Hatua za kufuata unapofanya uhakiki wa Picha kwa kutumia Yandex

132559898_gettyimages-1243579431.jpg


Yandex ni njia nyingine ya utafutaji inayotumika sana kufanya uhakiki wa picha.

JamiiCheck imekuandalia utaratibu wa hatua kwa hatua wa jinsi ya kutumia Nyenzo hii kufanya uhakiki wa picha.

1. Fungua Kivinjari Chako
Anza kwa kufungua kivinjari chako kwenye kifaa chako cha mkononi au kompyuta.

2. Tembelea Tovuti ya Yandex
Ingiza 'Yandex' kwenye sanduku la utafutaji la kivinjari chako na bonyeza kwenye matokeo yanayofanana na tovuti rasmi ya Yandex.

3. Pakia Picha
Kuna njia mbili za kupakia picha kwenye tovuti ya Yandex
  • Bofya kwenye alama ya kamera iliyo kwenye sanduku la utaftaji la Yandex na chagua 'Pakia Picha' au 'Upload' kisha upakie picha unayotaka kufanya uhakiki.
  • Ikiwa picha tayari iko kwenye wavuti, unaweza kunakili URL (Link) ya picha hiyo na kuibandika moja kwa moja kwenye sanduku la utaftaji la Yandex.
4. Bofya Kitufe cha Utafutaji
Baada ya kupakia picha husika, bonyeza kitufe cha 'Tafuta' ili Yandex ianze kutafuta picha kama hiyo kwenye wavuti.

5. Angalia Matokeo
Yandex itakuonyesha matokeo ya picha inayofanana kidogo au inayofanana kabisa na picha uliyopakia. Utaweza kuona tovuti zenye picha husika na maelezo zaidi kuhusu picha hiyo.

6. Kagua Chanzo cha Asili
Kagua matokeo kwa makini ili kubaini chanzo cha asili cha picha au taarifa zaidi kuhusu picha hiyo. Yandex itakuonyesha tovuti zenye picha, na unaweza kuchunguza zaidi ili kujua maelezo zaidi kuhusu picha hiyo.

7. Thibitisha na Tathmini
Baada ya kupata matokeo, tathmini taarifa ulizopata ili kubaini ikiwa picha ni ya kweli au la. Kulinganisha maelezo kutoka Yandex na vyanzo vingine itakusaidia kujenga uhakika.

Hitimisho
Baada ya kufuata hatua hizi, utakuwa umepata ufahamu zaidi kuhusu asili au maelezo ya picha hiyo. Kwa hiyo, utaweza kufanya tathmini inayofaa ya picha hiyo na kuamua ikiwa ni sahihi au la.

Kumbuka, Yandex ni chombo kingine muhimu kwa uhakiki wa picha, lakini pia ni muhimu kutumia vyanzo vingine na mbinu za uhakiki wa ziada kuthibitisha habari zaidi.

Pia soma: Hatua za kufuata unapofanya uhakiki wa Picha kwa kutumia Google Image Search
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom