Wenyeji wa Zanzibar, naombeni muongozo tafadhali

AY 5225

JF-Expert Member
Jul 16, 2023
484
1,135
Heshima yenu wakuu.

Niko Zanzibar kwa siku kadhaa sasa na nimekuja kwaajili ya kutafuta ridhiki. Naomba tips/muongozo kwa yeyote anayejua wapi naweza kupata kazi/kibarua na itapendeza zaidi malipo yakiwa ni kwa siku maana sina makazi.

Lengo langu ni kuwa na kazi mbili; moja ya kuifanya asubuhi mpaka jioni na nyingine iwe ya usiku mpaka asubuhi (ikiwa ya ulinzi itafaa pia maana nina cheti cha mafunzo ya JKT).

• Taaluma yangu ni degree ya management of social development.
• I have an excellent command of English na Kiswahili.
• Sina tatizo lolote la kiafya ninalolijua.
• Jinsia yangu ni (ME) na umri ni miaka 24.

Nina kitambulisho cha taifa na nimekuja na barua ya utambulisho wa makazi kutoka kwa mtendaji back home. Siombi mtu anisaidie makazi wala chakula, ninachoomba ni maelekezo ya wapi naweza kupata nafasi za kazi/vibarua kwa mchanganuo niliyotoa hapo nyuma na niko tayari kurudisha fadhila (pesa kidogo ya asante) kwa atakaenisaidia kufanikisha suala hili.

Nimejitambulisha kwa sheha na bag langu nimeomba anitunzie kwa muda nikiwa natafuta mahali pa kujishikiza. Kwa sasa napatikana maeneo ya Airport karibu na Golden Tulip hapa.

Naombeni muongozo wakuu.
 
Huyu jamaa kwa ukarimu kabisa jana nilimpigia simu tukaongea fresh tu leo pia nilimpigia tukaongea

Nimetoka kumtafutia kazi alizozitaka nampigia namuuliza umefikia wapi mpaka sasa kanikatia simu

Nahisi ashapata wenyeji

Kila la kheri kijana
We ni mtu sana. Endelea ivo ivo mkuu. Pamoja sana.
 
Huyu jamaa kwa ukarimu kabisa jana nilimpigia simu tukaongea fresh tu leo pia nilimpigia tukaongea

Nimetoka kumtafutia kazi alizozitaka nampigia namuuliza umefikia wapi mpaka sasa kanikatia simu

Nahisi ashapata wenyeji

Kila la kheri kijana

" Salio lako ni: Tsh0, Gawia (Bonasi): + MB 0-25/09/2023 "

Duuh! mkuu nikukatie simu kwa sababu zipi! Kama unakumbuka kwenye uzi wako na hata wangu nilisema simu yangu ni kuu kuu na ndio maana nikaweka mawasiliano yangu hadharani kwakua hata PM siwezi kufungua. Uliponipigia mara ya pili asubuhi simu yangu ikazima charge ghafla (kuitumia ni mpaka uwe karibu na charger) na nadhani nilikwambia nilikua na jamaa wa garage/car wash pale maana ndo ninapolala hivyo kupata sehemu ya kucharge simu yangu ni hekaheka.

Anyways, niko Smiles resort huku Nungwi na ndo nimepata sehemu ya ku'charge. Nimetaka kukutafuta ndo nimegundua bundle langu lime'expire, kuingia online ndo nakutana na message yako hii.

Umenikosea sana kuyaleta huku ila no hard feelings mkuu wala sikudai chochote, shukrani sana kwa ukarimu wako though, Allah akuzidishie In Shaa Allah.
 
Kweli kabisa mkuu, nauona mwanga.
Kuna mahala pengine wanapotoa vibarua unapajua?

hapana mkuu, ishu za vibarua mara nyingi zinataka connection, Anaweza toka mtu SHinyanga moja kwa moja akaja kazi zikiwa zinamsubiri huku wewe unahangaika hapo hapo ukawa hupati. Ila ukikomaa kidogo utazitia mikononi tu.
 
hapana mkuu, ishu za vibarua mara nyingi zinataka connection, Anaweza toka mtu SHinyanga moja kwa moja akaja kazi zikiwa zinamsubiri huku wewe unahangaika hapo hapo ukawa hupati. Ila ukikomaa kidogo utazitia mikononi tu.
Sawa mkuu, shukrani sana.
Pia naomba kuuliza maswali haya mawili;
1. Shamba gani ina hotel nyingi zaidi?
2. Shamba gani ina site nyingi za ujenzi?
 
Sawa mkuu, shukrani sana.
Pia naomba kuuliza maswali haya mawili;
1. Shamba gani ina hotel nyingi zaidi?
2. Shamba gani ina site nyingi za ujenzi?
Nungwi Kuna hotel nyingi zaidi ikifuatiwa na kusini paje, bwejuu,michamvi,jambiani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom