Vicky Kamata aokoka

AMEN ni habari nzuri basi anachotakiwa ni kutulia ndani ya Yesu kwani faida zake hazielezeki.
 
Zilikuwa ni habari za uvuguvugu nilizokuwa nazisikia bila kuamini, ila jana alithibitisha mwenyewe pale alipouulizwa na mtangazaji Rita wa Praise power pale Diamond Jubilee kama ni kweli ameokoka au lah!! Vick alijibu hivi " Yes!! nampenda Yesu"

kuthibitisha hayo aliimba kibao chake kinachooitwa yakale yamepita katika mashairi ya wimbo wake kuna maneno yanayosema hivi" kama mfalme ameshanisamehe ww ninani unayeendelea kunisumanga? unayeendelea kunisema vibaya?? yakale yamepita!!!

Ni wimbo mzuri na wenye kuvutia!!

Tumuombee Mungu, asonge mbele, ampigishe hatua zaidi, na awe mfano kwa wengine!!

Kila anaempenda Yesu ameokoka? Jibu lake halikujibu swali husika. BTW, kanisani na misikitini si kimbilio la kila mtu, japo sehemu hizo tukufu zimekuwa majalala ya waovu kukimbilia. BTW, hata mwizi akielekea kuiba ataomba Mungu amsaidie.....
 
Hongera sana dada Vicky kwa kumpokea YEsu

2+women.png
 
Majaribu yote haya kuna kuokoka? Labda useme kuna kuamua kujitahidi kuyashinda majaribu. So, HAKUNA KUOKOKA!!!
 
Kuokoka sio mchezo mkuu huyo anatafuta umaarufu mbele za watu hebu kumbuka msanii mmoja anaitwa Mr magali alijifanya mlokole kumbe alikuwa mlevi na anachukua mademu kama kawa na kuna siku live akatoka kwenye magazeti ya udaku, tangu ilipotokea ile skendo sikuwahi kumsikia yule jamaa akisema bwana Yesu tena

wewe unamsemea Vicky kama nani? huonagi jema la wenzio wewe nakuambia hili kwa mara ya pili!!! umaarufu gani anautaka tena?
live your life!!!
 
Amen Amen Vicky. Yesu alikuja kuvitafuta vilivyopotea! Makosa na dhambi zetu zinatakaswa na kuwa nyupe kama theluji! Yesu alikuja kwa ajili ya wenye dhambi! Kama umeokoka na uokoke kiukweli. Neno la Mungu limesema ni heri kuwa baridi au moto kuliko kuwa vuguvugu. Fahamu kuwa maisha ya kilokole ni kazi kubwa na inabidi ufanye kazi kubwa kuulinda wokovu wako. Kwenye ulokole si usanii, ni kweli kweli. Tafadahali usitumie njia ya ulokole kuimarisha usanii wa kidunia kama wafanyavyo baadhi ya watu wanaojiita waokole kumbe ni kuvaa ngozi ya kondoo wakati mwili ni wa Simba. Again, hongera na usiangalie nyuma kuwa eti watu au jamii itasemaje! Ukakitulia na Bwana Yesu utampata hata mume bora kama utahitaji kufanya hivyo maana neno la Mungu linasema, njooni tusemezane, hoja zenu na zijulikane mbele za Bwana.
 
Ulimuuliza kwa nini ameamua kuokoka, au anampenda Yesu tu, wengi huwa wana sababu maalum au Mahsusi, kama anajutia alofanya zamani, Mungu amsamehe.
 
kafulia huyo,,,,,,, kaona hana jipya zaidi ya mwanamke na maendeleo,,,,
 
kumpenda yesu si kuokoka, ni kushika dini kikawaida bila kuyumbishwa yumbishwa
 
Zilikuwa ni habari za uvuguvugu nilizokuwa nazisikia bila kuamini, ila jana alithibitisha mwenyewe pale alipouulizwa na mtangazaji Rita wa Praise power pale Diamond Jubilee kama ni kweli ameokoka au lah!! Vick alijibu hivi " Yes!! nampenda Yesu"

kuthibitisha hayo aliimba kibao chake kinachooitwa yakale yamepita katika mashairi ya wimbo wake kuna maneno yanayosema hivi" kama mfalme ameshanisamehe ww ninani unayeendelea kunisumanga? unayeendelea kunisema vibaya?? yakale yamepita!!!

Ni wimbo mzuri na wenye kuvutia!!

Tumuombee Mungu, asonge mbele, ampigishe hatua zaidi, na awe mfano kwa wengine!!

amen, nadhani atatoa vitu vikali huko
 
kipimo cha wokovu si kuimba tu nyimbo za Injili bali U-TURN katika mwenendo mzima wa Maisha. Ila tumwombe Mungu ili tumwone akipiga hatua kwa kile anachokiri ili isiwe ni gia ya kuingia soko la nyimbo za injili ambalo ni ngumu kusonga mbele kama hujaingia katika maombi sawa sawa na Yesu aamue kukutumia.
 
Back
Top Bottom