Vijana tusipitwe na hizi fursa!!

1. Kuuza maji
kwa walioko dsm kuanzia kimara,ubungo tabata na maeneo mengine mengi maji ni shida
Unafanyaje?
Kama una mtaji na eneo unaweza kuchima kisima na kuanza kuuza maji, pia kama huna eneo unaweza kuingia mkataba na mmiliki wa eneo utakaloona linafaa ukachimba kisima then mkakubaliana maybe (utachukua mapato kwa miaka mitano au saba na kumwachia kisima) au vinginevyo lkn kimaandishi na kisheria.
Wachimbaji wapo karibu chuo cha maji (ubungo) na maeneo mengine.
Kama huna mtaji wa kuchimba kisima unaweza kununua madum unakodi kirikuu(kinapakia madumu mpaka 50), tafuta migahawa, bar hata 5 tu uwahakikishie kuwapelekea maji kila siku, soko ni la uhakika.

2.Kuuza na kutengeneza vifaa vya simu na simu mf memory card, flash, ear phone, head phone, phone covers nk
Hapa nimelenga zaidi maeneo ya vyuo na hostel wengi wanauza ila hawatengenezi, ukiwa na fundi simu hiv vifaa unauza sana.

3.Kununua na kuuza ngozi za ng'ombe mbuzi nk
Hii nina uzoefu mdogo ila ni biashara yenye pesa sana kwani ngozi inauzwa kwa kilograms 5000@kg kwa bei ya zaman kidogo
So ukipata ngozi yenye 8kg 5000*8=40,000
Ngozi hiyo unaweza kununua machinjioni 5000_10000

4.Kutengeneza chaki
Hii ni fursa ya kuanzisha viwanda vidogo vidogo hasa kwa vijana mlioko maeneo yanayozalisha chokaa kwa wingi mkajiunga na kuchukua mikopo( mill 50 za uncle Magu kwa kila kijiji) na mkaanza kazi.
Soko lake ni la uhakika mnaongea na watu wa halmashauri wanaweza kuwapa tenda kwenye shule za serikali.Pia private schools vyuo nk

5.Kununua na kuuza dhahabu na madini mengine
Najua hapa watu wengi wanaogopa na kudhani biashara hii ni ya akina Mengi pekee
Sio kweli!!
Mfano; Gram 1 ya dhahabu kwasasa inauzwa 70000 (Dodoma)
Ukiwa na laki7 unapata gram 10
Ukiwa na 1.4mil unapata gram20
1gm sokoni(dsm) ni kuanzia 86000_93000
86000_70000=16000@gm
16000*20=320000 per trip.
Ma expats wapo humu watajazia nyama..
Note:Kama ni mgeni ni lazima umtafute mzoefu akusaidie kujua machimbo, mzigo original, soko nk
inahitaji research ya muda mrefu kidogo kabda hujaamua kuifanya.
USIINGIE KICHWA KICHWA HAPA.

6.Kilimo cha green house

My take; kulalamika tu hakuwezi kutukwamua tulipo,
magroup ya watsap, fb na mengineyo tuyatumie pia kwenye ujasiriamali kupeana fursa ktk maeneo tulipo na kuwezeshana bila kinyongo.
Tukifanya hivyo naamini tutafika.

Nawasilisha!!!
Mkuu ubarikiwe sana ntumie Pm namba zako nikutafute, kuusu Biashara ya Ngozi huwa nasafirisha sana mazao kutoka vijijini kuja mijini sasa huwa nakutana na Ngozi Nyingi sana sikujua kama ni dili
 
mkuu, nami niruhusu nikuPM unipe ABCs kuhusu biashara ya mazao kutoa vijijini to mijini.

-Kaveli-
 
Fursa isiyo na ma uzwazwa ni Forex Trading tu...
Ofisi yako ni Computer yako na Simu yako tu....
Hayo ma fursa sijui uanze kutafuta kiwanja, sijui leseni, wateja, mara majambazi wakuvamie.

Nilifungua Biashara ya Samaki Wabichi Tabora, ikafa...
Nimefungua banda la Chips Mwananyamala kwa Kopa, ikafa...
Nimeingia kwenye Matikiti, nimekutana na figisu kibao kwenye masoko ya Buguruni na Tandika.
Upumbavu tu... Forex ndio kila kitu.

Hahahaa Padri Mcharo , vipi wewe tayari ushaanza kuvuta mkwanja kwenye forex? au bado kwa training?

-Kaveli-
 
Fursa isiyo na ma uzwazwa ni Forex Trading tu...
Ofisi yako ni Computer yako na Simu yako tu....
Hayo ma fursa sijui uanze kutafuta kiwanja, sijui leseni, wateja, mara majambazi wakuvamie.

Nilifungua Biashara ya Samaki Wabichi Tabora, ikafa...
Nimefungua banda la Chips Mwananyamala kwa Kopa, ikafa...
Nimeingia kwenye Matikiti, nimekutana na figisu kibao kwenye masoko ya Buguruni na Tandika.
Upumbavu tu... Forex ndio kila kitu.

Forex traders always work smart
a91b2a98fdd0b96a8affb6d0e6cfa0cf.jpg
 
Hapo kwenye kuuza maji ukipata pikipiki yenye miguu mitatu ukaweka vzr kule nyuma unaweza beba hadi dumu 40...kwa bei ya dar dumu 500×40=20000 toa mafuta na gharama za maji ni kama max 10000...piga raound 5 kwa siku ndo utanielewa vzr...hiyo ya ngozi kweli kuna bro ndo biashara yake sijui wanafanyaje naitamani htr nilipo ngozi nyingi sn
 
Fursa isiyo na ma uzwazwa ni Forex Trading tu...
Ofisi yako ni Computer yako na Simu yako tu....
Hayo ma fursa sijui uanze kutafuta kiwanja, sijui leseni, wateja, mara majambazi wakuvamie.

Nilifungua Biashara ya Samaki Wabichi Tabora, ikafa...
Nimefungua banda la Chips Mwananyamala kwa Kopa, ikafa...
Nimeingia kwenye Matikiti, nimekutana na figisu kibao kwenye masoko ya Buguruni na Tandika.
Upumbavu tu... Forex ndio kila kitu.
wengine wageni mtaji lak 2 kwa wiki unapata ngap
 
1. Kuuza maji
kwa walioko dsm kuanzia kimara,ubungo tabata na maeneo mengine mengi maji ni shida
Unafanyaje?
Kama una mtaji na eneo unaweza kuchima kisima na kuanza kuuza maji, pia kama huna eneo unaweza kuingia mkataba na mmiliki wa eneo utakaloona linafaa ukachimba kisima then mkakubaliana maybe (utachukua mapato kwa miaka mitano au saba na kumwachia kisima) au vinginevyo lkn kimaandishi na kisheria.
Wachimbaji wapo karibu chuo cha maji (ubungo) na maeneo mengine.
Kama huna mtaji wa kuchimba kisima unaweza kununua madum unakodi kirikuu(kinapakia madumu mpaka 50), tafuta migahawa, bar hata 5 tu uwahakikishie kuwapelekea maji kila siku, soko ni la uhakika.

2.Kuuza na kutengeneza vifaa vya simu na simu mf memory card, flash, ear phone, head phone, phone covers nk
Hapa nimelenga zaidi maeneo ya vyuo na hostel wengi wanauza ila hawatengenezi, ukiwa na fundi simu hiv vifaa unauza sana.

3.Kununua na kuuza ngozi za ng'ombe mbuzi nk
Hii nina uzoefu mdogo ila ni biashara yenye pesa sana kwani ngozi inauzwa kwa kilograms 5000@kg kwa bei ya zaman kidogo
So ukipata ngozi yenye 8kg 5000*8=40,000
Ngozi hiyo unaweza kununua machinjioni 5000_10000

4.Kutengeneza chaki
Hii ni fursa ya kuanzisha viwanda vidogo vidogo hasa kwa vijana mlioko maeneo yanayozalisha chokaa kwa wingi mkajiunga na kuchukua mikopo( mill 50 za uncle Magu kwa kila kijiji) na mkaanza kazi.
Soko lake ni la uhakika mnaongea na watu wa halmashauri wanaweza kuwapa tenda kwenye shule za serikali.Pia private schools vyuo nk

5.Kununua na kuuza dhahabu na madini mengine
Najua hapa watu wengi wanaogopa na kudhani biashara hii ni ya akina Mengi pekee
Sio kweli!!
Mfano; Gram 1 ya dhahabu kwasasa inauzwa 70000 (Dodoma)
Ukiwa na laki7 unapata gram 10
Ukiwa na 1.4mil unapata gram20
1gm sokoni(dsm) ni kuanzia 86000_93000
86000_70000=16000@gm
16000*20=320000 per trip.
Ma expats wapo humu watajazia nyama..
Note:Kama ni mgeni ni lazima umtafute mzoefu akusaidie kujua machimbo, mzigo original, soko nk
inahitaji research ya muda mrefu kidogo kabda hujaamua kuifanya.
USIINGIE KICHWA KICHWA HAPA.

6.Kilimo cha green house

My take; kulalamika tu hakuwezi kutukwamua tulipo,
magroup ya watsap, fb na mengineyo tuyatumie pia kwenye ujasiriamali kupeana fursa ktk maeneo tulipo na kuwezeshana bila kinyongo.
Tukifanya hivyo naamini tutafika.

Nawasilisha!!!
Asante mkuu kwa kutufungua mawazo Allah akulipe
 
Mkuu Zillion natoa shukrani za dhati kwa niaba ya wana Jf wote.

Hapo kwenye biz ya ngozi,binafs niliwahi fanya biashara ya ng'ombe wa nyama pale V'nguti na Ukonga na ngozi mbichi nlikua napata 10,000 mpk 15,000 ss ila sijawahi kuifatilia

Huko Himo wakenya wananunuaje?

Na una taarifa zozote kuhusu biz ya zabibu nchini Kenya na miji yake?
 
Wakenya wananunua kwa kg mkuu,
Kwasasa sijajua bei halisi sokoni ila mwaka 2015 1kg ilikuwa inauzwa 5000 wanakuja wenyewe kununua na watz wengine hupeleka wenyewe.
Nasikia Morogoro pia kuna kiwanda cha kusindika ngozi ila sijui wananunuaje

Zabibu sina ufahamu kwa soko la nje, ila msimu uliopita viwandani walinunua 2000-2500@kg hii ni kwa Dodoma.
Ni bei ndogo kwakweli.
 
Fursa isiyo na ma uzwazwa ni Forex Trading tu...
Ofisi yako ni Computer yako na Simu yako tu....
Hayo ma fursa sijui uanze kutafuta kiwanja, sijui leseni, wateja, mara majambazi wakuvamie.

Nilifungua Biashara ya Samaki Wabichi Tabora, ikafa...
Nimefungua banda la Chips Mwananyamala kwa Kopa, ikafa...
Nimeingia kwenye Matikiti, nimekutana na figisu kibao kwenye masoko ya Buguruni na Tandika.
Upumbavu tu... Forex ndio kila kitu.
NDO WANAFANYAJE HAO FOREX MKUU
 
Wakenya wananunua kwa kg mkuu,
Kwasasa sijajua bei halisi sokoni ila mwaka 2015 1kg ilikuwa inauzwa 5000 wanakuja wenyewe kununua na watz wengine hupeleka wenyewe.
Nasikia Morogoro pia kuna kiwanda cha kusindika ngozi ila sijui wananunuaje

Zabibu sina ufahamu kwa soko la nje, ila msimu uliopita viwandani walinunua 2000-2500@kg hii ni kwa Dodoma.
Ni bei ndogo kwakweli.
Ngozi 1 ya ng'ombe ikishakauka inakuwa na wastani wa kg ngapi?

Zabibu msimu huu wamenunua mpk 1500 mkuu,,yani ni zaidi ya shida
 
mkuu samahani unaweza nipa ramani ya fursa ya ununuzi wa madini? Nimeupnda
Mkuu,
Madini hasa dhahabu yanapatikana maeneo mengi sana hapa Tz mf: Tanga, Mbeya, Dodoma, Geita, Mwanza, Mara, Shinyanga nk mfano Dodoma(wilaya ya Bahi wanchimba sana
Mtu yeyote ukienda na pesa cash unauziwa mzigo hapo mgodini wewe unapeleka dar Kkoo (wahindi wananunua kwa wingi na kusafirisha)
Sehemu nyingi za wachimbaji wadogo huwa wanauza kwa mteja yeyote anayepatikana.
Bei ni kama nilivyoainisha hapo awali.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom