Vijana wa mkoa wa Ruvuma wazindua kampeni na wimbo wa bwela kuni(njoo hapa)

BongeMwepesi

Senior Member
Aug 13, 2013
125
83
Wakiongea na waandishi wa habari na vijana wanaotokea mkoa wa Ruvuma miongoni mwao wakiwa wasanii wamezindua kampeni ya Bwela Kuni( Njoo Hapa). Hii ni press release iliyoletwa na mratibu wa kampeni hiyo.

UZINDUZI RASMI WA KAMPENI YA BWELA KUNI & NA KUACHIWA RASMI KWA WIMBO WA BWELA KUNI.
Mkoa wa ruvuma kihistoria ni mkoa uliobarikiwa na unaofahamika kwa kuwa na wasanii wa nyanja mbalimbali wakiwamo wanamuzik,waimbaji,wacheza ngoma na waigizaji.

baadhi ya wanamuziki na wasanii wenye asili ya mkoa wa ruvuma waliovuma na wanaoendelea kuvuma ni mwanamuziki mkongwe aliyekuwa akiimba nyimbo za dansi na sasa nyimbo za injili Cosmas Chidumule,marehemu Dr.Remmy Ongala ambaye baada ya kutoka kongo aliishi katika mkoa wa ruvuma kijiji cha matimila na baadae alikuja kuwa moja ya wanamuziki wa bendi ya super matimila,pia kwa sasa kuna wanamuziki na wasanii wengine wengi katika tasnia mbalimbami wenye asili ya mkoa wa ruvuma na ambao wanafanya vizuri,baadhi yao ni msanii nguli wa mziki wa bongo flavor Prof.Jay,Mrisho Mpoto,Godzilla,Shetta,Suprano,mwana kwaya mkubwa na nguli Mh. Captain John Komba, Jokate, rose Ndauka, marehemu Juma Kilowoko (Sajuki), marehemu Recho Haule (wapumzike kwa amani),na maproducer wakubwa kama c9 kanjenje, Mr.T touch na wengine wengi.

Hakika ni ukweli usiopingika kwamba vijana wengi wenye asili au wanaotokea mkoa wa ruvuma wamebarikiwa vipaji katika sanaa(muziki,uigizaji,dansing) lakini mara nyingi wamekuwa wakikwamishwa na jinsi gani ya kuweza kufikia malengo yao kwa kutambulika na kupata fursa katika majukwaa ya kitaifa na kimataifa.

Kwa hiyo kutokana na hilo wadau mbalimbali vijana pamoja na c9 kanjenje ambaye ni producer mkubwa wa studio za c9 kwa kushirikiana na wasanii wa mziki wa kizazi kipya,injili ,wasanii wa kuigiza wakaona kuna haja ya kufanya kitu katika hili na ndipo wazo la kuanzisha mradi huu wa Bwela Kuni ndio ukazaliwa.

Bwela Kuni ni nini? Neno la kingoni lenye maana ya (Njoo hapa)
Hii ni kampeni maalumu iliyoanzishwa na vijana wanaotokea na wenye asili ya mkoa wa Ruvuma wakiwemo pia wasanii wa mziki wa kizazi kipya, wasanii wa mziki wa injili, waigizaji na wasanii wengine wa kada tofauti tofauti kwa madhumuni ya kuweza kuamsha hali na hamasa ya wananchi wa mkoa huu na wenye asili ya mkoa huu na watanzania kwa ujumla,kuweza kutangaza sifa za mkoa huu,historia ya mkoa,tamaduni za watu wa mkoa,fursa mbalimbali zipatikanazo katika mkoa huu,ikiwemo fursa za uwekezaji katika kilimo, utalii, biashara, Elimu na uvuvi kupitia sanaa.Vilevile kuweza kutangaza vipaji vya wasanii hawa,uwezo wao na kujitambulisha kitaifa na kimataifa hatimaye kutumia vipaji vyao vya sanaa kama sehemu kubwa ya kujipatia ajira.

Kampeni hii kwa kuanza imewaunganisha wasanii vijana wenye asili ya mkoa wa Ruvuma kuandaa na kurecord nyimbo inayoitwa "bwela kuni" ambayo imeandaliwa na mtayarishaji wa muziki naye mwenye asili ya mkoa wa ruvuma bwana c9 kanjenje na nyimbo hii ndiyo inabeba dhima ya project nzima.
Tunaamini kupitia kampeni hii vijana wataweza kuamsha hali na hamasa kote Tanzania kuhusu sifa na mazuri yapatikanayo katika mkoa wa Ruvuma na wataonyesha vipaji vyao na kuonekana na wadau mbalimbali wa sanaa atimaye kupata nafasi katika ulimwengu wa sanaa na burudani.

Uzinduzi rasmi wa kampeni hii utafanyika mkoani Ruvuma mwisho wa mwezi wa tisa, ambapo utaambatana na uhamasishaji wa fursa mbalimbali na sanaa katika wilaya zote za mkoa huu na jumla ya ziara zote itafanyika songea kwa kuwaunganisha watu waliofanikio wenye asili ya mkoa huu katika Nyanja mbalimbali kama wanataaluma,wafanyabiashara,madaktari,viongozi wasanii ambao ni wachanga na wasanii waliofanikiwa na wenye majina makubwa katika sanaa na wenye asili ya mkoa wa ruvuma kuweza kukutana na wananchi wa mkoa wa Ruvuma na vijana wachanga wenye vipawa mbalimbali kuweza kuwahamasisha na kupeana mbinu mbalimbali kuweza kufanikiwa katika maisha na katika sanaa.pia tunategemea kuwe na tamasha kubwa kabisa la sanaa na muziki katika viwanja vya majimaji vikihusisha wasanii wenye asili ya mkoa huu.

Wimbo Wa Bwela Kuni ambao umebeba dhima ya project hii, umeimbwa na wasanii wa muziki wa kizazi kipya(bongo flavor) na wanamuziki wa gospel. Jumla ya wasanii kumi na tano wameshiriki katika kutunga na kuimba wimbo huu wa bwela kuni wasanii hao ni Herieth Ndosi(ambaye ni mwanamuziki wa nyimbo za injili),Single J,G luck, Cammy Bway, Roby Songea,Gemy Rymez,Fobyone,Bad H badilika,G Van,Zero Wiz, FM, HDM, Full P,Tony na D Pesa.

Wasanii walioimba wimbo huu ni wasanii wenye vvipaji vya hali ya juu na wanafanya mziki kwa muda sasa.Wimbo huu kama unavyoitwa bwela kuni "njoo hapa" mashairi yake yamelenga kuueleza sifa za mkoa wa ruvuma na watu wake katika kila nyanja kiuchumi,kihistoria,kiutamaduni na mambo mbalimbali yanayohusu mkoa.

Wimbo umezungumzia utamaduni,utamaduni wa watu wa mkoa huu ni wacheshi,wenye upendo,wapenda amani na ni watu wasikivu sana.
Wimbo umwezungumzia historia ,katika historia ni kwamba mkoa huu una historia nzuri ya wapigania uhuru especially vita ya majimaji na pia kuna makumbusho ya wapiganaji uhuru wa kingoni.

Wimbo umezungumzia fursa za uwekezaji,kwa wawekezaji ni kuwa tunawakalibisha kuja kuwekeza katika mkoa wa ruvuma kwenye sekta mbalimbali.
Wakulima waje kuwekeza kwenye mkoa wa ruvuma sababu ni mkoa wenye ardhi kubwa na shughuli za kilimo na ni mmoja kati ya mikoa mikubwa minne inayoongoza katika uzalishaji wa chakula,
Utalii,kuna vivutio vya utalii,makumbusho ya taifa ya vita vya majimaji,pia mbuga ya wanyama ya selous.

Wafanyabiashara kuwekeza katika biashara na shughuli mbalimbali sababu katika mkoa wa ruvuma ndio sehemu inayopatikana uranium na project kubwa ya mkuju river inaendelea pale.

Wavuvi pia kuna ziwa nyasa ambalo ni maarufu kwa uvuvi hasa uvuvi wa dagaa watamu sana wanaitwa dagaa nyasa.
Vyuo vikuu, kuna vyuo vikuu vya st.joseph, utumishi wa umma, open university, st.augustine, kwa hiyo kuna fursa kwa wenye vyuo waweze leta huku, pia watu kujenga hosteli.

Hitimisho:
Tunawaomba na tunawaita wadau mbalimbali kote Tanzania,Wawekezaji,wakulima,wafanya biashara,wanataaluma,viongozi ,wadau wa utalii na mariasili na wadau wa sanaa na muziki waje kutumia fursa zipatikanazo katika mkoa huu wa Ruvuma,kuwekeza katika fursa hizi na kuwekeza kwa vijana hawa na wengine wengi wenye vipawa mbalimbali, kwa mameneja wa sanaa kuweza kujitokeza kuwaangalia na kuwachukua vijana wanaoona wanafaa kuingia kwenye label na kampuni zao, kwa waandaaji wa matamasha na wadau wengine wa mziki kuweza kutambua vipaji hivi na kuvipa nafasi kuweza kusikika na kuwepo kwenye matamasha na majukwaa ya muziki.

kwa viongozi na wizara kuweza kusaidia na kuwatumia vijana hawa wenye vipaji vipaji vya hali ya juu katika uhamasishaji wa mambo yenye tija katika nchi yetu.

Kama tulivyosema kuwa hii project ni endelevu tunategemea itatuletea hali, hamasa, umoja, upendo, mshikamano miongoni mwa vijana na watanzania wote kwa ujumla.

Sanaa ni Maisha, Sanaa ni Burudani, Sanaa ni Ajira
 
Back
Top Bottom