Video; Mwenyekiti Mbowe amtaka rais Kikwete kuacha unafiki katiba mpya

CHADEMA

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
488
2,468
Sehemu ya hotuba ya Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe akifungua kikao cha Kamati Kuu kinachofanyika jijini Dar es Salaam kwa siku 2, Julai 18-19, 2014.

Hotuba ya Mwenyekiti ilijikita katika mchakato wa Katiba Mpya, tulikotoka, tulipo na tunakopaswa kuelekea.

Last edited by a moderator:
CHADEMA CHANUKA TENA!!! VIONGOZI WA CHADEMA MKOA WA KIGOMA WATANGAZA KUTOKA CHADEMA na KUJIUNGA na ACT-TANZANIA::
Katika kile ambacho Wanachadema wengi wamechoshwa na uongozi wa Chama hicho, hatimaye Viongozi wa Chadema Mkoa wa Kigoma Mwenyekiti wa Mkoa Jaffari Kasisiko, Katibu wa Mkoa Msafiri Wamarwa na waandamizi wa Mkoa, Leo wametangaza kuachana na Chadema Chama cha Ukanda,Ukabila,Udini na utawala wa kifalme na kujiunga na Chama cha Wazalendo ACT.Hili ni anguko kubwa la CHADEMA kwani taswira ya Chadema nchini imekuwa ikijengwa na Viongozi hao. Chadema kwa sasa inapumulia mashine na ipo chumba mahututi. Chama cha ACT kimepata mvuto mkubwa na kuwa kimbilio la wapenda demokrasia,UWAZI na Uwajibikaji.
R.I.P CHADEMA.
 
Hahahahaahahahaha,Chagadema choka mbaya niko Temeke hapa ni nouma
 
Mkuu ifweero unaambiwa mwenyekiti kahutubia wewe unasema wanachama wanakimbia! Sikiliza basi hotuba ya mwenyekiti huenda ikawa na kitu.
 
Last edited by a moderator:
Asante mkuu, kamanda amejaa busara, ujasiri na hekima ya hali ya juu. Maccm yanabaka haki ya watanzania

God bless CHADEMA!!
 
Hints za hotuba ya Mwenyekiti wa CHADEMA alipokuwa akifungua kikao cha kawaida cha Kamati Kuu kinachokaa kwa siku 2, kuanzia Julai 18-19, 2014 Mbezi Beach Hotel, ambayo ilijikita kwenye suala la Katiba Mpya.

· Kinachoendelea ndani ya nchi kwenye suala la mchakato wa Katiba Mpya ni dalili ya wazi ya kukosekana kwa political leadership.

· Hali hiyo inajidhihirisha wazi kutokana na makundi mbalimbali ya kijamii ndani ya nchi kuchukua self initiative za kuokoa mchakato mzima huku uongozi wa kiserikali ambao ungepaswa kuwajibika katika jambo hilo nyeti, ukiwa haujui kitu cha kufanya.

· Amesema kuna ombwe kubwa la uongozi wa kisiasa kwenye suala zima la mchakato wa Katiba Mpya kutokana na viongozi wahusika kuwa insensitive na masuala yanayoweza kuiokoa nchi au kuizamisha.

· Amesema kuwa UKAWA wameliona jambo hilo ndiyo maana wamesikia kilio cha makundi mbalimbali katika jamii yanayotaka kuona mchakato wa katiba ukiendelea kwa manufaa ya wananchi na kukubali kushiriki mazungumzo yanayoweza kuokoa mchakato wa katiba mpya kwa manufaa ya wananchi.

· "Hatuna sababu za kukataa mazungumzo…lakini tunazo sababu za kutorudi bungeni. Sisi hatutafuti kushindana kwenye suala hili, kwa sababu wanaopaswa kushinda ni wananchi kwa kupata Katiba Mpya wanayoishiriki, kuimiliki na kuikubali."

· "Mchakato wa Katiba Mpya umedhihirisha wazi ombwe la uongozi wa kisiasa nchini. Upo ushuhuda wa wazi. Tumeona makundi mengine, zikiwemo taasisi za dini, taasis zisizo za kiserikali, wanazuoni, viongozi wastaafu mbalimbali, wanataaluma kadha wa kadha wametoa kauli za kulenga kuokoa mchakato wa Katiba Mpya."

· "Mchakato wa Katiba Mpya ni mchakato wa kisiasa, lazima kuwepo na usimamizi na uongozi wa kisiasa…sasa ni wazi panapotengenezwa au kuachiwa ombwe lazima ombwe hilo lijazwe na vyombo au vitu vingine, kama ilivyotokea sasa kwa makundi mbalimbali yenye nia njemana taifa letu," amesema Mwenyekiti Mbowe.

· Akizungumza kwa niaba ya CHADEMA na UKAWA, Mwenyekiti Mbowe amesema kuwa anashukuru sana makundi yote kwa juhudi zao za kuokoa mchakato wa Katiba Mpya, ikiwemo Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya ambayo alisema kuwa imeendelea kufanya mashauriano mbalimbali kwa ajili ya manufaaya taifa.

· Amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa wito kutoka kwa makundi hayo kuwataka UKAWA warejee bungeni, bado jambo moja la msingi halijazungumzwa kwa kina nalo ni sababu hasa ya kwa nini hali iliyopo imefikia hapo ilipo.

· "Nini kimekwamisha hasa mchakato huu, kwa nini tumefikia hapa tulipo leo? Ni vigumu sana kuweza kukubali tu rai ya kurudi bungeni bila kuzungumza na kujadiliana kwa kina sababu hasa zilizotufanya tutoke, utakuwa sawa na uwendawazimu.

"Ni wazi hatuwezi kukataa mazungumzo lakini tunazo sababu za kukataa kurudi bungeni. Ni vyema ieleweke wazi kuwa wenye mamlaka na mchakato huu hapa ulipokwama ni rais…wala si UKAWA, wala si CHADEMA, wala si Tume ya Warioba, sasa Rais anapoachia ombwe inakuwa tatizo kubwa," amesema Mbowe.

Mwenyekiti Mbowe amesema kuwa kutokana na sauti za makundi hayo, UKAWA walikubali kurudi kwenye mazungumzo kwa kuamini kuwa yanaweza kuwa na manufaa kwa wananchi wanaotaka Katiba Mpya na bora.

Amesema katika masuala ya majadiliano na maridhiano ni suala la kawaida kwa kiongozi au viongozi mwenye maono kukubali mazungumzo, ikiwa ni njia mojawapo ya kuziba ombwe hilo la uongozi wa kisiasa.

"Hapo ndipo tulipofika. Tumefanya mazungumzo ambayo hatimaye kila upande utalazimika kuweka concerns zake…sasa upande wa CCM wamekutana kwenye Kamati Kuu yao kwa siku mbili, lakini kwa taarifa za ndani kabisa za kikao hicho ambazo tunao ushahidi wake, bado CCM hawana nia thabiti na dhati kwenye suala hili.

"Wako kwenye hila za kutaka kufanya ulaghai…wanafikiri wanaweza kulegeza msimamo wa UKAWA kurejea bungeni kisha warudie kufanya yale yale ambayo waliyafanya kabla hatujatoka. Tunawaambia taarifa zao tunazo…wanataka kuharibu mchakato mzima kisha kurejea kwenye hali ya sasa.

"Naomba kusema hivi UKAWA iko tayari kwa mazungumzo kwa ajili ya taifa letu, taifa hili limelilia Katiba Mpya kwa miaka mingi, wananchi wanataka Katiba Mpya na bora, hatuko tayari kurejea kwenda kunajisi maoni ya wananchi, kia patakapotokea hila kama wanazopanga kufanya, hatutasita kuchukua hatua.

"Kama wanapanga mbinu chafu za kututenga nawaambia mbinu zao hazitafanikiwa hata kidogo. Mungu yuko paoja na CHADEMA ndiyo maana hata wanayoyajadili, kama walivyofanya juzi tumeweza kuyajua. Kikao cha Julai 21 alichoita Msajili wa Vyama tutakwenda na tahadhari zote.

"Ningependa kutumia fursa hii kumsihi Rais Kikwete walau ajifunze hata kama ni kwa kujilazimisha…ajifunze kutokuwa mnafiki ili anavyokwenda kumaliza awamu yake ya uongozi aliache taifa likiwa na misingi bora ya amani ambayo ni haki na matumaini kwa wananchi wake,"amesema Mwenyekiti Mbowe.

Mwenyekit Mbowe amemalizia hotuba yake ya ufunguzi kwa kusisitiza kuwa iwapo mchakato huu wa Katiba Mpya, UKAWA hawako tayari kushiriki uchaguzi mkuu ujao kwa sheria za uchaguzi zilivyo hivi leo chini ya usimamizi wa tume isiyokuwa huru kama inavyoonekana sasa.

Kikwete hawezi acha unafiki maana ni jadi yake

-Anasema UKAWA walitoka tu nje bila sababu.......huuu ni unafiki uliopita mipaka yaani hajuwi sababu????

-Anasema mapepo yameingilia mchakato wa katiba (yeye ndiye aliengilia na kuvuruga) ......huuu ni unafiki uliopita mipaka

-Anasema Taifa la tanzania ni tajiri sana lakini hafaham kwanin watanzania bado masikini....unafiki mbona Riziwani sio masikini? katowa wapi utajiri naye katoka shule hivi karibuni?

-Anasema (kikwete) hakushiriki mauwaji ya Daud Mwangosi mbona Kamuhanda kapandishwa cheo nani kaidhinisha kama siyo yeye.... Unafiki

-Anasema (Kikwete) hakushiriki mateso na mabomu yaliyoangamiza CHADEMA na wafuasi wao ARUSHA ...Mbona kamanda Andengenye kapandishwa cheo nani kabariki kama sio yeye.....Unafiki

-Anasema yupo teyari kuwapa watanzania katiba mpya, mbona hawaambii ccm kujadili rasimu ya Joseph Sinde Warioba .. Unafiki

.
.
.
.
.Unafiki wa Kikwete utalingamiza taifa la Tanzania.
 
Hakuna bajeti ya coffee na juice Ikulu. Rais Kikwete hana muda wa kuongea na kikundi cha watu wabinafsi na wenye matakwa ya kuligawa taifa. Rais Kikwete anaongea na wananchi wote wa Tanzania wenye matakwa ya kulijenga taifa.

Kelele hizi zote ukizichuja utagundua wanataka kwenda Ikulu kunywa kahawa na juisi.

Hotuba yenyewe imejaa fallacious argumentation.

Unamuomba Rais akutane na kikundi kinachojiita UKAWA, halafu hapo hapo unasema Rais ni mnafiki. Sasa kama Rais ni mnafiki, unataka akutane na wewe ili iweje?.

Tulisema, mlitoka kwenye bunge la Katiba kwa matakwa yenu, na matakwa hayo hayo yatawafanya mrudi bungeni.

Mtarudi tu bungeni. Hizi hoja za kutunga za kusema "tumenasa mazungumzo" ndani ya Kamati Kuu ya CCM haziwezi kuwahadaa wananchi.

Katiba za vyama vyenu ni majanga na mmechakachua. Mchakato wa Katiba ya nchi lazima itakuwa ni kina kirefu katika fikra zenu.

Taifa linaendelea hata bila uwepo wa kikundi kinachojiita UKAWA.
 
Chadema hamna mamlaka ya kulalamikia katiba mpya ili hali hiyo ya chama chenu mnaikanyaga kanyaga.

Acheni michezo ya kitoto nyinyi wachaga.
 
CHADEMA CHANUKA TENA!!! VIONGOZI WA CHADEMA MKOA WA KIGOMA WATANGAZA KUTOKA CHADEMA na KUJIUNGA na ACT-TANZANIA::
Katika kile ambacho Wanachadema wengi wamechoshwa na uongozi wa Chama hicho, hatimaye Viongozi wa Chadema Mkoa wa Kigoma Mwenyekiti wa Mkoa Jaffari Kasisiko, Katibu wa Mkoa Msafiri Wamarwa na waandamizi wa Mkoa, Leo wametangaza kuachana na Chadema Chama cha Ukanda,Ukabila,Udini na utawala wa kifalme na kujiunga na Chama cha Wazalendo ACT.Hili ni anguko kubwa la CHADEMA kwani taswira ya Chadema nchini imekuwa ikijengwa na Viongozi hao. Chadema kwa sasa inapumulia mashine na ipo chumba mahututi. Chama cha ACT kimepata mvuto mkubwa na kuwa kimbilio la wapenda demokrasia,UWAZI na Uwajibikaji.
R.I.P CHADEMA.

CHADEMA ipo kwenye chaguzi, hao walishatemwa kwenye mchujo, waende wakafie na act huko! Hatuhitaji oil chafu
 
Hakuna mtu atakaye waruhusu kwenda ikulu kunywa chai tena na hakuna budget hiyo!
 
Hakuna bajeti ya coffee na juice Ikulu. Rais Kikwete hana muda wa kuongea na kikundi cha watu wabinafsi na wenye matakwa ya kuligawa taifa. Rais Kikwete anaongea na wananchi wote wa Tanzania wenye matakwa ya kulijenga taifa.

Kelele hizi zote ukizichuja utagundua wanataka kwenda Ikulu kunywa kahawa na juisi.

Hotuba yenyewe imejaa fallacious argumentation.

Unamuomba Rais akutane na kikundi kinachojiita UKAWA, halafu hapo hapo unasema Rais ni mnafiki. Sasa kama Rais ni mnafiki, unataka akutane na wewe ili iweje?.

Tulisema, mlitoka kwenye bunge la Katiba kwa matakwa yenu, na matakwa hayo hayo yatawafanya mrudi bungeni.

Mtarudi tu bungeni. Hizi hoja za kutunga za kusema "tumenasa mazungumzo" ndani ya Kamati Kuu ya CCM haziwezi kuwahadaa wananchi.

1. Kwani base ya mjadala bunge la katiba nini?

2. Reference zao katika mjadala zinaongozwa na nini

3. Jaji Warioba alifanya nini kuhusu katiba ili iweje ndani ya bunge la katiba?

4. Inawezekana kuwa na kikao bila kuwa na ajenda rejea....yaani kila mtu anakurupuka kivyake?

5. Kama sio unafiki nini msimamo wa Kikwete kuhusu taratibu rejea na msingi wa undwaji katiba mpya.... wapi wanapata mamlaka ya rejea ya mjadala wa katiba katika bunge maalum.

6. CCM wanajadili rasim gani na nani ametowa mawazo, nani amekusanya maoni kwa sheria ipi ikiwa ile ya Warioba hawaijadili?

Tafadhali naomba tufanye mdahalo unishawishi niaamini kwa hoja sio vioja kwamba Kikwete sio mnafiki kwa kunijibu swali baada ya swali hapo juu.
 
Ccm hawana dhamira ya dhati ya kulipatia taifa letu katiba mpya! Kwenye bunge maalumu la katiba wamejaza maccm kila kona toka kwa walemavu mpaka kwa wavuvi!
 
CHADEMA ipo kwenye chaguzi, hao walishatemwa kwenye mchujo, waende wakafie na act huko! Hatuhitaji oil chafu
Wewe na wenzako ndio oil chafu.mmefulia...wa mwisho asisahau kufunga mlango
 
Aachen unafki usokuwa na tija hvi hoja unayoandka hapa unawafkiria kizazi kijacho? wanao n wajukuu wako.UKAWA wapo sahih shida mmelishwa UNGA wa ndere ndo maana hamuoni.....Think Globally Not Localy
 
Ccm hawana dhamira ya dhati ya kulipatia taifa letu katiba mpya! Kwenye bunge maalumu la katiba wamejaza maccm kila kona toka kwa walemavu mpaka kwa wavuvi!
Watz wenyewe ndio wanaipenda ccm, utawapatia wapi ambao sio ccm au wachukuliwe watoto wa shule??
 
Sehemu ya hotuba ya Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe akifungua kikao cha Kamati Kuu kinachofanyika jijini Dar es Salaam kwa siku 2, Julai 18-19, 2014.

Kweli Mbowe Kiboko ya Mafisadi wakiongozwa na mnafiki JK raisi mnafiki anayetishwa na watu baki tu analegea haya sasa yanamtokea anayageuka maneno yake mwenyewe mbele ya wanasiasa aina ya Mbowe
 
Back
Top Bottom