Kushambuliwa Ole Sendeka kuwafungue macho wanasiasa kuelekea uchaguzi Mkuu; wasiokubalika wanapenda sana elimination

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
905
4,203
Wanasiasa wenye mvuto na ushawishi kwa jamii chukueni tahadhari. Wapo watu wameletwa Duniani kuongozwa ila wanatamani kuongoza.

Kipindi hiki hali ya tamaa uwaka sana mioyoni mwa wanasiasa. Malipo mengi utolewa kwa vijana wavuta bangi na wasio na kazi waende kudhulumu nafsi za wale wanaokubalika.

Mtakumbuka kuna kipindi Ndugai aliwahi kumpiga mgombea mwenzake fimbo adharani; assume zile hasira angekaa nazo ndani angepanga nini kwa mpinzani wake?

Tunapoelekea uchaguzi wanasiasa na familia zenu kuweni makini Dunia imebadilika sana, wakatili wanatamani wakabidhiwe jamii waongoze.
 
Back
Top Bottom