Vijana tusipitwe na hizi fursa!!

Hii kimara au ubungo unayoizungumzia ina shida ya maji ni ya mkoa gani?? Kama dar utakuwa hujafanya research vzr.maji kimara sahizi yanatoka kila siku.na hapa nipo sehem wanaunga bomba lingine lipitishe maji mtaani.kiufupi kwa sasa kimara hakuna shida ya maji
 
Hii kimara au ubungo unayoizungumzia ina shida ya maji ni ya mkoa gani?? Kama dar utakuwa hujafanya research vzr.maji kimara sahizi yanatoka kila siku.na hapa nipo sehem wanaunga bomba lingine lipitishe maji mtaani.kiufupi kwa sasa kimara hakuna shida ya maji

mkuu Kibajajitz , kwahiyo saahivi maeneo yote ya Ubungo na Kimara shida ya maji is no more? ofkoz mimi sio mkazi wa maeneo hayo, na nilikuwa nataka nikaifanye hiyo biashara ya kuuza maji ya kisima kwenye maeneo hayo.
 
mkuu Kibajajitz , kwahiyo saahivi maeneo yote ya Ubungo na Kimara shida ya maji is no more? ofkoz mimi sio mkazi wa maeneo hayo, na nilikuwa nataka nikaifanye hiyo biashara ya kuuza maji ya kisima kwenye maeneo hayo.
Ni hakuna kiongozi na mradi unazidi endelea kupelekwa soon kimara yote itakuwa masaki 24hrs maji.mimi naishi huku kimara.hata zile gari za kuuza maji hazipo mtaani.wale wafanya biashara wa maji sahizi imekula kwao wamebaki na matank yao tu.
 
Fursa isiyo na ma uzwazwa ni Forex Trading tu...
Ofisi yako ni Computer yako na Simu yako tu....
Hayo ma fursa sijui uanze kutafuta kiwanja, sijui leseni, wateja, mara majambazi wakuvamie.

Nilifungua Biashara ya Samaki Wabichi Tabora, ikafa...
Nimefungua banda la Chips Mwananyamala kwa Kopa, ikafa...
Nimeingia kwenye Matikiti, nimekutana na figisu kibao kwenye masoko ya Buguruni na Tandika.
Upumbavu tu... Forex ndio kila kitu.

sawa
 
1. Kuuza maji
kwa walioko dsm kuanzia kimara,ubungo tabata na maeneo mengine mengi maji ni shida
Unafanyaje?
Kama una mtaji na eneo unaweza kuchima kisima na kuanza kuuza maji, pia kama huna eneo unaweza kuingia mkataba na mmiliki wa eneo utakaloona linafaa ukachimba kisima then mkakubaliana maybe (utachukua mapato kwa miaka mitano au saba na kumwachia kisima) au vinginevyo lkn kimaandishi na kisheria.
Wachimbaji wapo karibu chuo cha maji (ubungo) na maeneo mengine.
Kama huna mtaji wa kuchimba kisima unaweza kununua madum unakodi kirikuu(kinapakia madumu mpaka 50), tafuta migahawa, bar hata 5 tu uwahakikishie kuwapelekea maji kila siku, soko ni la uhakika.

2.Kuuza na kutengeneza vifaa vya simu na simu mf memory card, flash, ear phone, head phone, phone covers nk
Hapa nimelenga zaidi maeneo ya vyuo na hostel wengi wanauza ila hawatengenezi, ukiwa na fundi simu hiv vifaa unauza sana.

3.Kununua na kuuza ngozi za ng'ombe mbuzi nk
Hii nina uzoefu mdogo ila ni biashara yenye pesa sana kwani ngozi inauzwa kwa kilograms 5000@kg kwa bei ya zaman kidogo
So ukipata ngozi yenye 8kg 5000*8=40,000
Ngozi hiyo unaweza kununua machinjioni 5000_10000

4.Kutengeneza chaki
Hii ni fursa ya kuanzisha viwanda vidogo vidogo hasa kwa vijana mlioko maeneo yanayozalisha chokaa kwa wingi mkajiunga na kuchukua mikopo( mill 50 za uncle Magu kwa kila kijiji) na mkaanza kazi.
Soko lake ni la uhakika mnaongea na watu wa halmashauri wanaweza kuwapa tenda kwenye shule za serikali.Pia private schools vyuo nk

5.Kununua na kuuza dhahabu na madini mengine
Najua hapa watu wengi wanaogopa na kudhani biashara hii ni ya akina Mengi pekee
Sio kweli!!
Mfano; Gram 1 ya dhahabu kwasasa inauzwa 70000 (Dodoma)
Ukiwa na laki7 unapata gram 10
Ukiwa na 1.4mil unapata gram20
1gm sokoni(dsm) ni kuanzia 86000_93000
86000_70000=16000@gm
16000*20=320000 per trip.
Ma expats wapo humu watajazia nyama..
Note:Kama ni mgeni ni lazima umtafute mzoefu akusaidie kujua machimbo, mzigo original, soko nk
inahitaji research ya muda mrefu kidogo kabda hujaamua kuifanya.
USIINGIE KICHWA KICHWA HAPA.

6.Kilimo cha green house


My take; kulalamika tu hakuwezi kutukwamua tulipo,
magroup ya watsap, fb na mengineyo tuyatumie pia kwenye ujasiriamali kupeana fursa ktk maeneo tulipo na kuwezeshana bila kinyongo.
Tukifanya hivyo naamini tutafika.

Nawasilisha!!!
 
Mkuu hiki kilimo cha greenhouse umewahi kukifanya? Kama jibu lako ni ndio hebu tueleze kwaufupi changamoto ulizokutana nazo mpaka udiriki kuwaonya watu wasikifanye!
Ndio, na mpaka nasema hvyo ujue Nina uhakika, but kama mwaniona muongo dumbukizeni hizo million 8-10 then mtuletee mrejesho

Maybe Kwa wale watakao lima maeneo yenye baridi ndo wanaweza kuambulia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom