Inapotokea umekwenda msibani ukamkuta rafiki yako mnayefahamiana vizuri hadi kwenye familia zenu analia na kusaga meno kuliko hata mke/mume na ndugu wa marehemu wakati unajua kuwa hawakuwa na uhusiano wowote wa karibu utalichukuliaje suala hilo? Jamaa umeshawahi kwenda naye kwenye misiba mingi pamoja na ya ndugu zake wa karibu lakini hajawahi kuangua kilio kiasi hicho. Hata siku mama yake mzazi alipofariki mlikuwa wote lakini hakulia hivyo. Nimeshindwa kumuuliza kilichomsibu.