikiwa ni pamoja na kupoteza maisha yake.Pia upande wa CCM wameshatambuwa kuwa Ludo amekosana na CHADEMA kutokana na usaliti wake hivyo wanaweza wakamdhuru wao wenyewe halafu wakawasingizia CHADEMA kuwa ndio waliyofanya hivyo.Ukizingatia kuwa CCM wameshaishiwa sera wamebaki wanawadhuru watu na kutembea kwenye majukwaa kuwasingizia CHADEMA kuwa ndio wanaodhuru watu.Rejea kutekwa kwa Ulimboka alieawataja watekaji wake kuwa ni vyombo vya dola,Morogoro kijana alipigwa risasi na polisi,Mwagosi kauawa na polisi lakini utekaji huo na mauaji hayo CCM wamegeuza kuwa sera na kuihubiri majukwaani kuwa waliyofanya hivyo ni CHADEMA.
 
mkuu, nakupongeza sana kwa kuwaambia ukweli chadema. ila kwa jinsi wanavyokushambulia inadhihirisha ni kwa namna gani hawapendi kumwona ludovick anakuwa huru. wamesahau kuwa ni huyo huyo ludovick ndiye walimtumia katika matukio mengi likiwemo la chacha wangwe, kulegeza mataili ya gari la zito, kung'oa kucha, meno na macho akina ulimboka na kibanda. ccm wanawatega tu

kama chadema waliweza kufanya hayo yote na serikali inajua na ikakaa kimya basi hakuna umuhimu wa kuwa na hiyo serikali,otherwise magaidi,wang'oa kucha na meno bila ganzi,majangili na nk ni maccm.
 
Wameishamtumia sasa hivi wamemtelekeza.

Huyu Mwigulu hafai kabisa kamtumia shushu wake karekodi video ya ugaidi kamupelekea halafu kamterekeza ushahidi wake wa mbinguni atakwenda kuutoaje sasa.
 
waHI jamaa yetu kamtoe Ludo. hizo bondi za milioni 10 wala zisikutishe. huwaga wanajisemea tu maneno kwenye makaratasi. hata kama umeamkia mandazi mawili leo bado unaweza kusaini bondi ya milioni 10. wahi kamtoe mshikaji. atakuwa na siri kubwa sana huyu chama hakijui. wahi fasta!


Hahahahaaaaaa....mkuu umenichekesha sana
 
sijamaanisha ludovicik kukutana na viongozi wa ccm mahabusu ninacho kitolea taarifa ni yeye kutumiwa kisiasa.

atumike mara ngapi kwani? Hamna jipya, wakamtoe wamtumie vyovyote wapendavyo, acha kuhofia mambo yasiyo na msingi. Ludo hawezi kuiendesha cdm wala nini, kaishajianika alivyo wala hana thamani kwa chama, waliomtumia wamtoe wamtumie tena kwa style wapendayo
 
Atakae muwekea dhamana huyo mliberali Ludo, atatutambua, kama kamfanyia hiyo ndugu yake Lawax, itakuwaje yeye?
 
Kwani Ludovic ana undugu wowote na viongozi wa Chadema makao makuu kama wa kiukanda,ushemeji au ukoo?
 
lkn hata akitumiwa kisiasa na wakti watz tushafahamu kuwa yeye alitaka kukiangamiza chama haitasaidia kitu mkuu. msaliti kumkarbisha tena nyumbani mwako?!
 
Huyu kijana anapaswa kuvuna aliyopanda. Sioni sababu ya kumtoa. Najua CCM na washirika wake watafanya kila njia kumtoa, waache wamtoa. Usitudanganye kuwa huyu kijana atakuja kuwa mwema, msaliti ni msaliti tu. Tunaweza kumtoa ila dhamira yake bado anaifanyia kazi. Mwigulu juzi akiwa Arusha katamka wazi kuwa kuna kijana ndiye aliyerekodi ile movie, sasa kwa huruma gani CHADEMA waliyo nayo mpaka wamtoe huyu Ibilisi, msaliti?
 
Kwani Ludovic ana undugu wowote na viongozi wa Chadema makao makuu kama wa kiukanda,ushemeji au ukoo?

Ni rafiki wa karibu na Lwakatare. Ni kama ndugu sasa, maana Lwakatare ni Baba wa ndoa wa Ludovick, kwa maana kuwa Lwakatare ndiye aliyesimamia ndoa ya Ludovick. Hoja yako ni kama una sifa zote za uliberali.
 
Mbona wote cdm nikisoma maelezo yenu ni kana kwamba mnakiri ule uzi wa lwakatare sio wakutengeneza bali ludo ni facilitator wa issue ya ukweli ndio maana mnamuhukumu kwa kutoa siri za chama

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Ni rafiki wa karibu na Lwakatare. Ni kama ndugu sasa, maana Lwakatare ni Baba wa ndoa wa Ludovick, kwa maana kuwa Lwakatare ndiye aliyesimamia ndoa ya Ludovick. Hoja yako ni kama una sifa zote za uliberali.
Nimekusoma blender ya kusaga na kukoboa.Halafu leo tumepishana posta unanukia kicameroun cameroun....
 
Ludovick kuisafisha CHADEMA manake ni kwamba akiri kuwa ni kweli alipokea sh. elfu 50 za Mwigulu na software zote zilizotumika katika mchezo huo kutoka kwa Muhiddin Issa Michuzi na ni kweli aliwasiliana na Mwigulu kuhusu jambo hilo kama alivyosema Shushushu wa kujitegemea Mabere Marando, kitu ambacho kama ataongea hivyo either kwenye mkutano au popote ni kwamba atakuwa amekiri kosa rasmi la kuwa ni msaliti na hakuna atakayemwamini tena ndani ya CHADEMA na hawezi kupewa wadhifa wowote na bila kusahau urafiki wao na Lwakatare utaishia hapo, anachotaka kufanya Ludo ni kuonyesha hana hatia katika hili na ndio maana ameendelea kuonyesha alama ya V kila afikapo mahakamani japo huwa hajiamini kwa sababu anajua watu wameshapoteza imani nae, kwake yeye suala ni kukana makosa yote na kushinda kesi mahakamani, ndio ushindi wake.Ushauri wako ni mzuri kwa CDM lakini ni mtihani kidogo kwa Ludo.
Baada ya kusoma kipade hiki katika gazeti la Mwananchi

Hata hivyo, mwenzake Joseph Ludovick ambaye wanashtakiwa pamoja, alikwama kupata dhamana baada ya wadhamini wake kushindwa kuwa na vielelezo vyenye vigezo kulingana na masharti ya dhamana.


Baada ya kuweka nukuu hiyo mimi kama mwana CHADEMA kindakindaki naomba kuwatahadharisha viongozi wa chadema makao makuu kuwa hakuna kosa kumbwa watakalo lifanya kama kumtelekeza LUDOVICK mahabusu.

Kuna kauli nilibahatika kuisikia kutoka kwa baadhi ya viongozi waandamizi wa CCM ya kwamba hakunakitu wanakisubiri kwa hamu kuu kamahicho na endapo kikitokea,hapo ndipo watakapo timiza lengo lao na watahakikisha wanamtoa mahabusu kwa njia yoyote ile ili awasaidia kazi zao.

Wanajamvi na wana chama wa chadema kauli hii bado naendelea kuifatilia ili kujua nini kinaendelea.

Pia napenda kuwaambia viongozi wangu kuwa endapo hili likifanikiwa hatutakuwa na mahali pa kuficha nyuso zetu, chama chetu kitachafuliwa kabisa, mimi kama mwana chama nisingependa hilo litokee kwasababu litamaliza muda wetu mwingi kama wanachama kwa kukitetea na kukisafisha chama badala ya kupigania yaliyo na maana mbele yetu kama rasimu ya katiba mpya.

hata kama amekisababishia chama matatizo ni wajibu wetu kuambatana nae na sasa tumpatie kazi ya kukishafisha chama kwa maana yeye ndiye anaefahamu mchezo mzima ulivyokuwa.

NARUDIA TENA KUWAOMBA VIONGOZI WA CHADEMA MAKAO MAKUU MSIMTLEKEZE JOSEPH LUDOVICK RWEKEZA MAHABUSU KWANI LITAKIGHARIMU CHAMA.

baada ya kusema hayo naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom