Jinsi tunavyoumia sasa ndivyo ndugu zetu albino walikua wanaumia ikifika uchaguzi
Mpaka leo tumebakiza siku 8 kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika, lakini mpaka leo hii tumepoteza wanasiasa tisa tayari. Wanasiasa tuliowapoteza ni, Mohamed Mtoi (CHADEMA), Estomi Malla (ACT WAZALENDO), Celina Kombani (CCM), Mch. Christopher Mtikila (DC), Abdalah Kigoda (CCM), Emmanuel Makaidi (NLD), Deo Filikunjombe (CCM) na kuna madiwani wawili mmoja wa CCM na mwingine wa ACT, majina yao nimesahau. Munga Baba zilaze roho za marehemu hawa mahali pema peponi.
Kuna watu watasema ni mipango ya Mungu, wengi watasema hivi, lakini mimi sitaki kila kitu tuseme ni mipango ya Mungu. Hivi Mungu ni muuaji??? Mungu wetu ni katili namna hii??? Labda niulize swali, akitokea jambazi akakupiga risasi ukafa papo hapo, tutasema ni mipango ya Mungu??? Inamaana Mungu atakuwa amepanga jambazi akupige risasi?? Halafu mwisho wa siku Mungu huyo huyo aliyepanga ufe kwa kupigwa risasi na jambazi, atamuhukumu huyo jambazi aliyekupiga risasi au jambazi akitubu basi Mungu huyo huyo atamsamehe? Hapana, mimi binafsi sitaki kuamini kuwa vifo vyote ni mipango ya Mungu, hapana.
Ni kweli tunaishi na kuna siku ikifika ni lazima tufe. Hakuna ubishi hapo lazima kifo kitatuchukua, lakini kuna vifo vinasababishwa na sisi binadamu wenyewe. Katika maisha kuna harakati nyingi sana, na moja ya harakati hizo ni za kutafuta utawala na maslahi. Hizi ni harakati hatari sana katika maisha ya binadamu. Wote tunafahamu kuwa Ubunge au Urais au Udiwani kwa sasa hivi hapa Tanzania ni issue kubwa, ni dili hasa. Siwezi kushangaa kama kuna watu watafanya wawezanyo hata ikibidi kutoa roho za wenzao ili mradi tu wapate nafasi hizo. Hatuwezi tukabisha katika hili, wote tumeshuhudia Albino wakiuawa kikatili na wengine kunyofolewa viungo vyao kisa watu tu wanataka utajiri na mafanikio kisiasa. Tunalijua hili, wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu ushirikina, upigaji ramli na utabiri wa wanaojiita manabii huwa unashamiri sana. Viongozi wengi sana ni washirikina na hili halina ubishi hata kama hakuna ushahidi wa wazi wazi.
Sina maana ya kusema kuwa vifo vyote hivyo vya hao wanasiasa vilivyotokea ni matokeo ya kibinadamu, la hasha, lakini kuna mashaka sana. Kuna vifo vimetokea katika mazingira ya kutatanisha sana. Kuna maswali mengi sana ya kujiuliza. Is it fate or coincidence? Is it fate or it is just survival of the fittest?
Tumebakiza siku 8 kufika tarehe 25 October. I have a bad feeling about this election. Siku 8 zilizobakia ni nyingi sana. Kwa jinsi mambo yanavyokwenda sijui, tutegemee kusikia lolote lile.
Mwenyezi Mungu, Baba wa rehema tuepushe na mabalaa na utuokoe kutoka kwa yule muovu.
By Son of Gamba.
ss wale wa matusi na kashfa za ooh cjui fulani mgonjwa endeleeni....
Naona uchaguzi angalau Vifo vya albino hatujasikia 2005 na 2010 ilikua balaa
Vifo Hivi vinasura Tatu..AU none
1. mapenzi ya Mungu
2. Uadui wa kisiasa ..uliozalishwa na kura ZA maoni vyama vyote
3.Kumkufuru Mungu kwa kukashifiana kulikopitiliza kwa mambo ambayo binadamu Hana uwezo nayo
4. Msongo wa mawazo na uchovu Hasa kutokana na ugumu wa ratiba , kukataliwa na WANANCHI na kuleta sononeko , kutumia gharama Kubwa na kuishiwa pesa kabisa pia kunaweza kuleta msongo wa mawazo
Masaburi yupi? Kama ni huyu wa Ubungo...hafai
Nilikuwapo Mkuu na mimi naeneza ujumbe. Watu wapaswa kufahamu.Mkuu Km ulikuwepo ndo mstari wa jana na Leo kwny maombi ya uchaguzi