Vijana tusipitwe na hizi fursa!!

Zillion

JF-Expert Member
May 15, 2017
1,358
1,819
1. Kuuza maji
kwa walioko dsm kuanzia kimara,ubungo tabata na maeneo mengine mengi maji ni shida
Unafanyaje?
Kama una mtaji na eneo unaweza kuchima kisima na kuanza kuuza maji, pia kama huna eneo unaweza kuingia mkataba na mmiliki wa eneo utakaloona linafaa ukachimba kisima then mkakubaliana maybe (utachukua mapato kwa miaka mitano au saba na kumwachia kisima) au vinginevyo lkn kimaandishi na kisheria.
Wachimbaji wapo karibu chuo cha maji (ubungo) na maeneo mengine.
Kama huna mtaji wa kuchimba kisima unaweza kununua madum unakodi kirikuu(kinapakia madumu mpaka 50), tafuta migahawa, bar hata 5 tu uwahakikishie kuwapelekea maji kila siku, soko ni la uhakika.

2.Kuuza na kutengeneza vifaa vya simu na simu mf memory card, flash, ear phone, head phone, phone covers nk
Hapa nimelenga zaidi maeneo ya vyuo na hostel wengi wanauza ila hawatengenezi, ukiwa na fundi simu hiv vifaa unauza sana.

3.Kununua na kuuza ngozi za ng'ombe mbuzi nk
Hii nina uzoefu mdogo ila ni biashara yenye pesa sana kwani ngozi inauzwa kwa kilograms 5000@kg kwa bei ya zaman kidogo
So ukipata ngozi yenye 8kg 5000*8=40,000
Ngozi hiyo unaweza kununua machinjioni 5000_10000

4.Kutengeneza chaki
Hii ni fursa ya kuanzisha viwanda vidogo vidogo hasa kwa vijana mlioko maeneo yanayozalisha chokaa kwa wingi mkajiunga na kuchukua mikopo( mill 50 za uncle Magu kwa kila kijiji) na mkaanza kazi.
Soko lake ni la uhakika mnaongea na watu wa halmashauri wanaweza kuwapa tenda kwenye shule za serikali.Pia private schools vyuo nk

5.Kununua na kuuza dhahabu na madini mengine
Najua hapa watu wengi wanaogopa na kudhani biashara hii ni ya akina Mengi pekee
Sio kweli!!
Mfano; Gram 1 ya dhahabu kwasasa inauzwa 70000 (Dodoma)
Ukiwa na laki7 unapata gram 10
Ukiwa na 1.4mil unapata gram20
1gm sokoni(dsm) ni kuanzia 86000_93000
86000_70000=16000@gm
16000*20=320000 per trip.
Ma expats wapo humu watajazia nyama..
Note:Kama ni mgeni ni lazima umtafute mzoefu akusaidie kujua machimbo, mzigo original, soko nk
inahitaji research ya muda mrefu kidogo kabda hujaamua kuifanya.
USIINGIE KICHWA KICHWA HAPA.

6.Kilimo cha green house

My take; kulalamika tu hakuwezi kutukwamua tulipo,
magroup ya watsap, fb na mengineyo tuyatumie pia kwenye ujasiriamali kupeana fursa ktk maeneo tulipo na kuwezeshana bila kinyongo.
Tukifanya hivyo naamini tutafika.

Nawasilisha!!!
 
naomba mchanganuo wa kuanzisha green house tafadhali...
Mchanganuo
Green house ya mita 8 kwa 24
Gharama inafika mill 8 mpaka 9 kutegemea na eneo ulipo.
Material ni vyuma maalum vya kutengeneza frem, Nylon ya kufunika juu(kama paa), nyavu ya kuzungusha kuzunguka gh, nyaya za kubania wavu, nyaya za kufunga ndani kwaajili ya kushika mazao, tank la maji Lt 1000, drips za kutandaza kwenye matuta kwaajili ya umwagiliaji na zege kwaajili ya kusimika nguzo
 
Greenhouse mita 8*24
Mfano zao la nyanya

Inaingia miche 700
Ukiihudumia vizuri mche mmoja unatoa 16_24kg
Mazao ya greenhouse Mara nyingi yanauzika supermarket kwasababu hayapigwi dawa na matunda yanakuwa mwonekano mzuri sana, (bei ya supermarket iko juu kuliko mtaani)

Therefore kama 1kg ni sh 1500
kwa miche 700
Mche mmoja unatoa 16kg. (kima cha chini)
16*700*1500= 16,800,000 kwa miezi sita pekee.
 
Mkuu kwa dsm sina uzoefu ila ngozi nyingi zinauzwa Himo (Moshi) wakenya ndio wanunuzi wakubwa coz wana viwanda vingi vya usindikaji na wananunua kwa bei nzuri zaidi.
Himo sehemu gani hapo mkuu, sokoni pale?
 
Safi sana mkuu Zillion , uzi murua kabisa. Ideas zote hapo ziko poa sana. Ila hiyo ya maji nitaifanyia kazi very soon Mungu akinijaalia, uzuri wake inaruhusu hata kwa mtaji mdogo... naanza na madumu tu kadhaa.

Watu kama wewe ndiyo wanaifanya jf iwe sehemu sahihi ya kupatia maarifa na taarifa mbali mbali zenye manufaa.

Kweli vijana tupambane mapema kujikwamua kiuchumi.
 
1. Kuuza maji
kwa walioko dsm kuanzia kimara,ubungo tabata na maeneo mengine mengi maji ni shida
Unafanyaje?
Kama una mtaji na eneo unaweza kuchima kisima na kuanza kuuza maji, pia kama huna eneo unaweza kuingia mkataba na mmiliki wa eneo utakaloona linafaa ukachimba kisima then mkakubaliana maybe (utachukua mapato kwa miaka mitano au saba na kumwachia kisima) au vinginevyo lkn kimaandishi na kisheria.
Wachimbaji wapo karibu chuo cha maji (ubungo) na maeneo mengine.
Kama huna mtaji wa kuchimba kisima unaweza kununua madum unakodi kirikuu(kinapakia madumu mpaka 50), tafuta migahawa, bar hata 5 tu uwahakikishie kuwapelekea maji kila siku, soko ni la uhakika.

2.Kuuza na kutengeneza vifaa vya simu na simu mf memory card, flash, ear phone, head phone, phone covers nk
Hapa nimelenga zaidi maeneo ya vyuo na hostel wengi wanauza ila hawatengenezi, ukiwa na fundi simu hiv vifaa unauza sana.

3.Kununua na kuuza ngozi za ng'ombe mbuzi nk
Hii nina uzoefu mdogo ila ni biashara yenye pesa sana kwani ngozi inauzwa kwa kilograms 5000@kg kwa bei ya zaman kidogo
So ukipata ngozi yenye 8kg 5000*8=40,000
Ngozi hiyo unaweza kununua machinjioni 5000_10000

4.Kutengeneza chaki
Hii ni fursa ya kuanzisha viwanda vidogo vidogo hasa kwa vijana mlioko maeneo yanayozalisha chokaa kwa wingi mkajiunga na kuchukua mikopo( mill 50 za uncle Magu kwa kila kijiji) na mkaanza kazi.
Soko lake ni la uhakika mnaongea na watu wa halmashauri wanaweza kuwapa tenda kwenye shule za serikali.Pia private schools vyuo nk

5.Kununua na kuuza dhahabu na madini mengine
Najua hapa watu wengi wanaogopa na kudhani biashara hii ni ya akina Mengi pekee
Sio kweli!!
Mfano; Gram 1 ya dhahabu kwasasa inauzwa 70000 (Dodoma)
Ukiwa na laki7 unapata gram 10
Ukiwa na 1.4mil unapata gram20
1gm sokoni(dsm) ni kuanzia 86000_93000
86000_70000=16000@gm
16000*20=320000 per trip.
Ma expats wapo humu watajazia nyama..
Note:Kama ni mgeni ni lazima umtafute mzoefu akusaidie kujua machimbo, mzigo original, soko nk
inahitaji research ya muda mrefu kidogo kabda hujaamua kuifanya.
USIINGIE KICHWA KICHWA HAPA.

6.Kilimo cha green house

My take; kulalamika tu hakuwezi kutukwamua tulipo,
magroup ya watsap, fb na mengineyo tuyatumie pia kwenye ujasiriamali kupeana fursa ktk maeneo tulipo na kuwezeshana bila kinyongo.
Tukifanya hivyo naamini tutafika.

Nawasilisha!!!
Hivi ndivyo vitu vya kuandika.Siyo siasa tuuuuu! Safi Mkuu.
 
Greenhouse mita 8*24
Mfano zao la nyanya

Inaingia miche 700
Ukiihudumia vizuri mche mmoja unatoa 16_24kg
Mazao ya greenhouse Mara nyingi yanauzika supermarket kwasababu hayapigwi dawa na matunda yanakuwa mwonekano mzuri sana, (bei ya supermarket iko juu kuliko mtaani)

Therefore kama 1kg ni sh 1500
kwa miche 700
Mche mmoja unatoa 16kg. (kima cha chini)
16*700*1500= 16,800,000 kwa miezi sita pekee.
mkuu mtaalamu wa hii kitu nampataje?
 
Hiyo namba tatu hiyo ichunguze vizuri biashara ya ngozi inasumbua kwa sasa baada ya kupigwa marufuku ngozi isitoke nje ya inchi
 
Fursa isiyo na ma uzwazwa ni Forex Trading tu...
Ofisi yako ni Computer yako na Simu yako tu....
Hayo ma fursa sijui uanze kutafuta kiwanja, sijui leseni, wateja, mara majambazi wakuvamie.

Nilifungua Biashara ya Samaki Wabichi Tabora, ikafa...
Nimefungua banda la Chips Mwananyamala kwa Kopa, ikafa...
Nimeingia kwenye Matikiti, nimekutana na figisu kibao kwenye masoko ya Buguruni na Tandika.
Upumbavu tu... Forex ndio kila kitu.
 
Back
Top Bottom