Vijana 15 wenye nguvu na ushawishi ktk CHADEMA

Kiongozi umeelewa swali??mada haijasema utaje nani mwenye chama. Mbona mnarukiaga hoja kwa jazba bila kuzielewa??? Sio lazma kila hoja humu uijibu wewe, kwenye huu mtandao wapo watu wengi tu wenye majibu fasaha ya hoja zitolewazo. usijipe jukumu la kujibu kila hoja hata kama huna mchango wa maana katika hoja husika. Hamjisikiagi vibaya kuchanwa kila mara???

Mkuu, mbona unajipa kazi Mods!.
Nakushauri tu fungua forum yako uweke masharti yako! Hivi wewe ni nani humu JF mpaka upangie watu vitu vya kuongea? Kama upendi posts zangu zipotezee tu mkuu, JF ni huru sio ya CDM wala CCM au CUF, au ya mzee wako.
Unachotakiwa ni kufuata sheria na kanuni za JF halafu punguza porojo
 
Such a wonderful analysis japo niungane na wadau wengine kuhusu Mnyika John huyu jamaa kweli deserves to be the first in the list aisee he is very smart hata kama hana ushawishi ndani ya Chama ila yuko organised, focused, hana papara etc...... Yeye ni mfano wa kuigwa aiseee..... ningekushangaa sana ungemweka Godbless Lema kwenye hiyo list coz hana sifa yeyote ya kuwepo huko labda uandae list nyingine ya Vijana wenye ushawishi kwenye migomo na maandamano na mambo mengine yafananayo na hayo. Ila wenzie wamfundishe japo najua jamaa agoma kwa ubishi. Ila hii analysis imetulia big up..................
 
VIJANA 15 BORA WENYE NGUVU CHADEMA HAWA HAPA:-


  1. Zitto Kabwe
    • Naibu Katibu Mkuu.
    • Mbunge – Kigoma Kaskz – 2005 – hadi sasa.
    • Mshauri wa Rais wa Ujerumani masuala ya kiuchumi – Sahara.
    • Ana uthubutu. Ana nguvu sana ndani ya Chama.
  2. John Mnyika
    • Mkurugenzi wa Vijana kwa miaka 6.
    • Mkurugenzi wa Mambo ya Nje hadi sasa.
    • Amekaimishwa Ukatibu Mkuu mara nyingi.
    • Mbunge wa Ubungo – 2010 hadi sasa.
    • Yupo focused.
    • Hana ushawishi ndani ya Chama kwa wanachama wa chini sababu hajichanganyi. Anakubalika na vijana.
  3. John Heche.
    • Diwani wa Tarime Mjini – 2008 – 2010.
    • Alibebwa na uchaguzi wa marudio.
    • Ana nguvu kubwa ya ushawishi ndani ya Chama ingawa hana cheo chochote.
    • Aligombea Uenyekiti wa vijana – akaangushwa na Kafulila.
  4. Halima Mdee.
    • Mbunge – 2005 – hadi sasa (Viti maalum & Kawe)
    • Ni mwanamke kijana anayekubalika sana ndani ya Chama.
    • Ana uthubutu mkubwa sana..
  5. Dady Igogo.
    • Afisa wa Chama.
    • M/kiti wa kamati ya wagombea kwenye Timu ya Taifa ya Kampeni.
    • Aligombea Unyekiti wa Bavicha – akaangushwa na Kafulila.
    • Ana uthubutu, yupo focused & mkakati.
    • Ana ushawishi kwa vijana wa Chadema.
  6. Regia Mtema.
    • Ni Mbunge 2010 – (Viti Maalum)
    • Aligombea jimbo la Kilombero.
    • Ni mlemavu anayekubalika na mwenye uthubutu.
    • Ni Afisa wa Chama.
    • Anakubalika na kundi la vijana wa kike.
  1. Ezekiel Wenje
    • Mbunge wa Nyamagana.
    • Ana uthubutu.
    • Yupo focused.
    • Amebebwa na uchaguzi wa Nyamagana – 2010.

  1. Habib Mchange.
    • Amebebwa na siasa za makundi sana.
    • Ana ushawishi sana kwa vijana.
    • Ana mikakati, yuko focused.
    • Aligombea jimbo la Kibaha – 2010 akapata > 40%
    • Ana uthubutu + anakubalika.
    • Ni mwanafunzi wa mwaka wa pili – UDOM.
  1. David Silinde.
    • Mbunge wa Mbozi Magh. 2010 – hadi sasa.
    • Ana uthubutu
  1. John Mrema.
    • Ni Mkurugenzi wa Bunge & Halmashauri.
    • Aligombea ubunge jimbo la Vunjo.
    • Yupo Strategic na focused.
    • Ana uthubutu.
    • Amebebwa sana na siasa za makundi.
Wengine ni:-
  1. Vincent Nyerere.
  2. Owawa Steven
  3. Burton Gwakisa.
  4. Mwakajila Emanuel
  5. Mhonga Said Ruhwanywa.


Je, Unamzungumzia Raisi gani wa Ujerumani ? Nani alikuambia nchi ya Ujerumani inaongozwa na Raisi ? ... tafathali acha kuwaongopea watu wazima !!

 
Zito hastahili kuwa namba 1 katka hiyo list.
Anayestahili namba hiyo ni Mnyika John John kwa sababu:
-Alishinda kwa kishindo kikubwa mno katika jimbo la Ubungo lililokuwa na ushindani mkubwa sana kuliko majimbo yote Tanzania, akichuana na mgombea wa ccm aliyekuwa anabebwa sana na chama chake na vilevile Julius Mtatiro aliyekuwa na ushawishi mkubwa sana wa kisiasa.
-Alikaimu nafasi ya Ukatibu mkuu wa chama katika kipindi cha uchaguzi mkuu akiwa yeye ndiye mtendaji mkuu nafasi ambayo aliimudu barabara.
-Alipigia kampeni wagombea wengine wa chadema katika kipindi hicho hicho.
-Bado aliendelea kushikilia nyadhifa zake nyingine bila kutetereka.
-Yuko focused na Hakurupuki
-Hana papara wala uchu wa madaraka wala uroho wa utajiri wa haraka haraka.

Kwa upande wake, Zito yeye ni kinyume cha hayo hapo juu.
Kwa mawazo yangu Zito alistahili namba 5.

List yangu ni hii hapa:
1. Mnyika
2. John Mrema
3. Halima Mdee
4. Hezekia Wenje
5. Zito
6. Higness Samson

Udini mtupu.

Muulize Mbowe yaliyomkuta mara pale Zitto alipoamua na kuthubutu kugombea Uenyekiti wa taifa Chadema.
 
comrades.
Nimelenga vijana wenye nguvu ndani ya chama!
Highness ni mgeni ndani ya chama. Hajulikani, hana ushawishi. Ana ushawishi ilemela.
Zitto nje inawezekana hana nguvu. Lakini ndani ya muundo wa kiuongozi na vikao vya chama, chadema hawawezi kupuuza nguvu zake! Pengine angeshatimuliwa.
Mnyika ana nguvu nje ya chama, ndani ya chani ya chama hawezi kumpiku zitto.
he! Mbona umeongea kinyumenyume!
 
Je, Unamzungumzia Raisi gani wa Ujerumani ? Nani alikuambia nchi ya Ujerumani inaongozwa na Raisi ? ... tafathali acha kuwaongopea watu wazima !!


Dogo kama huna data usiongee!
Ujerumani inayo Rais wake japo si mtendaji. Mtendaji mkuu ni Chancellor. Ila kaa ukijua Rais yupo.
Google that!
 
Udini mtupu.

Muulize Mbowe yaliyomkuta mara pale Zitto alipoamua na kuthubutu kugombea Uenyekiti wa taifa Chadema.

Unaijua dini yangu...!!!!!???
Umeangalia sababu lakini....!
Au ndo akili yako ipo barubaru kama jina lako!
 
Acha kuanza kugawa majembe ya chama, kama wewe unaona wana nguvu baki nayo moyoni coz kuanza kunamba inakatisha tamaa na wengine. CDM vijana kwa wazee wako fit, 4ur Info, CDM wamejipanga zaidi ya miaka 10 kupata mafanikio waliyo nayo leo so chama kipo focused bana
 
Haki ya Mungu ungejua navyofight kwa ajili ya CDM huku mtaani kwetu na popote nnapokwenda usingeacha kunitaja but all in all 2po pamoja.
 
Je, Unamzungumzia Raisi gani wa Ujerumani ? Nani alikuambia nchi ya Ujerumani inaongozwa na Raisi ? ... tafathali acha kuwaongopea watu wazima !!


Duh kweli wewe siyo mtu mzima, na kwa taarifa yako jamaa amepatia.
Kama ulikuwa hujui leo jua, ujerumani ina raisi na alishawahi kuja tanzania miaka kama 2,3 iliyopita.
Nenda google tafuta ujue mambo. Na kwa kukuongezea Israel nao wana raisi. Acha kuongea mambo ambayo hujui. Unamjua chancellor angela markel tu, yupo raisi pia.
 
Back
Top Bottom