Assimilation policy ya wanasiasa kuelekea uchaguzi mkuu

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
4,496
8,735
Assimilation policy ni policy ilio sana tumiwa na Wareno na Wafaransa kwenye makoloni yao na wajuvi wa Historia wanasema ilifanikiwa sana.

Sasa Bongo kila uchaguzu ukikaribia ni lazima wanasiasa waanze kuitumia ili kuwahadaa wajinga kwamba they are the same.

Ukiona First lady wa zamani anapanda pikipiki si kingine bali ni assilimilation policy ya kuwafanya wale wajinga jimboni mwake waamini huyu ni mwenzet, huyu ni kama sisi, wakati uhalisia ni hadaa tupu, akitoka hapo anapanda gari la milion 500 ilhali raia wanashindia uji, hata pesa ya panado tu ni tatizo kwao.

Hizi nyakati ni nyakati za asilimilation policy, nyakati za Wanasiasa kwenda kucheza Draft, Bao na kunywa kahawa vijiweni, kuhudhuria misiba hata ya Mbwa yote hayo kuhadaa wajinga wa hii nchi kwmba wako pamoja na ni wenzao.

Ni nyakati zile tinted kwenye vyoo vya gari zao kuondondolewa ili kukoleza assimilation policy.

Wanasiasa kubadili magari na kuanza kutembelea nagari ya kawaida sana ni kawaida nyakati hizi.

Juzi niliona eti kuna mmoja anatishia kujizuru endapo Mradi wa maji hautakamilika, hii ni maigizo ya levo za juu kabisa, na cha kusikitisha raia walimuchukulia serious kabisa.Raia wanashindwa kuelewa mradi haukamiliki kwa sbaabu pesa hakuna na pesa nyingi zinaenda kwenye anasa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom