Vibarua kiwanda cha Bakhresa Buguruni

SAS unataka mtu Eti kupkia na kupanga unga kwnye lorry ulipwe laki nane Kweli yaani uje asbuhi ushike nyuzi na kupanga unga ndio ulipwe milion kweli 😃😎 ujira Ni mzuri Ila angalau kima Cha chini kifike 350 at least
Hatuzungumzii alipwe laki 8 au mlio ,walipwe kama serikali ilivyoelekeza ,utamlipaje mtu Tsh 3000 per day? Kama ni rahisi aajiri wanae kina yusuph waje kubeba magunia wapakize kwenye scania.
 
hapo hatari yaani ukiingia tu mle ndani ni kama uwanja wa vita kwanza kuna giza halafu kitu kinachotoa mwanga ni moto mmoja mkali wa rangi ya blue joto sasa nimefika pale nimezunguka kama week unawahi unaambiwa leo kumejaa dah ila ukipata unapiga mzigo kuna kitengo kuanzia 10k mpaka 30k kwa siku ila shughuli yake ukitoka kama umechovywa kwenye masizi
Moto wa bluu m@#m&£e 😆 dah
 
Hii thread nimeisoma comment zote, hela inatafutwa kwa nguvu na jasho afu ujira mdogo na hakuna usalama wa kazi. Nimewaza nani atakuja kuwasemea watanzania wenzetu wanaoonewa huko viwandani. Ni Serikali Haijui??? So sad aisee.
Cyo pwa.na unakuta unategemewa.
 
Hata wafanyakazi wa kampuni za usafi zaidi ya kuuza sura ulipwa Kati ya laki na 20 hadi 50 tena baada ya siku 40 hadi 50 na awapewi yote ukopwa nusu nyingine uambiwa mwezi ujao. Kazi masaa 10 kwa siku, SAwa na elf 4 kwa siku.
Walinzi hizi kampuni za wastaafu wa jeshi Hakuna anaelipwa zaidi ya laki unusu kwa mwezi nao urushwa mwezi Ili wasiache kazi. Palikuwa na jamaa anakaa airport dar lindo lipo mikocheni anakanyaga kwa mguu kwenda na kurudi job, mshahara laki moja baada ya siku 40.Ukimchek kaulamba mkanda nje kisa tu akae mjini. Wakati kijijini angefanya makubwa kupitia kufyatua tofali za kuchoma.
Kuna jamaa angu mmoja hapa kaajiriwa kishirika flani kidogo pale mikocheni. Huwa ananivimbia Sana kwamba wanaoajiriwa Wana akili nyingi sabab yeye fom four na mm degree ishakula msamba mtaani. Huyu jamaa sijui analipwa kias gani ila Ile taasisi degree zote zinalipwa laki 3 tu. Na yeye fom four. Kila tarehe 20-30 hunipigiaga simu kuomba nisaidie hela ya kula au vocha. Dah! Motherfuc*** cheap labour 😡
 
Asikuambie mtu Kuna cha wachina cha moshi cement Hawa jamaa ni hatari unaweza piga kazi kwa matusi kweli lakini ikifika kudai haki Yako kwa mwezi lazima uende bunduki japokua ujira mdogo
 
Nakushauri kama una laki 3 nenda tandika kuna kampuni inaitwa WATU LTD wanatoa pikipiki kwa njia ya mkopo ila kianzio lazima uwe na laki 3.
Marejesho kwa siku unapeleka elfu 7500 ila wao wanataka marejesho kwa wiki ambayo ni 50500,mkataba ni kwa muda wa miezi 15 ambayo ni sawa na mil 3,300,000 .
Vigezo uwe na barua kutoka serikali yako ya mtaa,uwe na tin number,uwe na mdhamini mmoja mwenye leseni ya udereva au kitambulisho cha nida tu ukikamilisha kila kitu pikipiki unapata siku hiyo hiyo.
Ukipata pikipiki tafuta smartphone ya bei rahisi jiunge na huduma ya bolt,Uber na in drive bro pesa utakayopiga hutoamini .
Kuna vijana ni degree holder niliwashauri hivyo leo hii hawana muda na ajira pesa wanayoingiza mwalimu akasome

Hivi wewe yale maelekezo niliyokupa na kumpanga Mtu akupe ajira ya sh 220,000 kwa mwezi cash,

Ukasema utaenda, mpaka leo hujaenda maana yake ni nini? Nyie ndo mnafanha watu wasisaidie watu.

Sasa ulikuja huku kulalamika nini? Nime ku pm, nimekupa maelekezo, mpaka leo namuuliza HR wa ile office hujafika, maana yake nini?
 
Hivi wewe yale maelekezo niliyokupa na kumpanga Mtu akupe ajira ya sh 220,000 kwa mwezi cash,

Ukasema utaenda, mpaka leo hujaenda maana yake ni nini? Nyie ndo mnafanha watu wasisaidie watu.

Sasa ulikuja huku kulalamika nini? Nime ku pm, nimekupa maelekezo, mpaka leo namuuliza HR wa ile office hujafika, maana yake nini?
Mkuu saidia na hawa 🙏🙏🙏 FAIZHAD
 
SITOSAHAU SIKU NILIPOTAKA KUFA PALE KIWANDANI

Ilikua mapema mwaka jana nilipitia kipindi kigumu sana baada ya kuyumba kiuchumi na degree yangu mkononi ikanilazimu kujizima data na kutafuta kazi yoyote iwe rasmi au isiwe rasmi.Nikazama zangu jf ndipo nikapata muongozo wa kwenda kiwanda cha unga kwa kurubuniwa kwamba kwa siku malipo inafika hadi buku 8 nikajipa. moyo..

Basi nikafata tafatibu zote siku ya pili nikaenda na barua ya mtendaji then nikaambiwa siku ya pili usiku nikaanze kazi.Basi bwana nikazama zangu pale mida ya saa 1 jioni nikawakuta wenzangu wapo tayari wanasubiri kuanza kazi.Wakagawa msosi pale ndani kila mtu sahani ya wali(upo kama makande) na maharage na ndizi mbivu.Kwa kua ni siku ya kwanza nikawa na uoga uoga wa kula ule msosi na niliogopa kuja kukatwa kwenye malipo.Jamaa wakawa wananishangaa huyu msela vipi huu msosi ni lazima kuchukua haijalishi unataka au hutaki.Basi kuna jamaa akasema chukua nipe mm nitakula,wakawa wanagombania nipe mim nipe mimi.Basi nikachukua ule msosi nikampa jamaa mmoja akala na wa kwake.

Kimbembe kilianza baada ya masaa mawili viroba vilipoanza kushika toka kwenye vinu vinashuka kama mvua na vinu vipo vya kutosha mule ndani.Ili kusubiria viwe vingi ndio kazi ianze wale jamaa wakasema tuchezeni boli humu ndani(mpira wa makaratasi).Basi tukagawana huku na huku tukaanza kucheza mpira.Katika harakati za kuucheza ule mpira nikajibamiza vibaya sana kwenye kinu kipo kama upinde afu kule mbele kama wembe kwa makali yake.Ghafla bin vuu nikajikuta nipo chini nimezungukwa na watu kibao damu zinavuja kama kuku katoka kuchinjwa..Aisee nilijua leo ndio siku yangu siwezi kutoboa maana nilipasuka katikati ya kichwa.Wakaniinua pale sina hata nguvu wakasema nikapumzike pale kazi inataka kuanza.Nilishindwa coz damu zilikua zinavuja sana kuna jamaa akanielekezaa bafu akasema nikaoge ili niwe sawa.

Nilijivuta nikaenda kuoga kule bafuni maji yote yalijaa damu tu yani ili siku ilikua ndio bye bye sema Mungu hakupanga tu.Nikarudi kule ndani jamaa ndio wanagawana watu kwa makundi waanze kazi.Cha ajabu na mimi nikaitwa nikapangiwa kundi nibebe viroba.Nikawaeleza siko sawa damu zinavuja sana lakini hakuna aliyeelewa.Wakasema humu ndani ni lazima kila mtu afanye kazi.Kazi ikaanza nikaambiwa na mm nibebe kichwani zile kilo 25 kwa 50 yena viwili trip moja.Ilikua ngumu sana kubeba lakini sikua na jinsi nikajaribu tripu moja nakashindwa kichwa kilikua kinauma sana.Wakanibadilisha section wakasema niwe nawapakia watu kichwani wenyewe wanaita kijiko,yani unabeba viroba viwili pale chini na kumpa mtu kichwani.Nimefanya mara moja tu kuna jamaa akanigusa pale kichwani na kiroba basi damu zikaanza upya kutoka nikaamua kuacha nikasema liwalo na liwe cha kufia nini.

Basi nikatoka pale nikaenda nje kukaa toka ile saa 4 mpaka saa 12 asubuhi jamaa wanabeba tu vile viroba.Walikua kama 30 hivi lakini viroba walivyobeba ni zaidi ya 6,000 yani kila mmoja kama mia 2 hivi.Asubuhi ya saa 1 tukaitwa wote kwenye mgao wa pesa.Kaja kiongozi wao akasema leo kazi hamna hivyo kila mtu atapata elfu 2,aisee nilichoka mwili na akili yani kazi yote ile mtu alipwe elfu 2.Kuna watu walikua wanapinga mm kupewa ile elfu 2 kisa sijafanya kazi.Sema jamaa akanipa ile buku 2 akasema ukatibiwe.Nimetoka pale naona kama ndoto nikarudi zangu geto ile pesa nikafanya nauli sikubakiwa hata na senti..

Nimefika home kichwa chote kimeloa damu na nimepasuka vibaya sana.Sikua na pesa hivyo nikachukua chumvi na beseni nikaanza kujisafisha huku nikipata maumivu makali sana.Sikwenda kabisa hospitali hadi leo hii na nilipona kwa uwezo wa Mungu baada ya mwezi kupita.Nashukuru hivi sasa nipo sehemu nzuri japo sio sana ila sio kama mwanzo.Leo nilipita ile njia ya kiwandani nikakumbuka kuleta kisa hiki.
View attachment 2484012
We umeenda kiwandani kufanya kazi hilo la kucheza mpira mlilitoa wapi?
 
Kazi za viwandani hasa Tanzania ni hatari sana kwa afya na uhai wako ,do it for your own risk , safety zero ,vitendea kazi hamna ,mazingira mabovu na hatarishi kwa afya na uhai , ujira mdogo sana na usiofaa kabisa + manyanyaso na overwork .
Compliance ya OSHA (Occupation safety and health ) ni always zero ,hivyo ndio viwanda uchwara vya bongo.
Kuna mdau kaongelea kiwanda cha NONDO Nyakato steel-Mwanza , kile ni mfano mmoja wapo , mwaka jana hapo Nyakato steel bomu lilipuka humo ndani ,yote hiyo ni uzembe wa compliance ya masuala ya safety ,wao wanafanya biashara ya kuteyusha chuma chakavu yet hamna mifumo thabiti ya kuchunguza na kusort vyuma vinavyoletwa ili kuyeyushwa ,matokeo yake wanaokoteza kila aina ya chuma na kuvipeleka kwenye vinu /furnaces kuyeyushwa ,upuuz mtupu .
Hivi viwanda vingi bongo vinaoperate kama criminal cartels za mamafia ,Kwanza wengi wanaoendesha hivyo viwanda ni matapeli tu ,wanatapeli hata hivyo viposho vya elfu mbili mbili wanavyowalipa hao vibarua utakuta kuna muda hawawalipi ,mambo ya ovyo kabisa
Hao Osha na Tucta wapo kwenye payroll ya hao ma cartel wenye viwanda so hakuna anaejali.
 
Watu wametoa lawama, malalamiko ila hawajaeleza nini kifanyike, serikali ifanye nini.

Hivi viwanda vinasaidia watu, ndio maana watu wanaendelea kwenda, tofauti na hapo usingewaona wanaenda huko viwandani
Wanaendelea kwenda sababu hawana option, lkn kiuhalisia hizo kazi hazifai kwa mustakabali wa afya ya binadamu.
 
Back
Top Bottom