Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 912
- 4,249
Chama cha mapinduzi kilipuuza tukio la imani za kishirikina na ukatili lililofanywa na Mbunge Gekul kwa kuvikataza vyombo vya dola kuchunguza wala kuchukua hatua.
Leo tena wana CCM wamerekodiwa huko Singida wakipanga njama za mauaji kwa njia ya ajali au radi. Haya yanafanywa na viongozi wakubwa wa CCM wakiwemo wabunge.
Natumaini huu mfumo wa chama kuishi kwa kuamini sana ushirikina umepelekea chama kupata viongozi wasio na sifa. Angalia umaskini uliopo Singida linganisha na aina ya viongozi hawa akina Kingu ambao wao wanawaza kuua na kutesa wenzao tu. Hakuna baraka zinaweza kupatikana katika aina hii ya viongozi.
Kijana yupo UVCCM anawaza kuua watu sita kisa siasa na chama kimekaaa kimya na kuelekeza hizi clip zisisambazwe. Nikiwa kwenye group la CCM huku kanda ya ziwa kuna kiongozi mkubwa amediriki kuelekeza kwamba polisi wasimamie mtu atakayesambaza habari hizi akamatwe kwa maelezo kwamba chama kitafanyia kazi ndani kwa mfumo wake. Kama huku kuna makatazo yakutochukua unadhani haya makatazo yanakosa baraka kutoka juu?
Chama kimeacha misingi yake nakubali kutumia polisi, tume ya uchaguzi na viongozi wasio na sifa kukandamiza haki. Natambua hizi clip hazitapatikana kwa sababu zimeelekezwa zifungwe ila ukweli ni kwamba tunatengeneza jamii ya ushirikina. Kijana mdogo anawezaje kuwa na carrage yakuua watu sita na tukaona kawaida? Mbunge anawezaje kupanga njama za mauaji ya viongozi wasiokubaliana naye na chama kukaa kimya?
Tumekuwa wepesi sana kufumbia macho maovu kisa yapo ndani ya CCM ila sasa hivi tunakoelekea yataturarua wenyewe kwa wenyewe.....