Thomali

New Member
Mar 2, 2023
2
7
Vijana wenzangu ifike wakati sasa tuwekane wazi ya kuwa, hatuna tena mtu wa kumtegemea; sio wazazi, sio ndugu, hivyo vijana wenzangu tuamke na tukajipambanie wenyewe.

Maisha ni mafupi sana kusubiri kile tunachokitaka kitufuate tulipo, tena kwa muda muafaka.

Najua wengi tunatafuta ajira pia wengi tunatafuta pesa ili kufikia malengo yetu, lakini itoshe kusema kuwa kila mtu ana riziki yake, sio lazima tufanane kwa kuigana kisa umeona mwenzako kafanya hiki nawewe unataka ufanye kitu hicho hicho. Namaanisha sio ununue bodaboda kisa mwenzako kanunua bodaboda, la hasha.

Tusiishi kikondoo, tujitafute kwa kujitofautisha na wengine kimawazo, kibiashara hata kiutekelezaji. Kuna vitu vingi vya kufanya ili kujikwamua kiuchumi, hivyo tusikariri kila tukiambiwa tujiajiri tunawaza mtaji na fremu.

JITAFUTE mwenyewe kwanza.
 
Back
Top Bottom