Video aliyorusha Miss World kuhusu hali ya umaskini Tanzania; Mama Salma na wenza wa viongozi wa Tanzania bado wanaona ni sahihi kulipwa mabilioni?

Pamoja na ubinafsi wa viongozi, kuna hulka huwa tunayo kwamba wanaokuja kutusaidia kuna wanachopata. Hii husemwa hasa pale mtoa msaada akiwa na ngozi nyeupe, japo hata mwezetu akianzosha taasisi ya kusaidia jamii, tunakimbilia kusema ni dili anafukuzia hela za wazungu. Sijui tunataka wenye mahitaji kwenye jamii yetu wasaidiwe na nani. Kuhusu huyu miss world, nimeona twitter mtu kaandika wazungu huwa wa mikakati sana, kwamba msaada aliotupa miaka minne iliyopita anakuja kuutumia kushinda miss world. Kwamba binti mwenye miaka 18 alikuwa na foresight ya kwenda sehemu ngeni kabisa kwake, kijijini ndani ndani, akajenga shule watoto wasome, Ili miaka ya mbeleni pengine vitamsaidia ashinde miss world. Hao watoto wanaosomeshwa elimu waliyopata si kitu, issue ni binti kashinda miss world Kwa kuwatumia.

Wakati huo huo sisi watoto ambao wala hatuhitaji kwenda mbali kuona wanavyoishi hatuna msaada kwao. Tunawafungia vioo wakija kutuoshea vioo vya magari barabarani, wakituomba hela tukiwa kwenye foleni tunasema wanatumiwa, ni mradi wa mtu, zikianzishwa harakati kupambania uboreshwaji wa maisha kwa wote, sio tu hatuungi mkono, tunabeza.
Sasa katika hali ya kawaida, Yeye kujenga shule Tz kama malengo yake ya muda mrefu ya kushinda miss world Sisi kama Tz tunapata hasara gani zaidi ya faida ya kujengewa shule?

Aliyeargue hivyo atakuwa kiongozi mwenye wivu kuwa yeye hajafanya chochote na binti wa miaka 18 amefanya kitu.

Na bado this time akija kuleta msaada mwingine atasindikizwa na msafara wa V8 new model kama kumi hivi za viongozi zilizonunuliwa kwa kodi ya mtanzania……

Shame on us!
 
Mkuu;

Hoja ya yako sio video ya huyo Miss world ila umejiegesha kwenye hiyo habari ili umseme mama Salma Kikwete.

Hii inaonesha ni jinsi gani huna uelewa mzuri wa haki, madaraka, kazi na majukumu ya bunge na mbunge.

Pia huna taarifa sahihi kuhusu taratibu na hatua za kutunga na kupitisha sheria bungeni na kwa kwa ujumla namna bunge linavyojiendesha.

Nakushauri upitie katiba na kanuni za bunge kabla ya kunyoshea watu vidole!

Mheshimiwa Salma kama mbunge alitumia haki yake kupeleka hoja hiyo bungeni, ikapolewa na kuandaliwa kupitia ofisi ya mwanasheria Mkuu wa serikali na kurudishwa bungeni ambapo ilipitishwa na wabunge wengi bungeni.

Kosa lake liko wapi?? Tupunguze chuki!
You're stupid
 
Mficha uchi hazai Tanzania bado ni masikini huo ndio ukweli miaka 20 iliyopita kulikuwa na issue ya mapanki.

Mpaka yule mwandishi akaletewa mizengwe ila ukweli tulikiwa tunakula mapanki

Hawa wanafanya hivi kutusaidia huu ndio uhalisia wa maisha yetu !!!!

Mpaka uwa najiuliza miaka 60 ya Uhuru Nyerere, mwinyi, Mkapa, kikwete, Magufuli na Samia walishindwa nini kusolve tatizo la msingi ambalo ni umasikini.!! ?
Uongozi ni ajira na sio wito, Nyerere alikurupuka kudai uhuru bila kujiandaa.
 
Mkuu;

Hoja ya yako sio video ya huyo Miss world ila umejiegesha kwenye hiyo habari ili umseme mama Salma Kikwete.

Hii inaonesha ni jinsi gani huna uelewa mzuri wa haki, madaraka, kazi na majukumu ya bunge na mbunge.

Pia huna taarifa sahihi kuhusu taratibu na hatua za kutunga na kupitisha sheria bungeni na kwa kwa ujumla namna bunge linavyojiendesha.

Nakushauri upitie katiba na kanuni za bunge kabla ya kunyoshea watu vidole!

Mheshimiwa Salma kama mbunge alitumia haki yake kupeleka hoja hiyo bungeni, ikapolewa na kuandaliwa kupitia ofisi ya mwanasheria Mkuu wa serikali na kurudishwa bungeni ambapo ilipitishwa na wabunge wengi bungeni.

Kosa lake liko wapi?? Tupunguze chuki!

😁

Itachukua muda sana Mtanzania kuendelea...

Yaani bado hujaelewa mfano wa jamaa...

Kama mume/mke alikuwa Rais, Makamu wa Rais, Waziri mkuu na analipwa mafao kwa maisha yake yote, iweje wenza wao wachukuliw3 kama wastaafu wa kitaifa?

Hayo mafao wa waume au wake zao hayawatoshi?
 
Mkuu hata mimi sikubaliani ni hili ila wa kuulizwa ni ofisi ya mwanasheria mkuu, wabunge wote na spika.

Waulizwe, Ilikuwaje wakapitisha sheria ya namna hii. Sisi wadau wa JF tukiulizana humu hata tukakesha hatutapata majibu na wala hatutabadili chochote!

Wabunge ni wawakilishi wa wananchi, je sisi wananchi, walipa kodi na tozo nchi hii, tuliwatuma kupitisha hoja hiyo??

Je wabunge wetu hawa walitushirikisha ili tukubaliane na tujipange namna ya kuwahudumia hao wastaafu wenza kupitia kodi zetu???

Na je katiba inasemaje kuhusu wananchi kuwaadhibu wabunge wanapopitisha hoja ambayo sisi wanachi hatujawatuma wala kushirikishwa?

Bunge ni mahali pa wabunge kupeleka hoja za kutoka kwa wananchi sio za kwao. Shida ni bunge la chama kimoja kupitisha kila jambo bila kushirikisha wananchi au kufanya tafakuri ya kina.

Hii ndio hasara ya uchafuzi uliopita wa Mwendazake! Na bado kuna sheria kibao zenye madhara makubwa kwa wananchi , omba tu yasikukute!

Rais Samia naye mpaka sasa haja batilisha na anaonekana hana nia ya kubatilisha sheria yoyote mbovu iliyopo awali. Badala yake ameweka mazingira laini kwa kutumia mamlaka ya Rais. Akitoka tu imekula kwetu mazima!

Akitokea punguani mwingine akasimamia hizo sheria mbovu japo halali ndio wananchi watajua hawajui!! Na mzunguko wa jenga bomoa, ponya umiza, nenda mbele rudi nyuma utaendelea daima!

Mzunguko mzuri ni wa aina ya spring japo unazunguka lakini unapiga hatua na hata ikatokea umedondoka utanesa.

ila huu mzunguko tuliomo sisi ni duara kavu, kila tukifanya jitihada tunarudi pale pale! Maneno kibao, hatua sifuri!
 
😁

Itachukua muda sana Mtanzania kuendelea...

Yaani bado hujaelewa mfano wa jamaa...

Kama mume/mke alikuwa Rais, Makamu wa Rais, Waziri mkuu na analipwa mafao kwa maisha yake yote, iweje wenza wao wachukuliw3 kama wastaafu wa kitaifa?

Hayo mafao wa waume au wake zao hayawatoshi?
🙏
 
Miss world ni binti mdogo aliyezaliwa masafa ya mbali na Tanzania. Alipofika Tanzania miaka minne iliyopita alitembelea Arusha na kukuta familia zisizo na uwezo wa mlo wa siku wala malazi. Watoto wengi zaidi ya asilimia 20 walibainika kutokwenda shule. Wawapo shuleni wanakosa chakula huku wakitumia muda wa zaidi ya masaa manne kwenda na manne kurejea majumbani kwao.

Binti huyu alishiriki kujenga shule na akajitolea kufundisha. Alijitolea chakula na malazi ikiwemo kuwanunua wanafunzi mavazi. Stori hii imerushwa live na inasambaa mitandaoni. Wanaojadili wanaona kama fedhea kwa watawala wetu huku watawala wakijinadi kwamba inatangaza utalii na kuitangaza nchi yetu.

Kwa maana nyingine watawala tatizo la watoto kukosa shule siyo big deal bali kwao wao wanaona kama video hii inatangaza utalii. Nimesoma comment ya waziri mmoja akisifia video ile akidai imesaidia wengi kuifahamu Tanzania.

Mimi nikawa na Mtizamo tofauti; nilipoona video hii nimejiuuliza Mama Salma Kikwete anakosa nini hadi achukue fedha za wananchi maskini ziwe zake na familia yake kupitia sheria mpya aliyopenyeza bungeni ya mafao ya wenza wa viongozi?

Hao wenza wa viongozi wana umaskini gani hadi wajione wao wanafaa kulipwa mabilioni ya kodi za umma for years huku wananchi wakikosa mlo mmoja?

Huyu binti Miss Worl hana pensheni lakini ana moyo wa Mungu na upendo. Huyu binti siyo Mtanzania ila ameonyesha kujali na kuthamini uhai wa watoto wetu. Huyu binti siyo mweusi bali ametambua kila binadamu anahitaji haki ya elimu na kuishi.

Natambua wenza walio wengi ni wanawake kuliko wanaume. Natambua waliopigania kulipwa mabilioni haya ni wanawake na siyo wanaume. Natambua wanawake wote waliopigania hii hoja wamezaliwa familia bora. Natambua wanawake hawa hawajawahi kuwaza wala kufikia kusaidia yeyote kwa fedha zao kama alivyofanya huyu binti. Wengi wao utumia fedha za umma kuzifanya mali yao na kutumia miradi ya umma kama fadhila kwa jamii.

Wanawake weusi jitafakarini, waume zenu walipopata madaraka walijilimbikiza mali za umma. Mwenyenzi Mungu akakasirika na sasa wakimaliza muda wa huduma wanachokiona mbele yao ni magonjwa na hivyo vile walivyochuma kwa dhulma vimeoza na kuishia kuwatibu kuliko kuvisaza.

Naona wanawake nao wameamua kujilimbikizia mali za maskini kwa msingi wa sheria. Wanawake viongozi wa Tanzania wamewakwa tamaa na nafsi zao zinawaza kuishi kwa anasa pale wenzao wao wanapoostaafu.

Amini Amin nawaambia......kwa kuwa pensheni hii italipwa mkiwa hai na ili msilipwe pensheni hii kwa muda mrefu na kunyonya maskini , Mwenyenzi Mungu anakwenda kuwapa maisha mafupi sana. Kisheria mtalipwa ila kiroho mtalipwa kwa muda mfupi sana.

Haiwezekani binti wa miaka 24 aje kwenye nchi yenye kila kitu akasaidie kulisha watoto wetu huku ninyi mkijilimbikizia mabilioni msiyoyafanyia kazi

Hongera miss world kwakuwainua wanetu.
SISI TUKO BIZE KUINGIZA SIASA KWENYE KILA UPANDE, HATA VIONGOZI WANAOTUMWA WAKAPELEKE MAENDELEO, AKILI YAO YOTE INAWAZA KULINDA INTERESTS ZA CHAMA TAWALA.
 
  • Thanks
Reactions: Auz

Kama serikali kwa ujumla, ina matumizi ya hovyo tena ya anasa, ilhali wanakwenda kukopa ili kujiendesha, hao wenza hawajali kama serikali na chama chao wasivyojali.
 
Mkuu;

Hoja ya yako sio video ya huyo Miss world ila umejiegesha kwenye hiyo habari ili umseme mama Salma Kikwete.

Hii inaonesha ni jinsi gani huna uelewa mzuri wa haki, madaraka, kazi na majukumu ya bunge na mbunge.

Pia huna taarifa sahihi kuhusu taratibu na hatua za kutunga na kupitisha sheria bungeni na kwa kwa ujumla namna bunge linavyojiendesha.

Nakushauri upitie katiba na kanuni za bunge kabla ya kunyoshea watu vidole!

Mheshimiwa Salma kama mbunge alitumia haki yake kupeleka hoja hiyo bungeni, ikapolewa na kuandaliwa kupitia ofisi ya mwanasheria Mkuu wa serikali na kurudishwa bungeni ambapo ilipitishwa na wabunge wengi bungeni.

Kosa lake liko wapi?? Tupunguze chuki!
ujinga, ubinafsi na tamaa zilizopitiliza zinaanzia hapo kwenye kutumia haki yake vibaya, hyo hoja kuipeleka Bungeni kwake ni kosa kubwa kwenye jamii yenye utambuzi na kujielewa na sababu tosha ya kufanya mamlaka na Taasisi zenye mlengo wa kuendeleza ustawi wa jamii kumulika taa kwa mhusika, ikiwezekana na jamii inayomzunguka kama familia, maana Mtu kama mwanamke kuja na wazo hilo upo uwezekano mkubwa kwamba amejadili na familia yake hususan mmewe. Inasikitisha sana kuwa na jamii yenye watu wenye tamaa iliyopitiliza mkapa shetani mwenyewe analalamika.
 
Mkuu;

Hoja ya yako sio video ya huyo Miss world ila umejiegesha kwenye hiyo habari ili umseme mama Salma Kikwete.

Hii inaonesha ni jinsi gani huna uelewa mzuri wa haki, madaraka, kazi na majukumu ya bunge na mbunge.

Pia huna taarifa sahihi kuhusu taratibu na hatua za kutunga na kupitisha sheria bungeni na kwa kwa ujumla namna bunge linavyojiendesha.

Nakushauri upitie katiba na kanuni za bunge kabla ya kunyoshea watu vidole!

Mheshimiwa Salma kama mbunge alitumia haki yake kupeleka hoja hiyo bungeni, ikapolewa na kuandaliwa kupitia ofisi ya mwanasheria Mkuu wa serikali na kurudishwa bungeni ambapo ilipitishwa na wabunge wengi bungeni.

Kosa lake liko wapi?? Tupunguze chuki!
Wewe ni mjinga kabisa
 
Back
Top Bottom