Viongozi tumieni nafasi zenu kwa manufaa ya taifa nzima, Madaraka yanapita

F4B

JF-Expert Member
Jan 13, 2022
331
418
Kichwa cha habari kinajieleza hapo juu kwenye post hii.Ndugu zangu wanajamii forum great thinker naomba kujilipua msemo wao. Katika taifa letu kuna viongozi wanapokuwa madarakani wanajisahau katika majukumu yao wanafikili watabaki madarakani daima na mambo hayatabadilika.

Viongozi nawaasa na kuwaomba muwapo madarakani tumieni nafasi zenu vizuri kwa manufaa ya taifa kwa ujumla kwa kurekebisha sheria kandamizi, kanuni kandamizi na kuzifuta kabisa ikiwezekana ili kujenga taifa lenye upendo na ustawi bora zaidi.

Nimesema najilipua,Case study ya Mhe Moses Nape Nnauye kwanza nikiri huwa ninafurahishwa na kupendezwa na siasa zake lakini mara ya kwanza alipoingia madarakani serikalini mwaka 2015,alijisahau akafungia Bunge live na kuleta sheria ya vyombo vya habari ya mwaka 2016'kwa maoni yangu sheria hii siyo rafiki sana kwa vyombo vya habari na wana habari wenyewe hata jana umeitetea sana, Naomba nimkumbushe ndugu yangu huyu je? ipo siku uliwahi kufikiri UTASHIKIWA BASTORA mchana kweupe halfu watu waseme mtu huyo aliyekushikia BASTORA hawamjui? jibu litakuwa hapa lakini ni wapi au sehemu gani ulikosea?Nayo ni sehemu moja ni pale mlipotakiwa kufanya marekebisho sahihi ya sheria hata katiba ya nchi hamkufanya hivyo kwa sababu kila kitu mlikiona kinaenda sawa kwa upande wenu nyinyi mkiwa CCM lakini hamkufikilia kuhusu raia wengine imagine kitendo hicho imefanyiwa wewe uliyewahi kuwa katibu mwenezi CCM taifa na una Siri nyingi tu za serikali je? Mimi
mlala hoi wa msamvu?? Kifupi hamkujua ipo siku atakuja mtu kushika madaraka na akayatumia vibaya madaraka hayo na usimfanye kitu chochote.

Ndugu yangu Nape kwa sasa umeshajifunza nazani utafanya kilichosahihi zaidi kwa mstakabari wako binafisi kisiasa na taifa kwa ujumla.

Case study ya Mzee Lowasa na Sumaye hawa wazee wetu wameitumikia nchi yetu vizuri tu kwa heshima sana tu lakini kwa maoni yangu hawakuwahi kuwa na maono ya taifa hili kwa kesho yake kwani wamewahi kuhika nafasi nyeti serikalini ambazo kwa maoni yangu wangezitumia vizuri kwa ustawi wa taifa letu tusingekuwa hapa.Walikuwa na uwezo wa kuleta madiliko mbalimbali mfano katika sheria zetu za uchaguzi na uhuru wa vyama vya siasa,ni Sumaye na Lowasa waliokuwa mstari wa mbele kuhujumu wapinzani kwa kauli na matendo yao kwa mfano Sumaye alikuwa anawaambia wafanya biashara wakubwa huwezi kuwa upinzani kisha ukaendesha biashara yako kwa amani ni lazima ujiunge CCM vinginevyo ukiwa upinzani utapata misuko suko ya hapa na pale hadi ufunge biashara yako.Vilevile Lowasa naye alitumia mbinu zile zile kipindi yupo madarakani.Wazee wetu hawa 2015 walijiunga CHADEMA lakini walishindwa kuendelea na siasa za upinzani kwani sheria, kanuni na katiba yetu mbovu havikuwapa nafasi ya kuendelea kufanya siasa katika uwanja uliosawa wakiwa huko.

Kumbe kipindi wakiwa madarakani wasingekuwa wabinafisi na wenye maono ya Tanzania ya kesho wangejitahidi walao kuleta mabadiliko katika namna ya kuendesha siasa zetu kwa haki na uaswa n uhuru zaidi ikiwemo kuwa na Tume huru ya Uchaguzi hivyo Maisha yangeendelea kama kawaida.Lakini hali haikuwa hivyo waliishia kuishi kwa kujipendekeza ili wapatiwe stahiki zao ambazo ni haki yao kwa mujibu wa sheria zetu.Hapa tatizo hawakuwahi kuliona kipindi wanakula mema ya nchi.

Mifano ni mingi lakini leo niishie hapa na mimi naamini mitandao ya kijamii ina nguvu kubwa ikitumiwa vizuri na viongozi wa kitaifa na ngazi mbalimbali za uongozi na sisi wenyewe watumiaji.Nawatakia jumapili njema.
 
Back
Top Bottom