Vikwazo vya Kikatiba katika kuleta Maendeleo na Demokrasia

Hakuna njia zaidi ya kustaarabika tu....
Tatizo hili ni hulka ya binadamu. Huko West tunakodhani wamestaarabika wako kama sisi hivi hivi tu, unakumbuka yale ya Bush Vs Gore? Kinachowabana wenzetu ni utaratibu mzuri wa kisheria walio nao. Kwa upande wa Bush ilishindikana kwa vile majaji watano walikuwa wamewekwa pale ama na Baba yake au na Reagan.
 
kifungu cha uchaguzi wa raisi kiingie katika katiba ya nchi

na isomeke hivi:
ni uhaini kushiriki kumpa/kumuondolea mgombea wa kiti cha uraisi kura isiyo/iliyo halali yake---then baada ya hapo sheria itatafsiri hilo kosa libebe adhabu gani.

matokeo ya raisi yahojiwe mahakamani.

Kweli kabisa, Kuharamisha kura za wizi ni njia moja. Je nani atakuwa responsible kwa kura za wizi? Candidate huwa haibi ila maajenti wake. Mnaonaje kama tukiwa na lead time ya muda wa kama miezi miwili tangu uchaguzi hadi inauguration ili migogoro yote itokanayo na uchaguzi itatuliwe kwanza? Baada ya hapo Rais aneyiongia madarakani anajua kuwa anayo mandate ya kuongoza nchi nzima siyo clique ya watu wachache tu.
 
Hakuna demokrasia kwa watu kipato chao ni chini ya dola moja kwa siku, 90% hawana taaluma yeyote, 98% hawako kwenye formal sector.

niliwahi sikia mtu mmoja alienda kwenye kituo cha kura akitafuta vibarua wa kulima shamba kwa posho ya 10,000/= watu wote waliacha kupiga kura na kwenda kupalilia mihogo! mwingine alienda kwenye mkutano wa mwenzie na 20lts za gongo na kiroba cha chumvi ule mkutano ulivunjika akina mama waliwahi mgao wa chumvi na wazee wakabaki wakiburudika kinywaji!

Muulize mheshimiwa shubiri ya Geita kisa aliyejenga choo stend kakosa ubunge!

Intelahamwe, Kony, Nkunda na Raila kuingia ikulu kwa kuchoma walokole sio sawa. EAG eldoret na kibaki hakuna relation yeyote. wanaoleta vurugu kenya sidhani kama kura walipiga kwani ni watoto na vijana.

Sasa tufanyeje?
Tuondoe ujinga kwanza kwa kuhakikisha watoto wetu wanaenda shule, watz tuache biashara za hiace na lodge bubu tujenge shule na vyuo, mch.getrude katuonyesha mfano hata mungu kambariki ubunge umemfuata nyumbani.

(1) Australia wana sheria inayowabana watu kupiga kura; nadhani kutokupiga kura ni kosa dogo la jinai. Ni muhimu na sis tuwe na sheria za namna hiyo ili kuhakikisha kuwa kila raia anapiga kura yake yeye mwenyewe hata kama anampigia mtu kwa kununuliwa, mradi tu atumie haki yake ya kidemokrasia. Tukishakamilisha hilo, itaacha nafasi chache sana za ku-stuff kura haramu kwenye ballot box.

(2) Wizi mwingine wa kura hutokea kweye kuhesabu na kujumlisha idadi kura. Ndiyo maana nadhani taifa linatakiwa liweke investament ya kutosha kwenye tume ya Uchaguzi. Kama serikali iliamua kuwalipa mamilion ya fedha maafisa wa TRA kusudi wasiibe, nadhani wakati umefika kuwalipa mamilioni ya fedha maafisa wa uchaguzi kusudi wasimamie ujenzi wa demokrasia sawasawa.
 
Hawa viongozi waliopigania kile wanachoita uhuru ni problem katika demokrasia maana wao wanaamini ni wao wanaoweza kutawala. Sasa hii itaendelea kuwa problem hadi watakoishia wote. Tatizo linakuja pale ambapo inaonekana wanawarithisha watoto wao vyeo pamoja na tabia zao zote mbovu za kifisadi. Hili ndio litasababisha sisi waafrika tuendelee kukunjiani ngumu na kukimbilia misituni.

Kama walivyosema wengine, hizo strategies alizotoa Kichuguu ni nzuri sana kama hawa jamaa wangekuwa wanaiba tu kura, haya majamaa yakiona yamekwama kuiba yananyang'anya kabisa kwa nguvu kwa kutumia majeshi kama walivyofanya kule Zanzibar 1995, 2000 na 2005 na kama walivyomnyang'anya ubunge Lwakatare pale Bukoba 2005. Kwa hiyo tunaongelea watu ambao hawana ustaarabu wa kawaida unaotarajiwa kwa binadamu wa karne hii. Labda Kikwete anaweza akabadilika, lakini sidhani kwa sababu hata yeye alikuwa anachekelea ushindi wa 80% wakati akijua kabisa kuna makura mengine alibambikizwa!

Kitila,

Viongozi waliopigania Uhuru kwa sasa hivi ni wachache sana waliobaki. Tatizo ni kuwa wale waliowarithi wanaijeweka kama wao pia walipigania uhuru.
 
Tatizo hili ni hulka ya binadamu. Huko West tunakodhani wamestaarabika wako kama sisi hivi hivi tu, unakumbuka yale ya Bush Vs Gore? Kinachowabana wenzetu ni utaratibu mzuri wa kisheria walio nao. Kwa upande wa Bush ilishindikana kwa vile majaji watano walikuwa wamewekwa pale ama na Baba yake au na Reagan.

Hapana bwana hawako kama sisi. Hivi hiyo 2000 uliona watu wangapi wakipigana mapanga? Wangapi walikufa kutokana na hiyo saga? Aliyeshindwa alikubali, yakaisha, taifa likasonga mbele. Sasa niambie Kenya mshindi wa kweli ni nani na mshindwa ni nani, na kama huyo mshindwa amekubali kushindwa? Wangapi wameshakufa Kenya kutokana na huu uchaguzi wa juzi? Huo utaratibu mzuri unaousema ndio ustaarabu wenyewe kwani si wakati wote mtu utakuwa-favored na sheria lakini kwa vile ni sheria, basi inabidi iheshimiwe. Kwa nini sisi tunashindwa kuwa na utaratibu kama huo? Hivi mtu kama Kibaki kweli ungemtegemea kufanya haya anayotuhumiwa kufanya ukizingatia nafasi aliyokuwa nayo kabla hajawa raisi? Kama sisi sivyo tulivo kwa nini haya mambo yanatokea si ktk nchi moja tu bali nchi kibao Afrika. Angalia Zambia, angalia Zimbabwe walivyo sasa. Juzi nilikuwa naangalia Africa Channel wakimhoji Mugabe. Yaani sasa hivi Wazimbabwe wanatia huruma. Badala ya kuendelea wanazidi kutoendelea. Serikali yao imechapisha noti ya dola 200,000. Umeona wapi hiyo? Aisee nikitaka ninaweza kujaza jamboforum nzima nikizungumzia laana tuliyonanyo.
 
Njia Ya Kuondoa Wizi Wa Kura Ni Moja Tu, Muda Wa Uchaguzi Ukifika Raisi Anayemaliza Muda Ake Pembeni Nchi Iongozwe Na Jaji Mkuu Kama Rais Wa Muda Hadi Hapo Uchaguzi Utapokwisha Na Rais Aliyechaguliwa Kwa Kura Kutangazwa Na Malalamiko Yote (kama Yapo) Yawe Yameshatolewa Na Kupatiwa Ufumbuzi.

Hii nayo ni njia nzuri, ila ili kuendelea kutenganisha mahakama na utendaji hasa kwa vile wakati kuna mgogoro wa uchaguzi mahakama itahusika, ninadhani kuwa tuwe na utaratibu mwingine wa kuendesha serikali wakati wa Uchaguzi. Kuundwa kwa tume huru ya utumishi serikalini (Civil Service Commission) ni jambo la muhimu sana kiasi kuwa wakati wa uchaguzi shughuli zote za serikali ziendeshwe na tume hii chini ya mwenyekiti wake.
 
Hapana bwana hawako kama sisi. Hivi hiyo 2000 uliona watu wangapi wakipigana mapanga? Wangapi walikufa kutokana na hiyo saga? Aliyeshindwa alikubali, yakaisha, taifa likasonga mbele. Sasa niambie Kenya mshindi wa kweli ni nani na mshindwa ni nani, na kama huyo mshindwa amekubali kushindwa? Wangapi wameshakufa Kenya kutokana na huu uchaguzi wa juzi? Huo utaratibu mzuri unaousema ndio ustaarabu wenyewe kwani si wakati wote mtu utakuwa-favored na sheria lakini kwa vile ni sheria, basi inabidi iheshimiwe. Kwa nini sisi tunashindwa kuwa na utaratibu kama huo? Hivi mtu kama Kibaki kweli ungemtegemea kufanya haya anayotuhumiwa kufanya ukizingatia nafasi aliyokuwa nayo kabla hajawa raisi? Kama sisi sivyo tulivo kwa nini haya mambo yanatokea si ktk nchi moja tu bali nchi kibao Afrika. Angalia Zambia, angalia Zimbabwe walivyo sasa. Juzi nilikuwa naangalia Africa Channel wakimhoji Mugabe. Yaani sasa hivi Wazimbabwe wanatia huruma. Badala ya kuendelea wanazidi kutoendelea. Serikali yao imechapisha noti ya dola 200,000. Umeona wapi hiyo? Aisee nikitaka ninaweza kujaza jamboforum nzima nikizungumzia laana tuliyonanyo.

Hili swala la ugonvi ni kitu kingine, mimi nilikuwa naongelea kuhusu wizi wa kura. Nakubalina nawe kabisa kuwa swala la ugomvi litatatuliwa kwa watu kuwa wastaarabu.
 
Hili swala la ugonvi ni kitu kingine, mimi nilikuwa naongelea kuhusu wizi wa kura. Nakubalina nawe kabisa kuwa swala la ugomvi litatatuliwa kwa watu kuwa wastaarabu.

Kama swala ni wizi wa kura basi sidhani kama Bush aliiba kura. Kilichokuwa kinabishaniwa ni uhesabuji wa kura ambazo kwa namna moja ama nyingine zilikuwa zimeharibika. Unakumbuka mambo ya hanging chad..? Kwa mahesabu ya mwanzo Bush alikuwa anaongoza...so sijui ua uwizi wa kua yametokea wapi tena.
 
Wizi wa kura huwa haufanwyi na mgoimbea mwenyewe bali maajenti wake; nadhani nimezungumza hivyo kumjibu forumite mmoja hapo juu. Tatizo la Bush lilikuwa ni wizi wa kura kwa namna mbili:

(a) Namna ya kwanza ilikuwa ni kutohesabu kura za Al-Gore kwa kutumia visingizio mbalimbali. Cheir returning Officer Cathreen Harris ambaye alikuwa ni Vice-Chair wa Bush Comtee huko florida alikuwa ameweka maajenti wa kufanya jambo hilo katika maeneo yenye democrats wengi.

(b) Namna ya pili ilikuwa ni ku-stuff absentee ballots nyingi sana upande wa Bush na wakati huo huo kupunguza absentee ballots za upande wa Al-Gore.

Bush haukiba kura zile ila maajenti wake ndio waliofanya hivyo wakiongozwa na Cathreen Harris, wala siyo mdogo wake (Jeb Bush.) Matatizo hayo ndiyo tunayotafuta namna ya kuyaondoa.
 
Sina uhakika na hayo unayoyasema. Hivi unajua kuwa Al Gore hakuhitaji kushinda Florida ili awe raisi? Kama angeshinda state nyingine yoyote ile zaidi ya Florida leo hii pengine angekuwa raisi. Sasa maajenti wa Bush walijuaje kama ilikuwa lazima kwa Gore kushinda Florida na si kwa Tennessee au Arkansas kule kwa bosi wake? Kwanini hao maajenti hawakwenda kufanya manjonjo huko kwingine? Gore kama angeshinda TN ama AR ilikuwa imetoka hiyo hata kama Bush angeshinda Florida....
 
Nafikiri unataka tubishane kwa jambo lisilokuwa na ulazima wowote kulingana na mada hii. Ni kweli kuwa Al-Gore hakuhitaji Florida tu, lakini electoral politics pia huwa zina calculations zake. Florida lilikuwa ni jimbo la muhimu sana kwa Al-Gore (na kwa Bush pia) kwa vile hakuwa na uhakika kama angeshinda Pennsylvania ambalo lilikuwa linaongozwa na Tom Ridge wakati huo. Umuhimu wa FL ulipungua baada ya kuwa ameshashinda PA. Kushindwa kwake TN ilikuwa ni kosa lakini kama angeshinda TN na kukosa PA bado asingeshinda urais bila ya kuwa na FL. Mwaka huo 2000 mimi nilikuwa naishi Miami na nakuambia kuwa jamaa walii-invest sana kwenye jimbo hilo siyo mchezo.

Hata hivyo swala nililokuwa nazungumzia mimi siyo politics za USA, bali namna ya kutafuta mbinu angalau za kupunguza wizi wa kura huku kwetu ambako udanganyifu huweza kusababisha mauaji makubwa kama haya tunayoshuhudia Kenya
 
Hiyo ndio solution kaka watu watauuana we mwisho wa sikuRAILA atakubali
solution ni kukaa chini na kuonge jinsi ya kumaliza matatizo,,so hiyo kuuuana isitutishe sana wamekufa rwanda wengi tu mwisho ikapatikana democracy nini kenya:::::tuombe mungu wakumbuke kuwaacha wale watoto wadogo waweze kuongeza nchi baadae,,
 
(1) Australia wana sheria inayowabana watu kupiga kura; nadhani kutokupiga kura ni kosa dogo la jinai. Ni muhimu na sis tuwe na sheria za namna hiyo ili kuhakikisha kuwa kila raia anapiga kura yake yeye mwenyewe hata kama anampigia mtu kwa kununuliwa, mradi tu atumie haki yake ya kidemokrasia. Tukishakamilisha hilo, itaacha nafasi chache sana za ku-stuff kura haramu kwenye ballot box.

(2) Wizi mwingine wa kura hutokea kweye kuhesabu na kujumlisha idadi kura. Ndiyo maana nadhani taifa linatakiwa liweke investament ya kutosha kwenye tume ya Uchaguzi. Kama serikali iliamua kuwalipa mamilion ya fedha maafisa wa TRA kusudi wasiibe, nadhani wakati umefika kuwalipa mamilioni ya fedha maafisa wa uchaguzi kusudi wasimamie ujenzi wa demokrasia sawasawa.

Pointi ya kwanza kidogo inafanya nitafakari, lakini hii ya pili haijaingia kabisa akilini mwangu mkuu, kwani hao wa TRA wanaolipwa mamilioni hawaibi? na mbona karibuni tu tumeona kwenye vyombo vya habari ya kuwa hawa jamaa wanashika bendera kwa wizi! na mamilioni tunawapa kwenye mifuko yao.
Hao Tume miaka mingi imepita wao wanahesabu mabilioni tu na sio milioni, ukija uchaguzi utumbo mtupu! Malipo gani tena wanataka?
Kama Tume za Uchaguzi Africa, hazitakuwa huru, watawala na wenye mamlaka za Dola wataendelea kuwapangia kazi na kuwaingilia katika taratibu zao, Waafrica tutaisikia tu democracy milele na milele.
Kwa mfano:Kivuitu amenukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa hana uhakika na matokeo aliyoyatangaza na kuwa aliyatangaza kutokana na shinikizo na kubanwa na wanasiasa kutoka vyama vikubwa viwili vya PNU cha Kibaki na ODM cha Odinga.

Kivuitu alizidi kubainisha maajabu aliyoyafanya alipoeleza kuwa alikipeleka cheti cha ushindi wa Kibaki Ikulu baada ya baadhi ya watu kutishia kuwa watakichukua na kukipeleka, wakati jukumu hilo ni lake.

Nilipofika Ikulu wakati napeleka cheti, nilimkuta Jaji Mkuu akiwa tayari kumuapisha rais," Kivuitu alinukuliwa na vyombo vya habari akisema.
Source: Tanzania Daima
Hapa utasemaje! malipo?
 
Kitila,

Viongozi waliopigania Uhuru kwa sasa hivi ni wachache sana waliobaki. Tatizo ni kuwa wale waliowarithi wanaijeweka kama wao pia walipigania uhuru.

Maneno msumari kichuguu. Hapo Zanzibar wala sio mbali sana, ukiongelea demokrasia tu, utaambiwa tumepindua na wao wapindue kama wanaweza! Ukiangalia anaeongelea maneno hayo amezaliwa baada ya 1964 au hiyo 1964 alikuwa hajui lolote (mtoto).
Najiuliza kampindua nani?
 
Iwapo anatokea kiongozi wa chama cha siasa chenye wafuasi wengi na kujinadi kuwa hayatambui mapinduzi ya 1964, ambayo ndio hayohayo yaliyobariki mfumo wa vyama vingi unategemea apewe jibu gani?
 
Iwapo anatokea kiongozi wa chama cha siasa chenye wafuasi wengi na kujinadi kuwa hayatambui mapinduzi ya 1964, ambayo ndio hayohayo yaliyobariki mfumo wa vyama vingi unategemea apewe jibu gani?

mzee kibunango unanikumbusha ya malaysia mkuu.

maana nnaona umewakalia kooni kinoma hawa jamaa kila wakijifurukuta ww huwaachi
 
Jamaa wanakera na mifano mfu kuhusu Zenj, eti mtoto hajui mapinduzi! Sidhani kama kuna mtoto ambae anakwenda skuli ambae hatojua mapinduzi ya 1964 ya maana gani.
 
Kwa maoni yangu nadhani kuwa ili uchaguzi uwe wa huru na haki basi yafuatayo yafanyike;

1. Kuwe na tume huru ambayo mwenye kiti wake achaguliwe na wanachi miaka mitatu kabla ya uchaguzi kufanyika.

2. Raisi ajiuzulu kabla ya uchaguzi kufanyika ili aipishe tume huru ifanye kazi yake.

3. Kura zihesabiwe sehemu zinapopigwa na hii ifanyike mara tu baada ya upigaji kura kumalizika.

4. Watu wasikatazwe kuondoka katika vituo vya kura wanaweza kushuhudia kwa kando kidogo uhesabiwaji wa kura.

5. Vyombo vya habari viruhusiwe kufanya coverage ya kuhesabu na kurusha hewa live.

6. returning officers wawe wanafanya kazi hand in hand na agents wa vyama vya siasa.

7. Namba ya maboxi ya kura yaliotumika yajulikane hesabu yake kabla yakuanza kuhesabiwa.
 
Back
Top Bottom