Jumla ya Askari Polisi 15 watunukiwa Vyeti vya Heshima Mkoani Ruvuma

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,989
aa8dc3c1-e8a8-4734-a29f-41bd86c96315.jpeg
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Marco G. Chilya amewataka Wakaguzi wa Polisi, Askari wa vyeo mbalimbali na watumishi raia ndani ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma kufanya kazi kwa kuzingatia haki, weledi na uadilifu katika kutoa huduma bora kwa wananchi ili kuweza kufikia lengo la Mkuu wa Jeshi la Polisi na Mhe, Raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan .

Hayo ameyasema leo Januari 11, 2023 katika Viwanja vya Kikosi Cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Ruvuma baada ya zoezi la utoaji wa zawadi kwa wakaguzi, Askari wa vyeo mbalimbali na mtumishi raia waliofanya vizuri zaidi katika kutoa mchango mzuri katika utendaji wa kazi wa kuimalisha Ulinzi na Usalama wa raia na Mali zao kwa kuzingatia haki na weledi na uadilifu katika kipindi cha mwaka 2023 ikiwa ni maadhimisho ya Family Police day.
a09daa8f-c9a1-44aa-b5a4-e3ef56a801e5.jpeg

04124fcc-1074-4e70-a6d0-ca0ce3419ff1.jpeg
Akiongea Kamanda Chilya (ACP) amesema kuwa zawadi hizo za heshima zilizotolewa ziwe chachu ya kwenda kufanya vizuri zaidi katika kipindi cha mwaka 2024 katika kutekeleza majukumu
ya kazi zao.

Aidha, aliongeza kwa kuwataka askari wote Mkoani Ruvuma kuhakikisha wanaongeza jitihada zaidi katika utendaji wao wa kazi ili kufanya vizuri zaidi katika kipindi cha mwaka 2024 na kufikia dhima na lengo la Jeshi la Polisi Tanzania katika kutoa huduma bora kwa wananchi sambamba na kuzuia, kutanzua na kufichua vitendo na viashiria vyote vya uhalifu.

Sanjari na utoajia wa zawadi pia Kamanda Chilya alikagua Gwaride la heshima lililoandaliwa pamoja na kukagua umahili wa maonyesho ya medani za kivita yaliyofanywa na askari wa F.F.U Ruvuma.
b0a13746-945a-41b1-b38f-ff0274cc5338.jpeg

c1c43e55-8df7-4f66-a3b4-ef89bb6d4b7b.jpeg

1c68474d-cacd-4321-8108-01927cdab20c.jpeg
 
Back
Top Bottom