Video Clip: Alichokisema Mhe. Joshua Nassari huko Kigoma

Sikiliza/Angalia:..........Kwa hisani ya Hon. Zitto Kabwe

Ndo maana amekutumia wewe...atleast mshipa wake wa aibu bado haujakatika wote. Nimeshangaa na kusikitika sana baada ya kuyasikia maneno ya Nassari as compared na walichoandika Mwananchi....na Zitto kuwatetea kwamba ''hicho kilichoandiwka ndicho kilichosemwa''
 
Sikiliza/Angalia:

Kwa hisani ya Hon. Zitto Kabwe

Maneno yanayotafsiriwa hapo ya Mh Nasari ni: "...kwa stahili hii sitashangaa miaka 5, 10 au 15 ijayo rais wa jamhuri hii akitokea kigoma...."

Nina mitazamo miwili

1. Kwanza namtetea Nasari.. Mbunge huyu alitoa maoni yake tu kwa jinsi alivo ona hali ilivokuwa hapo uwanjani siku hiyo... na kusema ukweli kumtendea haki hakumtaja Zito kuwa hatashangaa kuona miaka 5, 10 au 15 ijayo rais wa jamhuri akitokea kigoma na kuwa ni Zito.... hapo watu wameunganisha tu matukio na opinions za watu na wakati mbali mbali..of which saa nyingine ni sawa

2. Namlaumu pia Nasari - kuwa namwona akiwa jukwaani hasa akiona umati wa watu anakosa uwezo wa kuchuja maneno muafaka yanayostahili wapi na kwa nini aseme hivo... hajui kuwa kila mahali kuna siasa na watu wanatumia kila neno kisiasa na hata kulazimisha tafsiri ya maneno yake. Mfano kusema sitashangaa kuona miaka 5, 10 au 15 ijayo rais wa nchi hii akitokea Kigoma hii ilikuwa ni kosa hata kama alikuwa na nia nzuri. So hata baadae akikanusha bado wenzake hiyo ni point tu ktk siasa

Nasari (na wengine pia), anahitaji kujua anasema nini why, na wapi...ni muhimu sana kujua kuchuja maneno kabla hayaja toka kinywani.. Nasari sasa ni public figure ule utoto wa zamani lazima tu auache

Nilikuwepo pia NMC Arusha ilimcost sana kukanusha what he meant..sasa laziama tu abadilike hana jinsi

Kwa kaka yangu Zito na Chadema... why hili jambo la Urais ndani ya chadema mnaliweka kama vile ni vita fulani kati yenu... Zito ni kiongozi wa juu kabisa ktk chama inamaana hamliongelei ktk vikao vyenu hadi iwe issue kwenye mitandao, bungeni, mikutanoni...hamna 5,yrs, 10 yrs, 15yrs, 20 yrs, etc Strategic Plans ya chama chenu...ambayo hata issue ya who will be a president contestant for cdm haiwezi kuwa issue hivo kama ilivo sasa...

No I trust Zito, Mbowe, Slaa, Lisu, Prof. Safari, Marando, Prof. Balegu, Mnyika...nk hawashidwi to contain it and finish it within your inner meetings..

Na nyie wabunge wa cdm angalieni mnaposhindwa kuonyesha kuwa ni wamoja ni hatari kwenu binafsi na kwa chadema pia. Binafsi nimefurahia tukio la huko Kigoma by Zito but nimekerwa sana na what followed after the occasion ni malumbano yasiyo na tija kwa cdm, wabunge wenyewe, wapenzi wa cdm, na hata wanachi wengine tunaoona mbali
 
Last edited by a moderator:
Sasa kwani nini maana ya "quote"? Ukim quote mtu lazima utumie maneno yake halisi, ni wapi alimtaja Zitto kuwa rais?

Uko sahihi mkuu, hajam-quote, hapo amemtafsiri. Hao mwananchi wakasubiri muda upite ndio wabandi kirusi chao, utabiri kama huo ungeweza kufanywa na John mnyika alipokuwa jukwaani pale Ndago kwamba siku moja singida inaweza kutoa rais, halafu dr. kitila mkumbo isemwe amelengwa!!!! Wale jamaa wa "first class ikonomist" wangeiita "rabishi"
 
Sikiliza/Angalia:

Kwa hisani ya Hon. Zitto Kabwe

Gazeti la Mwananchi liliandika hivi:-

Kauli ya Nassari

‘Leo, ni mara yangu ya kwanza kufika Kigoma, lakini kwa jinsi ninavyoona mpangilio mzuri wa shughuli hii, naamini kabisa kuwa, Zitto Kabwe aliyeandaa hafla hii na kuwakusanya wasanii wa Kigoma kuwa kitu kimoja anafaa kabisa kuwa rais ajaye wa Taifa letu. Na haya ninayasema kwa uhakika bila hata chembe ya mzaha," alisema Nasari.

Mbona maneno haya ya Mwandishi wa Mwananchi sijayasikia kwenye Video Clip hii, kayatoa wapi?
 
Last edited by a moderator:
kwani tatizo ni nini wajameni?
Hata mimi najiuliza, kulikoni? Nani kasema nini nani hakusema nini?
Ikiwa ni hii clip, Nassari hakumtaja Zitto, walioshabikia Zitto ni waliohudhuria.
Ikiwa Zitto katumia maneno ya Nassari kuwa yeye ndie Mwanakigoma anayestahiki uraisi, kachemsha na amuombe radhi Nassari.
Ikiwa gazeti la Mwananchi limesema yasiyosemwa na Nassari, Zitto na wengineo, linajivunjia heshima, liwaombe radhi wahusika.
 
big mouth nassari verry naive, anaropoka kila kitu na kila mahali.. wakati mwingine sio lazima uongee unaweza punga mkono tu ukakaa..sifa mbaya
 
Zitto leta hapa pia na ile ya wakina Mdee, deo tuone maana ulisema utaleta pia kwa Nassary zitto ushahaibika ww na unafiki wako.
 
Ni aibu sana kwa Zitto Kabwe ambaye ni Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni! Umethubutu kusema kuwa, kilichoandikwa na Mwananchi ndicho kilichosemwa na Nassari, ona sasa clip uliyosema itaeleza kila kitu, inavyokuumbua!

Wewe usikurupuke, hebu soma mwananchi, Wabunge wamsafishia Zitto njia ya Urais 2015, wala hakuna mahali alipomtaja Zitto wala Chadema, na ameongelea in a very broad picture

Nina gazeti hilo hapa wala sio link nam-quote NASSARI: "Leo, ni mara yangu ya kwanza kufika Kigoma, lakini kwa jinsi ninavyoona mpangilio mzuri wa shughuli hii, naamini kabisa kuwa, Zitto Kabwe aliyeandaa hafla hii na kuwakusanya wasanii wa Kigoma kuwa kitu kimoja anafaa kabisa kuwa rais ajaye wa Taifa letu. Na haya ninayasema kwa uhakika bila hata chembe ya mzaha," alisema Nasari" .

Ndivyo walivyoandika mkuu labda ili kuondoa sintofahamu nenda kanunue gazeti la Mwananchi la tarehe 23 Julai 2012 Jumatatu....ISSN - 7573 Na. 04411
 
Heshima kwenu wanajamvi,

Uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 CDM walishindwa kusimamisha wagombea katika majimbo mbali mbali hakuna ubishi wapo wabunge na madiwani wa CCM walishinda ubunge na udiwani bila kupingwa. Hali hii ilisababishwa na vyama vya upinzani kutkuwa na mitandao ya kichama iliyoenea Tanzania nzima.

Chama cha CDM kwa hakika kilibaini kasoro hii na kuamua kuanzisha program yake ijulikanyo kama M4C ikiwa na nia ya kuwafikia wapiga kura wengi kabla ya uchaguzi wa mwka 2015. Kabla ya hii program ilikuwepo operesheni Sangara ambayo tunaaweza kusema kwa uhakika ilisaidia kukipatia chama matokeo mazuri katika uchaguzi 2010.

Wapo viongozi wa CDM ambao tumekuwa tukiwasikia wakihangaika huku na kule kuhakikisha M4C inafanikiwa bahati mbaya Zitto bila haya kaamua kuanzisha mtandao wake kama ule wa Kikwete kwaajili ya kuutwa ufalme wa magogoni.

Mheshimiwa Zitto ni aina ya wanasiasa wanaotanguliza maslahi binafsi na kuyakanyaga maslahi ya chama chake.

Tumekuwa tukisikia CDM ikisemwa ni chama cha kanda ya kaskazini, sijamsikia Zitto akikisaidia chama chake dhidi ya hizi propaganda hasa ikizingatiwa yeye anatoka ukanda mwingine.

Tumekuwa tukisikia CDM ni chama cha kikristo Zitto kwa nafasi yake ya Naibu Katibu Mkuu angetakiwa kukisafisha chama chake kwakuwa yeye si mkristo.

Propaganda hizi kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikitumiwa na CCM hasa baada ya kuishiwa hoja dhidi ya CDM. Naanza kuamini propaganda hizi pia zimekuwa zikitumiwa na Zitto au wapenzi wake kwa faida zake binafsi ndiyo maana hajawahi kukisaidia chama dhidi ya mashambuzi haya potofu.

Nilitegemea Zitto angejikita zaidi katika ujenzi wa chama chake na kupigania upatikanaji wa katiba nzuri badala yake anaunda mtandao wa wanasiasa wachovu ambao bila aibu wanatamka bungeni sasa ni zamu ya Kigoma.
 
Muda ukifika umefika,hakuna wa kuzuiya.Na bwana akisema amesema hakuna wakupingana naye,akisema Zitto ndiye ndiye atakaye kuwa raisi na akisema siye basi siye tusubirie 2015
 
Sikiliza/Angalia:

Kwa hisani ya Hon. Zitto Kabwe

Tunavyoangalia video hii tusome na maneno haya hapa chini:

Gazeti la Mwananchi liliandika hivi:-

Kauli ya Nassari
Kwa upande wake Nasari, alisema Mkoa wa Kigoma umejitokeza wazi kuwa na wanasiasa mahiri na wenye vipaji vya hali ya juu katika kupigania maslahi ya wananchi pamoja na kupambana na ufisadi unaodidimiza uchumi wa taifa letu na kuwanufaisha wachache kwa kutumia nafasi zao.

‘Leo, ni mara yangu ya kwanza kufika Kigoma, lakini kwa jinsi ninavyoona mpangilio mzuri wa shughuli hii, naamini kabisa kuwa, Zitto Kabwe aliyeandaa hafla hii na kuwakusanya wasanii wa Kigoma kuwa kitu kimoja anafaa kabisa kuwa rais ajaye wa Taifa letu. Na haya ninayasema kwa uhakika bila hata chembe ya mzaha," alisema Nasari.

Huku akishangiliwa na mamia hayo ya wakazi wa Kigoma, alifafanua kwamba wanasiasa vijana wamejipanga kuwatetea wananchi na hususani kundi la vijana katika kuondoa matatizo mbalimbali yanayowasibu katika maisha kwa kuwajengea mazingira mazuri ya kufanya kazi zao za uzalishaji mali.

Last edited by a moderator:
ngoja nimtafute zitto....uongo aliousema hapa hauna tija yoyote
 
Maneno yanayotafsiriwa hapo ya Mh Nasari ni: "...kwa stahili hii sitashangaa miaka 5, 10 au 15 ijayo rais wa jamhuri hii akitokea kigoma...."

Nina mitazamo miwili

1. Kwanza namtetea Nasari.. Mbunge huyu alitoa maoni yake tu kwa jinsi alivo ona hali ilivokuwa hapo uwanjani siku hiyo... na kusema ukweli kumtendea haki hakumtaja Zito kuwa hatashangaa kuona miaka 5, 10 au 15 ijayo rais wa jamhuri akitokea kigoma na kuwa ni Zito.... hapo watu wameunganisha tu matukio na opinions za watu na wakati mbali mbali..of which saa nyingine ni sawa

2. Namlaumu pia Nasari - kuwa namwona akiwa jukwaani hasa akiona umati wa watu anakosa uwezo wa kuchuja maneno muafaka yanayostahili wapi na kwa nini aseme hivo... hajui kuwa kila mahali kuna siasa na watu wanatumia kila neno kisiasa na hata kulazimisha tafsiri ya maneno yake. Mfano kusema sitashangaa kuona miaka 5, 10 au 15 ijayo rais wa nchi hii akitokea Kigoma hii ilikuwa ni kosa hata kama alikuwa na nia nzuri. So hata baadae akikanusha bado wenzake hiyo ni point tu ktk siasa

Nasari (na wengine pia), anahitaji kujua anasema nini why, na wapi...ni muhimu sana kujua kuchuja maneno kabla hayaja toka kinywani.. Nasari sasa ni public figure ule utoto wa zamani lazima tu auache

Nilikuwepo pia NMC Arusha ilimcost sana kukanusha what he meant..sasa laziama tu abadilike hana jinsi

Kwa kaka yangu Zito na Chadema... why hili jambo la Urais ndani ya chadema mnaliweka kama vile ni vita fulani kati yenu... Zito ni kiongozi wa juu kabisa ktk chama inamaana hamliongelei ktk vikao vyenu hadi iwe issue kwenye mitandao, bungeni, mikutanoni...hamna 5,yrs, 10 yrs, 15yrs, 20 yrs, etc Strategic Plans ya chama chenu...ambayo hata issue ya who will be a president contestant for cdm haiwezi kuwa issue hivo kama ilivo sasa...

No I trust Zito, Mbowe, Slaa, Lisu, Prof. Safari, Marando, Prof. Balegu, Mnyika...nk hawashidwi to contain it and finish it within your inner meetings..

Na nyie wabunge wa cdm angalieni mnaposhindwa kuonyesha kuwa ni wamoja ni hatari kwenu binafsi na kwa chadema pia. Binafsi nimefurahia tukio la huko Kigoma by Zito but nimekerwa sana na what followed after the occasion ni malumbano yasiyo na tija kwa cdm, wabunge wenyewe, wapenzi wa cdm, na hata wanachi wengine tunaoona mbali

Mkuu nimekusoma vizuri sana,maoni kama haya CDM na wahusika nadhani inafaa wayafanyie kazi.

CDM wajitahidi kuimarisha chama na kuona jinsi ya kuongeza namba ya wabunge katika uchaguzi ujao ambao wataisaidia Serikali kama watachaguliwa kuongoza nchi, kupoteza muda kujadili mambo ya urais inatoa nafasi kwa wapinzani wao kujiimarisha.

Kumbukeni anachofanya Katibu mwenezi wa CCM ni kazi kubwa sana kwa kuimarisha chama na kufufua uhai wa chama, sasa CDM wakianza kupoteza muda kujadili urais basi wajue wanatoa nafasi nzuri sana kwa wapinzani wao, after all, kipimo ni watu na sio mtu, kuwa na uwezo kitu kiomoja, ku-deliver kitu kingine na kukubalika kitu kingine!
 
Back
Top Bottom