Viendelezo (Extensions) 8 muhimu kwa kila wavuti ya Joomla

Kilongwe

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
423
115
viendelezo-bora-vya-joomla-dudumizi.jpg
Baada ya kukamilisha mafundisho ya Joomla, nimekuwa nikipokea barua pepe nyingi sana toka kwa watu ambao wamekuwa wakiniuliza juu ya template gani bora, kiendelezo gani bora na mengineyo. Ingawa hakuna jibu la moja kwa moja juu ya ubora, ila kuna jibu la moja kwa moja juu ya nini kinashauriwa. Hapa ninamaanisha, siwezi kusema kiendelezo hiki ni ndio bora au sio bora kuliko kingine kwani kuna njia na mambo mengi ya kuzingatia pindi unapochagua viendelezo vya Joomla. Ila ninaweza kusema kinedelezo kipi kinaweza kukusaidia vipi.


Leo hii nitagusia viendelezo vitano ambavyo kwenye kila wavuti kumi za Joomla, angalau tisa zitakuwa na moja ya viendelezo hivi.Kama haujawahi kutumia moja ya viendelezo hivi, basi huu ndio muda wa kuvitambua na kuangalia jinsi gani vinaweka kukusaidia kwenye ujenzi wa watuvi zako.

1. Akeeba Back up

Kama jina lake linavyojieleza, Akeeba au kwa kiswahili Akiba, waswahili walisema, Akiba, haiozi. Akeeba Backup ni moja na kiendelezo cha lazima kwenye kila wavuti iliyotengenezwa kwa kutumia Joomla. Ni kiendelezo kinachokusaidia kubackup website yako. Kwa kutumia Akeeba, unaweza kubackup website nzima (Mafaili pamoja na database) au ukachagua kubackup database pekee.


akeebay.jpg

Akeeba Backup ina matoleo mawili, moja ni la bure na lingine ni la kulipia, kwa ile ya kulipia inakuwezesha kufanya mambo mengi zaidi kama,kufanya automatic backup, hivyo hauna haja ya kuhangaika au kuwaza backup. Binafsi, nimekuwa nikiitumia Akeeba kwenye kila wavuti tunayoitengeneza kwenye kampuni yetu ya Dudumizi.

Na hii imetusaidia kuokoa muda haswaa pale mambo yanapoenda siko.

Akeeba pia, ni njia rahisi sana ya kuhamisha wavuti toka seva moja hadi nyingine kwani, kwa kutumia Akeeba, unaepuka matatizo (errors) nyingi zinazoweka tokea kwa kuhamisha wavuti kwa mkono. Kuipata Akeeba, nenda Hapa.

2. Admin Tools

Nayo pia inatoka kwenye kampuni moja na Akeeba, hii ni kiendelezo (Component) ambacho kinaokoa sana muda na kukupunguzia msongo wa mawazo. Admin Tools inakuwezesha kufanya mambo mengi kama, kukulinda kwa kiasi kikubwa na wavamizi (attack) wachanga kwa kutumia Web Application Firewall,kuboresha SEO ya wavuti yako, kutibu ruhusa (permissions) za mafaili kwenye seva, kuondoa spams, kuboresha database,kukutengenezea .htaccess imara na mengine mnegi mnegi mengi.


Binafsi, tumeweka sheria kuwa, kwenye kila wavuti ya Joomla inayotengenezwa na Dudumizi, Admin Tools ni kitu cha lazima. Hivyo tumia muda wako kuangalia nini inaweza kukusaidia.Kuna matoleo mawili ya Admin Tools, moja ni la bure na lingine ni la kulipia, hivyo kama unataka kufaidi mambo yote na kuwa salama, ninakushauri utumie toleo la kulipia. Unaweza kudownload kwenye wavuti ya Admin Tool

admintool.jpg

3. Joomla Contents Editor (JCE)

Tofauti kubwa kati ya Joomla na Wordpress kiutumiaji ni jinsi gani unaweza kutuma makala kiurahisi, Joomla bado ina matatizo ya kukuwezesha kutuma makala hasa picha, ukiwa na wavuti inayohitaji kuwa na picha nyingi, unaweza kuona kuwa Joomla si mahala pako. Ila, akhsante JCE, kwani wameweza kupunguza huu utata kwa kiasi kikubwa mno. JCE ni editor inayoweza kutumika kwenye wavuti ya Joomla na kukuwezesha kutuma makala na picha kwa haraka zaidi.


JCE nayo ina matoleo mawili, kuna la bure na la kulipia, ukinunua JCE, ndio utaweza kupata vipachiko (plugins) ambavyo vitakuwezesha kutuma picha kwa urahisi zaidi. Hivyo kama wewe unatengeneza wavuti ya habari au inayohitaji picha nyingi, basi JCE ndiyo mkombozi wako. Unaweza kudownload JCE kwa kwenye Hapa


jce.jpg
4. K2

Sababu kubwa iliyonifanya nipende Joomla ni kutokana na urahisi wake kimatumizi, yaani baada ya kumaliza kuitengeneza na ukamkabidhi mteja, hana haja tena ya kujua mambo ya kiufundi kwa sana,ila tatizo kubwa la Joomla ya awali ilikuwa ni utata wa kuhariri muonekano wa makala. Kwa kutumia kiendelezo cha asili cha Joomla (Joomla Contents) , ni mara chache sana utaweza kufikia unachokitaka. Hivyo basi, K2 ndio mkombozi kwenye hili, K2 inakuwezesha kutuma makala kwenye Joomla na kuzionesha kwenye kurasa ya mbele.

Uzuri wa K2 ni kwamba, sio tu kuwa inapatika bure, bali pia tayari kuna makampuni mengi sana yanatengeneza templates ambazo zinafanya kazi kwenye K2, hivyo unaponunua template, unapata na template ya K2 moja kwa moja. Hivyo inaokoa muda ambao ungetumia kuibadirisha Joomla ili ikidhi matakwa yako.


k2-v261.jpg
Kuipata K2, nenda Hapa.

5.Kunena

Jina lake linajieleza, Kunena, ni muda wa kunenanena na sisi tunanena kwa vina, haha. Kunena ni kiendelezo (Component) inayokuwezesha kuwa na Forums kwenye wavuti ya Joomla. Binafsi nimetumia viendelezo vingi vya forums, kwani website yangu ya kwanza kabisa kutengeneza miaka saba iliyopita ilikuwa na Forums, ingawa haikuwa na Joomla.

Hivyo nimetumia programu nyingi za forums, zile za Joomla na zile zisizo za Joomla, ila naweza kusema, Kunena ndio baba yao. Kama unataka forums, basi fikiria Kunena. Uzuri wa Kunena, ni kuwa inakuja na Joomla hivyo unakuwa na leseni ya kuifanyia chochote utakacho bila hiyana. Pia bila kusahau, Kunena ni bure kwa kwenda Hapa.


kunena.jpg

Kwa kutumia Kunena, hakuna tena ukingo wa nini unataka kufanya. Binafsi ninashauri sanasana kunena kwa wanaohitaji kutengeneza Forums. Ingawa kunena yenyewe ni bure, ila kama unataka kuiboresha zaidi kwa kuwa na muonekanao mzuri au kuongeza vitu vingine zaidi, unaweza kufanya wewe mwenyewe au ukanunua viendelezo kama template na vipachiko (plugins) toka kwa makampuni mengine (third party).

6. ACY Mailing.

ACY Mailing ni kiendelezo (Component) cha Joomla ambacho kinakuwezesha wewe kutuma email toka kwenye wavuti yako ya Joomla. Kiendelezo hiki ni muhimu sana kwa wale wanaotaka kufanya matangazo kwa njia ya Email (Email Marketing). Kwenye kampouni yetu ya Dudumizi, tumekuwa tukitumia ACY Mailing kwa muda sasa, na kuonesha ubora wake. Uzuri wa ACY ni urahisi wake wa kuhariri template unayotaka kutumia, pia kwakuwa inakaa ndani ya Joomla, inakuwezesha kuunganisha na viendelezi (extensions) vingine vilivyo ndani ya Joomla.


ACY Mailing inakuja na features nyingi sana, kama kukuwezesha kupata takwimu juu ya email zilizotumwa kama, nani kafungua, nani kaituma tena, email ngapi hazikufika nk, pia inakuwezesha kuwaondoa watu walioandika emal za kufoji, inakuwezesha pia kuongeza watu kwenye mlisho wa habari.


acymailing-dudumizi.jpg

ACY Mailing inawawezesha pia watembeleaji wa wavuti yako kujiunga na mlisho toka kurasa ya mbele (front end), hivyo una uwezo wa kuwaongeza au wao wenyewe kujiunga. Pia, sasa kuna toleo jipya kabisa la sms, unaweza kutumia ACY Mailing kutuma ujumbe kwa watumiaji wako moja kwa moja kwenye simu zao.


Bila kusahau, ACY Mailing inakuwezesha kuangalia ni vitu gani unaweza kuboresha ili kupunguza uwezekano wa email zako unazotuma kwenda kwenye sanduku la taka (spams box).

Kuna matoleo mawili ya ACY Mailing, lile la bure na la kulipia, hili la kulipia pia limegawanyika kwenye makundi kulingana na mahitaji yako. Unaweza kujionea mwenyewe kwa kwenda Hapa.

7. Virtuemart

Hii list nilitaka kuishia kwenye namba tano, ila nikajikuta nitakuwa sijajitendea haki mimi mwenyewe wala Joomla kama ningeishia kwenye namba tano na kuviacha ACY Mailing na Virtuemart. Kimsingi Virtuemart ni kiendelezo cha Joomla kinachokuwezesha kuwa na duka la online (Online Shop) kwa urahisi zaidi.

Virtuemart sio tu inaweza kutumika kama duka, pia inaweza kutumika kama showroom ya kazi au huduma. Ingawa kuwa na Virtuemart inayofanya kazi sawasawa inahitaji umakini wa hali ya juu ila ni moja ya kiendelezo ambacho kinahitaji nyota tano kwenye Joomla. Kama unafikiria kuwa na duka kwa kutumia Joomla, basi fikiria Virtuemart.


Uzuri wa Virtuemart ni kuwa, kama ilivyo kwa K2, tayari kuna makampuni mengimengi ambayo tayari yanatengeneza vipachiko (plugins) na templates za Virtuemart, hivyo kwa kutumia Virtuemart, unaweza kutengeneza wavuto ya kuuza vitu online ya aina yoyote unayotaka. Ukomo wake ni wewe na pesa kazo.


Virtuemart yenyewe ni bure, ila ni dhahiri utahitaji kununua viendelezo vya Virtuemart kama unataka kuwa na kazi inavyovutia. Binafsi nimetengeneza wavuti nyingi mno, zile za Dudumizi na hata zile za mapartner wetu. Hivyo ninaiamini sana Virtuemart. Uzuri pia, unaweza kuziunga Virtuemart na ACY Mailing hivyo ukawa unawatumia wateja wako taarifa za bidhaa mpya kila zinapotoka.


Unaweza kujifunza mengi kuhusu Virtuemart kwa kwenda Hapa.
gemylady.jpg

Gemylady.com, duka la kuuza vidani online lililotengenezwa kwa kutumia Virtuemart

8. Mobile Joomla

Ukweli usiopingika ni kuwa, wengi wa Watanzania wantembelea wavuti kwa kutumia simu za mkononi, hivyo, kama unataka kuwavuta watembeleaji hawa, basi kuwa na wavuti ya simu ni kitu cha lazima. Ingawa kwenye toleo jipya la Joomla wamezingatia sana watumiaji wa simu, ila wao wamezingatia sana wale watumiaji wa simu za kisasa zaidi (smart phone), kwa wale wezangu na mimi wanaotumia simu za tochi, na wale wenye internet za kusuasua, bado wanahitaji tovuti za simu za kawaida.


Mobile Joomla inakuwezesha kufikia malengo haya tena bila gharama yoyote. Mobile Joomla sio tu inakuwezesha kuwa na template ya kwa ajili ya simu, bali pia inakuwezesha kupunguza ukubwa wa picha ili ziendane na simu, pia unaweza kuna na jina la wavuti kwa ajili ya simu, mfano moja ya tovuti tulizotumia ni kama http://m.mjengwablog.com hii ni Joomla toleo la simu. Tembelea ujionee mwenyewe.


Bali, bure ina ukomo, kwa kutumia toleo la bure, kutakuwa na matangazo ya watengenezaji, hivyo kama unataka kuwa na matangazo yako, inabidi ununue toleo la kulipia.


Chanzo: Afroit.com


Je, wewe hutumia kiendelezo gani kwenye wavuti yako ya Joomla, endeleza kwenye mlolongo huu. Wiki zijazo tutakuletea viendelezo vingine.


Na: Mkata Nyoni
Chief Business Development Officer - Dudumizi
Email: mnyoni@dudumizi.com
Dudumizi.com / mkatanyoni.com / AfroIT.com
 
Back
Top Bottom