Vijana wa kiume kwa mfumo huu uliopo nchini chukueni maamuzi magumu

JABALI LA KARNE

JF-Expert Member
Apr 19, 2021
3,093
5,816
Vijana tegemezi wa kiume ambao ni graduates wanaongezeka sababu kazi zao zimeshikwa na dada zao wanaobebwa na mfumo wa Huyu ni Mwanamke, tumpe nafasi mwanamke, Haki sawa, Usishindane na mwanamke n.k.

Mabinti graduate wanapata kazi mapema kuliko vijana wa kiume, matokeo yake hata waoaji wanapungua kwa sababu ya uoga wa maisha ya majukumu ya ndoa na kuoa binti mwenye ajira aliyesoma.

USHAURI:
Vijana hakuna jinsi, tafuteni system nzuri ya kuingia mashambani. Serikali haiwezi kutoa ajira kwa wingi uliopo halafu binti wa kike anapewa kipaumbele kwenye ajira chache zilizopo. Huku mtaani hali ni mbaya. Vijana wengi ninaokutana nao wanahitaji msaada na si rahisi kuwasaidia wote.
 
Kuingia shambani ni ngum kwasababu haikua ndoto kurudi shamba lakin Haina namna itabidi turudi shamba maana maisha huwa hayana huruma kwa wavivu
Kuna mkakati wa mikopo kwa wakulima unakuja,MUNGU akisaidia ukifanikiwa ukukute eneo husika. Ombeni tu ufanikiwe.
 
Umeona mbali sas sisi vijana tungepata izo nafasi tukaoa wanapewa wanawake ambao pesa zao kujiremba hawahusiki katika majukumu ya ndoa
Na ndipo tatizo lilipo.

Kijana wa kiume anaambiwa ni jukumu lako kuoa, kutunza familia na kumtunza mke wako.

Huyo huyo kijana wa kiume anapoenda kwenye interview anakutana na ushindani kutoka kwa mwanamke ambaye anatakiwa aje amtunze, mwanamke anachukua nafasi yake ya ajira halafu jamii inategemea kijana aanzishe familia kwa kufunga ndoa na huyo mwanamke halafu wamnyooshee kidole kuwa hatimizi majukumu yake kama mwanaume.

Jamii inasahau kuwa wanamuandaa kijana kuwa mume halafu wanamnyima vitendea kazi vya kuwa mume kisha wanampa mwanamke na kusahau kuwa huyo mwanamke atahitaji mume mwenye vitendea kazi.

Matokeo yake vijana wapo mtaani wake zao ambao wanatakiwa waolewe na hao vijana wapo makazini.
 
Vijana tegemezi wa kiume ambao ni graduates wanaongezeka sababu kazi zao zimeshikwa na dada zao wanaobebwa na mfumo wa Huyu ni Mwanamke, tumpe nafasi mwanamke, Haki sawa, Usishindane na mwanamke n.k.

Mabinti graduate wanapata kazi mapema kuliko vijana wa kiume, matokeo yake hata waoaji wanapungua kwa sababu ya uoga wa maisha ya majukumu ya ndoa na kuoa binti mwenye ajira aliyesoma.

USHAURI:
Vijana hakuna jinsi, tafuteni system nzuri ya kuingia mashambani. Serikali haiwezi kutoa ajira kwa wingi uliopo halafu binti wa kike anapewa kipaumbele kwenye ajira chache zilizopo. Huku mtaani hali ni mbaya. Vijana wengi ninaokutana nao wanahitaji msaada na si rahisi kuwasaidia wote.
wasipoolewa na vijana wataolewa na rika la baba zao hata mke wa nne, kwani kuna shida gani? wanachoangalia wao sinipesa au?

vijana nao wakishajipanga vya kutosha wataoa rika la watoto wao, kwani sh. ngapi? maisha yanaendelea.
 
Sasa tukienda hivyo tutakuwa na jamii iliyojaa single mother wengi sana sababu wazee si waoaji kutokana na hofu ya kunyooshewa vidole kuoa binti zao na kutakuwa na mmomonyoko mkubwa wa maadili sababu ya ongezeko la watu kutembea na binti zao.

Mwisho sababu vijana wengi hawaajiriwi, kama hawatatafuta mbadala kutakuwa na wazee wengi wasio na pesa bali wazee tegemezi hivyo hata hao waoaji wazee hawatakuwepo.
 
Marehemu mzee reginald alimuoa jack hatukuona vidole vikinyooshwa.
 
solution ni kwenda shambani kama tu kijana aliandaliwa kwenda shambani tangu akiwa shule huko...

sio mtoto wa watu mmesomesha awe mwalimu na mkopo mlipatia asilimia 100 mwisho mnageuka eti ajira hamna nenda shambani, hilo shamba analielewa kwa siku moja au?
 
Shambani ni mbadala wa yeye kijana wa kiume kujinasua ikiwa hali itaendelea kuwa hivi. Angalau kuna nafasi ya kujinasua shambani kuliko kukaa mjini na kuangalia namna unavyotafunwa na maisha ukiwa hai.

Halafu huwezi jua huko shambani utakutana na fursa gani inayohusisha elimu yako uliyoisotoea kwa miaka mingi.
 
Wamepigika sana hao wanawake/wasichana kwa HONGO TENDO.. yaani kwa rushwa ya ngono na sisi sisi wanaume tuliokuwaga madarakani na vijisecta fulani kwa kudai tendo ili tuwape kazi wameshika kijiti sasa ..waacheni
 
Back
Top Bottom