Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,335
- 113,990
Hakuna njia zaidi ya kustaarabika tu....
Tatizo hili ni hulka ya binadamu. Huko West tunakodhani wamestaarabika wako kama sisi hivi hivi tu, unakumbuka yale ya Bush Vs Gore? Kinachowabana wenzetu ni utaratibu mzuri wa kisheria walio nao. Kwa upande wa Bush ilishindikana kwa vile majaji watano walikuwa wamewekwa pale ama na Baba yake au na Reagan.Hakuna njia zaidi ya kustaarabika tu....
kifungu cha uchaguzi wa raisi kiingie katika katiba ya nchi
na isomeke hivi:
ni uhaini kushiriki kumpa/kumuondolea mgombea wa kiti cha uraisi kura isiyo/iliyo halali yake---then baada ya hapo sheria itatafsiri hilo kosa libebe adhabu gani.
matokeo ya raisi yahojiwe mahakamani.
Hakuna demokrasia kwa watu kipato chao ni chini ya dola moja kwa siku, 90% hawana taaluma yeyote, 98% hawako kwenye formal sector.
niliwahi sikia mtu mmoja alienda kwenye kituo cha kura akitafuta vibarua wa kulima shamba kwa posho ya 10,000/= watu wote waliacha kupiga kura na kwenda kupalilia mihogo! mwingine alienda kwenye mkutano wa mwenzie na 20lts za gongo na kiroba cha chumvi ule mkutano ulivunjika akina mama waliwahi mgao wa chumvi na wazee wakabaki wakiburudika kinywaji!
Muulize mheshimiwa shubiri ya Geita kisa aliyejenga choo stend kakosa ubunge!
Intelahamwe, Kony, Nkunda na Raila kuingia ikulu kwa kuchoma walokole sio sawa. EAG eldoret na kibaki hakuna relation yeyote. wanaoleta vurugu kenya sidhani kama kura walipiga kwani ni watoto na vijana.
Sasa tufanyeje?
Tuondoe ujinga kwanza kwa kuhakikisha watoto wetu wanaenda shule, watz tuache biashara za hiace na lodge bubu tujenge shule na vyuo, mch.getrude katuonyesha mfano hata mungu kambariki ubunge umemfuata nyumbani.
Hawa viongozi waliopigania kile wanachoita uhuru ni problem katika demokrasia maana wao wanaamini ni wao wanaoweza kutawala. Sasa hii itaendelea kuwa problem hadi watakoishia wote. Tatizo linakuja pale ambapo inaonekana wanawarithisha watoto wao vyeo pamoja na tabia zao zote mbovu za kifisadi. Hili ndio litasababisha sisi waafrika tuendelee kukunjiani ngumu na kukimbilia misituni.
Kama walivyosema wengine, hizo strategies alizotoa Kichuguu ni nzuri sana kama hawa jamaa wangekuwa wanaiba tu kura, haya majamaa yakiona yamekwama kuiba yananyang'anya kabisa kwa nguvu kwa kutumia majeshi kama walivyofanya kule Zanzibar 1995, 2000 na 2005 na kama walivyomnyang'anya ubunge Lwakatare pale Bukoba 2005. Kwa hiyo tunaongelea watu ambao hawana ustaarabu wa kawaida unaotarajiwa kwa binadamu wa karne hii. Labda Kikwete anaweza akabadilika, lakini sidhani kwa sababu hata yeye alikuwa anachekelea ushindi wa 80% wakati akijua kabisa kuna makura mengine alibambikizwa!
Tatizo hili ni hulka ya binadamu. Huko West tunakodhani wamestaarabika wako kama sisi hivi hivi tu, unakumbuka yale ya Bush Vs Gore? Kinachowabana wenzetu ni utaratibu mzuri wa kisheria walio nao. Kwa upande wa Bush ilishindikana kwa vile majaji watano walikuwa wamewekwa pale ama na Baba yake au na Reagan.
Njia Ya Kuondoa Wizi Wa Kura Ni Moja Tu, Muda Wa Uchaguzi Ukifika Raisi Anayemaliza Muda Ake Pembeni Nchi Iongozwe Na Jaji Mkuu Kama Rais Wa Muda Hadi Hapo Uchaguzi Utapokwisha Na Rais Aliyechaguliwa Kwa Kura Kutangazwa Na Malalamiko Yote (kama Yapo) Yawe Yameshatolewa Na Kupatiwa Ufumbuzi.
Hapana bwana hawako kama sisi. Hivi hiyo 2000 uliona watu wangapi wakipigana mapanga? Wangapi walikufa kutokana na hiyo saga? Aliyeshindwa alikubali, yakaisha, taifa likasonga mbele. Sasa niambie Kenya mshindi wa kweli ni nani na mshindwa ni nani, na kama huyo mshindwa amekubali kushindwa? Wangapi wameshakufa Kenya kutokana na huu uchaguzi wa juzi? Huo utaratibu mzuri unaousema ndio ustaarabu wenyewe kwani si wakati wote mtu utakuwa-favored na sheria lakini kwa vile ni sheria, basi inabidi iheshimiwe. Kwa nini sisi tunashindwa kuwa na utaratibu kama huo? Hivi mtu kama Kibaki kweli ungemtegemea kufanya haya anayotuhumiwa kufanya ukizingatia nafasi aliyokuwa nayo kabla hajawa raisi? Kama sisi sivyo tulivo kwa nini haya mambo yanatokea si ktk nchi moja tu bali nchi kibao Afrika. Angalia Zambia, angalia Zimbabwe walivyo sasa. Juzi nilikuwa naangalia Africa Channel wakimhoji Mugabe. Yaani sasa hivi Wazimbabwe wanatia huruma. Badala ya kuendelea wanazidi kutoendelea. Serikali yao imechapisha noti ya dola 200,000. Umeona wapi hiyo? Aisee nikitaka ninaweza kujaza jamboforum nzima nikizungumzia laana tuliyonanyo.
Hili swala la ugonvi ni kitu kingine, mimi nilikuwa naongelea kuhusu wizi wa kura. Nakubalina nawe kabisa kuwa swala la ugomvi litatatuliwa kwa watu kuwa wastaarabu.
Kama swala ni wizi wa kura basi sidhani kama Bush aliiba kura. Kilichokuwa kinabishaniwa ni uhesabuji wa kura ambazo kwa namna moja ama nyingine zilikuwa zimeharibika. Unakumbuka mambo ya hanging chad..? Kwa mahesabu ya mwanzo Bush alikuwa anaongoza...so sijui ua uwizi wa kua yametokea wapi tena.
Sina uhakika na hayo unayoyasema. Hivi unajua kuwa Al Gore hakuhitaji kushinda Florida ili awe raisi? Kama angeshinda state nyingine yoyote ile zaidi ya Florida leo hii pengine angekuwa raisi. Sasa maajenti wa Bush walijuaje kama ilikuwa lazima kwa Gore kushinda Florida na si kwa Tennessee au Arkansas kule kwa bosi wake? Kwanini hao maajenti hawakwenda kufanya manjonjo huko kwingine? Gore kama angeshinda TN ama AR ilikuwa imetoka hiyo hata kama Bush angeshinda Florida....
(1) Australia wana sheria inayowabana watu kupiga kura; nadhani kutokupiga kura ni kosa dogo la jinai. Ni muhimu na sis tuwe na sheria za namna hiyo ili kuhakikisha kuwa kila raia anapiga kura yake yeye mwenyewe hata kama anampigia mtu kwa kununuliwa, mradi tu atumie haki yake ya kidemokrasia. Tukishakamilisha hilo, itaacha nafasi chache sana za ku-stuff kura haramu kwenye ballot box.
(2) Wizi mwingine wa kura hutokea kweye kuhesabu na kujumlisha idadi kura. Ndiyo maana nadhani taifa linatakiwa liweke investament ya kutosha kwenye tume ya Uchaguzi. Kama serikali iliamua kuwalipa mamilion ya fedha maafisa wa TRA kusudi wasiibe, nadhani wakati umefika kuwalipa mamilioni ya fedha maafisa wa uchaguzi kusudi wasimamie ujenzi wa demokrasia sawasawa.
Kitila,
Viongozi waliopigania Uhuru kwa sasa hivi ni wachache sana waliobaki. Tatizo ni kuwa wale waliowarithi wanaijeweka kama wao pia walipigania uhuru.
Maneno msumari kichuguu. Hapo Zanzibar wala sio mbali sana, ukiongelea demokrasia tu, utaambiwa tumepindua na wao wapindue kama wanaweza! Ukiangalia anaeongelea maneno hayo amezaliwa baada ya 1964 au hiyo 1964 alikuwa hajui lolote (mtoto).
Najiuliza kampindua nani?
Iwapo anatokea kiongozi wa chama cha siasa chenye wafuasi wengi na kujinadi kuwa hayatambui mapinduzi ya 1964, ambayo ndio hayohayo yaliyobariki mfumo wa vyama vingi unategemea apewe jibu gani?