Elections 2010 Vincent Nyerere... Leticia Nyerere... Fumbo kwa CHADEMA

Napinga hoja kwa sabau siamini kama kuna kitu kama damu lulu. Kama hawa wamechaguliwa kutokana na jina lao na si uwezo wao basi nchi hii imekwisha. Ni huku kusujudia watu kwa sababu ya uzawa wao unachangia kwa kiasi kikubwa kutufikisha hapa ambapo wakina na January nao wanaona wana damu ya lulu! Mama Maria alikuwa mke wa Mwalimu na si zaidi ya hapo. Kumgeuza leo oracle ni kutotutendea haki watanzania. Tuwape heshima wanayostahili kama binadamu lakini tusivuke mpaka na kuanza kuwasujudia. Mbaya zaidi hao unaowadai wana damu ya Mwalimu mbona waliojiita wasemaji wa ukoo waliwatolea nje? Walisema (I stand to be corrected) kuwa Vincent si ndugu wa karibu ( ingawa ni mtoto wa mdogo wake Mwalimu) na Leticia ni mtaliki wa mtoto wa Nyerere kwa hiyo si damu yao ( Makongoro amfungia safari Leticia Nyerere! ) Sasa hayo ya baraka yalikuwa wapi? Tumshukuru Mungu kwa Mwalimu lakini si kwa familia yake. Hapa si Korea ya Kaskazini.

Amandla......

Naheshimu mtazamo wako pia, kwani ni mitazamo tofauti. Lakini Nyerere mwenyewe alisema katika uhai wake kwamba katika vyama vyote vya upinzani alichokiona kuwa na umakini ni Chadema. Hivyo mimi ninaungana na mtazamo wa aliyeanzisha thread hii! Pia Dr. Slaa amekuwa akimuenzi Nyerere kwenye kampeni zake!
 
haya ndio mawazo yaliyokomaa. hongera sana
 
Chadema. Kama kuna fumbo Mungu ameweka juu yenu ni juu ya familia ya Nyerere. Haya ni maoni yangu binafsi. Yanaweza kupuuzwa ama kuungwa mkono. Sitajali. Ila nitasimama katika maono yangu.

Ndoto ya Baba wa Taifa ilikuwa ni kuona Tanzania inaendelea kuwa nchi ya amani na utulivu(dhana ambazo zinahubiriwa kinafiki na CCM ya leo). Nyerere hatunaye. Ametangulia kwenye haki.

Watoto wake warithi nini?

Nyerere hakuwa mwizi. Kwa hiyo watoto wake hawawezi kuwa wezi.

Nyerere hakuwa mtu wa viduku. Kwa hiyo watoto wake hawawezi kuwa watu wa kuandikwa kwenye magazeti ya udaku na kupigwa picha za kuweka kwenye blog za michuzi anayepigwa picha akibeba kinyago cha uume.

Nyerere alikuwa mtu wa watu. Watoto wake wanajaribu kukimbilia kwenye kundi (japo dogo) la watu wanaohubiri mageuzi na usawa katika jamii. Alianza Makongoro na NCCR. Mrema akamuangusha. Mrema akawa mnafiki asiye na msimamo anayefarakana na kila chama anachokuwa yupo. Lyatonga kafulia. Huyo tumuache.

Chadema.

Mungu amegeuza macho kwenu. Amewapa Vincent.

Jiulizeni.

Mwaka 2005, Chadema haikuwa na diwani jimbo la Musoma mjini. Leo ina madiwani 8 (usisahau uchakachuaji wa CCM). Damu ya Nyerere. Halmashauri ya Mji wa Musoma iko chini ya Chadema. Chini ya Nyerere.

Chadema musione kitu hiki kuwa kidogo. Na wala musione kuwa cha kawaida. Ni baraka za Mungu Chadema kuhusishwa na familia ya Nyerere, na popote pale walipo, CCM inawauma sana.

Mtembeleeni Maria (Mrs. Nyerere). Hebu muulizeni mzee alikuwa akisema nini kuhusu Tanzania ya leo walipokuwa wamelala kitandani. Atawaambia mengi yatakayosaidia kuturudisha Watanzania kwenye njia sahihi.

Nina amini kama Maria angeona tatizo, asingekubali Vincent na Leticia kugombea uongozi kupitia Chadema.

Kuna kitu Maria anacho. Mfuateni.

Namaliza kwa kusema: Ahsante Mungu kwa familia ya muasisi wa Taifa hili.

Chadema mumepewa Fumbo.

Epukeni ushetani uliokisambaratisha NCCR cha Mrema na kumuacha Makongoro akionekana mtu wa kawaida katika jamii, wakati damu yake ni lulu....damu ya Julius Kambarage Nyerere.

well articulated
 
Kinyang'anyiro cha Ubunge na Udiwani wa Musoma Mjini una mengi ya kueleza kuliko wengi mnavyodhani. Tutayasema katika muda muafaka. Tusherehekee kwanza.
 
Naheshimu mtazamo wako pia, kwani ni mitazamo tofauti. Lakini Nyerere mwenyewe alisema katika uhai wake kwamba katika vyama vyote vya upinzani alichokiona kuwa na umakini ni Chadema. Hivyo mimi ninaungana na mtazamo wa aliyeanzisha thread hii! Pia Dr. Slaa amekuwa akimuenzi Nyerere kwenye kampeni zake!

Kuna tofauti kati ya kumuenzi Nyerere na kuenzi ukoo wake. Watoto na ndugu wa Nyerere tunawajua na ni watu wa kawaida tu. Kutaka leo tugeuze Butiama kuwa sehemu ya pilgrimage kwenda kuomba baraka za mjane wa Nyerere ni kutudhihaki watanzania wengine. Dr. Slaa amemsifia na kumuenzi Julius Kambarage Nyerere na sio Maria au mmoja wa watoto wake. Atawaheshimu lakini kuwaenzi, hapana. Mtu unaenziwa kwa kitu ulichofanya na si kwa sababu tu ulizaliwa na fulani. Vincent na Leticia wanastahili sifa kama wana harakati kwa nafsi yao na si ati kwa sabau wana uhusiano na ukoo wa mwalimu. Ulimbukeni huu ndio unaotufanya tuwape vyeo vya ajabu watoto wa chekechea kwa sababu tu wanatoka katika ukoo fulani. Ukwelli ni kwamba kama Chadema wanataka kukubalika kwa sababu ati Nyerere aliwasifia basi hawana hoja. Chadema wanakubalika na watu kutokana na msimamo wao na si kwa sababu ya hizo baraka. Mnaotaka kuwageuza watoto wa kambo wa nyerere hamuwatendei haki wale wote waliotoka jasho kuifikisha Chadema hapa ilipo.

Amandla.........
 
Sauti ya hofu.

Si munawadharau!! Hatujasahau. Tarehe 14 October 2010 hakuna kiongozi wa Serikali alikwenda huko. Gazeti la Mwananchi likawaumbua. Mukaja na vitisho vya kutaka kulifungia.

Mungu si mwanadamu bwana.

Jaribuni kuwachakachua kama munaweza.

Andika kinachoeleweka. Wakina nani hao wanaodharauliwa? Kukataa kuwaenzi si kuwadharau. Wao si Miungu bali ni binadamu kama sisi.

Kiongozi wa serikali aende wapi na aende kufanya nini?

Na hilo la kuchakachua linatoka wapi? Mimi sipingi kuwa wameshinda kihalali ( sijui kama matokeo ya Leticia yamettoka). Ninachopinga ni huku kujipendekeza ati wameshinda kwa sababu wana damu ya lulu! naona ni upuuzi mtupu na kuwadhalilisha hao unaojifanya kuwatetea.

Amandla......
 
From mwananchi.(kwa manufaa ya wanaJF - si msimamo wangu mie)
Makongoro amfungia safari Leticia Nyerere
Friday, 17 September 2010 08:17
0diggsdigg
Frederick Katulanda, Mwanza

MWENYEKTI wa CCM mkoani Mara, Makongoro Nyerere, amemtupia madongo mgombea ubunge wa Jimbo la Kwimba, kupitia tiketi ya Chadema, Leticia Nyerere, kuwa anatumia jina la Nyerere ili kujipatia umaarufu wa kisiasa.
Makongoro pia amemtaka Leticia kuacha mara moja, kutumia jina la ukoo wa Nyerere katika harakati zake za kisiasa kwa kuzingatia kuwa ndoa kati yake na Madaraka Gedfrey Nyerere haipo tena.

Mwenyekiti huyo wa CCM na Madaraka ni watoto wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Leticia anagombea ubunge wa Jimbo la Kwimba, akichuana na Shanif Hirani Mansoor, anayewania kwa tiketi ya CCM.

Hatua ya Makongoro kumtaka Leticia aache kutumia jina la ukoo wa Nyerere katika shughuli za kisiasa, aliifanya juzi alipokuwa akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za CCM, katika Jimbo la Kwimba.

Kampeni hizo zilizinduliwa katika mji mdogo wa Hungumalwa, wilayani Kwimba.

Katika uzinduzi huo, Makongoro alielezea kushangazwa kwake juu ya hatua ya viongozi wa Chadema na Leticia, kutumia jina la ukoo wa Nyerere katika kujinadi kwa wapiga kura.

Alisema hata hivyo kitendo hicho kinacholenga katika kumwezesha mgombea huyo wa Chadema kuchaguliwa, hakitasaidia hata kidogo kushinda katika uchaguzi huo.

Alisisitiza kuwa ni makosa kwa mgombea huyo kutumia jina la ukoo wa Nyerere kujinadi, hasa ikizingatiwa kuwa ndoa baina yake na mdogo wake (Madaraka) haipo tena.

Kwa mujibu wa Makongoro, wanandoa hao walitengana miaka 12 iliyopita baada ya kutofautiana.

"Huyu anayejiita Leticia Nyerere hasemeshani na Madaraka, achilia mbali hata kusalimiana, sasa anatumiaji jina la ukoo wetu. Angalau mimi naweza kuzungumza naye, ni kweli alikuwa mke wa mdogo wangu na alibahatika kuzaa naye watoto watatu lakini mambo ya ndoa wengi mnayajua, sasa siyo mke wake tena," alifafanua.

Alisema ingawa hataki kuingia kwa undani kuzungumzia mgogoro kuhusu ndoa hiyo, alisema yeye na mkewe Jaji Aisha Nyerere, ndio walikuwa wasimamizi.

Alisema katika ndoa hiyo, hayati Mwalimu Nyerere, alitoa ng'ombe 30.

"Huo ni uongo, ninawaomba wananchi wa Jimbo la Kwimba muuachana naye na kumchagua mgombea wa CCM Shanif Mansoor," alieleza makongoro Nyerere.

Makongoro alidai kuwa wakati wa harusi, yeye alikuwa ofisa wa jeshi na mke wake alikuwa hakimu.

Pia alisema mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chadema, Dk. Wilbroad Slaa, amekuwa akimtumia Leticia kama mtaji wa kisiasa katika kuomba kura.

Katika hotuba yake, Makongoro pia alisema Dk Slaa naye anapoteza muda mwingi kuzungumzia ufisadi, wakati jambo hilo limeshashughulikiwa na Serikali ya Awamu ya Nne.
 
Kuna tofauti kati ya kumuenzi Nyerere na kuenzi ukoo wake. Watoto na ndugu wa Nyerere tunawajua na ni watu wa kawaida tu. Kutaka leo tugeuze Butiama kuwa sehemu ya pilgrimage kwenda kuomba baraka za mjane wa Nyerere ni kutudhihaki watanzania wengine. Dr. Slaa amemsifia na kumuenzi Julius Kambarage Nyerere na sio Maria au mmoja wa watoto wake. Atawaheshimu lakini kuwaenzi, hapana. Mtu unaenziwa kwa kitu ulichofanya na si kwa sababu tu ulizaliwa na fulani. Vincent na Leticia wanastahili sifa kama wana harakati kwa nafsi yao na si ati kwa sabau wana uhusiano na ukoo wa mwalimu. Ulimbukeni huu ndio unaotufanya tuwape vyeo vya ajabu watoto wa chekechea kwa sababu tu wanatoka katika ukoo fulani. Ukwelli ni kwamba kama Chadema wanataka kukubalika kwa sababu ati Nyerere aliwasifia basi hawana hoja. Chadema wanakubalika na watu kutokana na msimamo wao na si kwa sababu ya hizo baraka. Mnaotaka kuwageuza watoto wa kambo wa nyerere hamuwatendei haki wale wote waliotoka jasho kuifikisha Chadema hapa ilipo.

Amandla.........

Kweli CCM na watu wake kimepoteza dira.
 
Nyerere was an exceptional person, like it or not!!!! He is nothing like any of these greedy guys who force their ways to be leaders of people who actually never chose them
 
From mwananchi.(kwa manufaa ya wanaJF - si msimamo wangu mie)
Makongoro amfungia safari Leticia Nyerere
Friday, 17 September 2010 08:17
0diggsdigg
Frederick Katulanda, Mwanza

MWENYEKTI wa CCM mkoani Mara, Makongoro Nyerere, amemtupia madongo mgombea ubunge wa Jimbo la Kwimba, kupitia tiketi ya Chadema, Leticia Nyerere, kuwa anatumia jina la Nyerere ili kujipatia umaarufu wa kisiasa.
Makongoro pia amemtaka Leticia kuacha mara moja, kutumia jina la ukoo wa Nyerere katika harakati zake za kisiasa kwa kuzingatia kuwa ndoa kati yake na Madaraka Gedfrey Nyerere haipo tena.

Mwenyekiti huyo wa CCM na Madaraka ni watoto wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Leticia anagombea ubunge wa Jimbo la Kwimba, akichuana na Shanif Hirani Mansoor, anayewania kwa tiketi ya CCM.

Hatua ya Makongoro kumtaka Leticia aache kutumia jina la ukoo wa Nyerere katika shughuli za kisiasa, aliifanya juzi alipokuwa akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za CCM, katika Jimbo la Kwimba.

Kampeni hizo zilizinduliwa katika mji mdogo wa Hungumalwa, wilayani Kwimba.

Katika uzinduzi huo, Makongoro alielezea kushangazwa kwake juu ya hatua ya viongozi wa Chadema na Leticia, kutumia jina la ukoo wa Nyerere katika kujinadi kwa wapiga kura.

Alisema hata hivyo kitendo hicho kinacholenga katika kumwezesha mgombea huyo wa Chadema kuchaguliwa, hakitasaidia hata kidogo kushinda katika uchaguzi huo.

Alisisitiza kuwa ni makosa kwa mgombea huyo kutumia jina la ukoo wa Nyerere kujinadi, hasa ikizingatiwa kuwa ndoa baina yake na mdogo wake (Madaraka) haipo tena.

Kwa mujibu wa Makongoro, wanandoa hao walitengana miaka 12 iliyopita baada ya kutofautiana.

"Huyu anayejiita Leticia Nyerere hasemeshani na Madaraka, achilia mbali hata kusalimiana, sasa anatumiaji jina la ukoo wetu. Angalau mimi naweza kuzungumza naye, ni kweli alikuwa mke wa mdogo wangu na alibahatika kuzaa naye watoto watatu lakini mambo ya ndoa wengi mnayajua, sasa siyo mke wake tena," alifafanua.

Alisema ingawa hataki kuingia kwa undani kuzungumzia mgogoro kuhusu ndoa hiyo, alisema yeye na mkewe Jaji Aisha Nyerere, ndio walikuwa wasimamizi.

Alisema katika ndoa hiyo, hayati Mwalimu Nyerere, alitoa ng'ombe 30.

"Huo ni uongo, ninawaomba wananchi wa Jimbo la Kwimba muuachana naye na kumchagua mgombea wa CCM Shanif Mansoor," alieleza makongoro Nyerere.

Makongoro alidai kuwa wakati wa harusi, yeye alikuwa ofisa wa jeshi na mke wake alikuwa hakimu.

Pia alisema mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chadema, Dk. Wilbroad Slaa, amekuwa akimtumia Leticia kama mtaji wa kisiasa katika kuomba kura.

Katika hotuba yake, Makongoro pia alisema Dk Slaa naye anapoteza muda mwingi kuzungumzia ufisadi, wakati jambo hilo limeshashughulikiwa na Serikali ya Awamu ya Nne.

Makongolo huyo huyo alikuwa akimpigia kampeni Vincent Musoma Mjini.

Tulieni tuwasulubu.

Ndiyo kwanza tunaanza. Na haturudi nyuma.
 
Re: Vincent Nyerere... Leticia Nyerere... Fumbo kwa CHADEMA

Napinga hoja kwa sabau siamini kama kuna kitu kama damu lulu. Kama hawa wamechaguliwa kutokana na jina lao na si uwezo wao basi nchi hii imekwisha. Ni huku kusujudia watu kwa sababu ya uzawa wao unachangia kwa kiasi kikubwa kutufikisha hapa ambapo wakina na January nao wanaona wana damu ya lulu! Mama Maria alikuwa mke wa Mwalimu na si zaidi ya hapo. Kumgeuza leo oracle ni kutotutendea haki watanzania. Tuwape heshima wanayostahili kama binadamu lakini tusivuke mpaka na kuanza kuwasujudia. Mbaya zaidi hao unaowadai wana damu ya Mwalimu mbona waliojiita wasemaji wa ukoo waliwatolea nje? Walisema (I stand to be corrected) kuwa Vincent si ndugu wa karibu ( ingawa ni mtoto wa mdogo wake Mwalimu) na Leticia ni mtaliki wa mtoto wa Nyerere kwa hiyo si damu yao ( Makongoro amfungia safari Leticia Nyerere! ) Sasa hayo ya baraka yalikuwa wapi? Tumshukuru Mungu kwa Mwalimu lakini si kwa familia yake. Hapa si Korea ya Kaskazini.

Amandla......

Fundi Utumbo

Ulimwengu unakwenda kwa DNA sio Korea wala mawazo finyu ya Fundi Mchundo (technician)

Watoto wa Leticia wanakuwa kizazi cha nani?
 
Korea kaskazini!? Korea Kaskazini iko CCM ambako Baba na Mwana wanapokaa na kupanga kuiba kura za waTanzania
 
Back
Top Bottom