Mpigamimba
Senior Member
- Nov 26, 2022
- 198
- 235
Tabia ya unywaji pombe uliokithiri inaleta ndoto za ajabu ajabu. Mbali na ndoto hizo naona kabisa kuna ushetani unaniletea kivuli. Inapotokea umelala umelewa alfajiri unaota ujinga wa kukaa bar na kupoteza waleti, kutembea kifua wazi, ni dalili ya ukichaa.
Pombe inamadhara akilini, wakati unawaza ukatafute hela umelala una hangover ni ishara mbaya hata kama unahela benki.
Nina kazi na pesa napata, nina nyumba 3 siyo vibanda, usafiri Upo, tatizo ulevi. Huu ni shida na sifurahii hii kitu na sina sababu yoyote ya kufanya hivi vitu. Vijana epukeni pombe. Walah siyo useme utakunywa kaisi, hakuna cha kiasi.
Nilianza unywaji kidogo kidogo, nikazidisha, nikapunguza, nikaongeza, naona nazidisha na siwezi kuacha.
Wakati mwingine inanisabishia matukio ya hovyo hovyo njiani, kwenye vyombo ya usafiri, makutanoni, madaladalani najikuta nafyatua, na kuniletea kero.
Katika mahusiano wakati fulani najiona naweza acha danga hili narukia lile. Nakumbwaga na UTI za kutosha, naandikiwa mimadawa ya ajabu ajabu.
Baadhi ya bar nimepigwa stop kwa kuingia na mashine na kutishia watu. Naona kabisa siyo uungwana na utaratibu.
Vijana acheni pombe. Asikuambie mtu, pombe haina afya hata kidogo, hakuna cha marafiki, wala heshima, kwenye pombe ni fedheha.