Vibali vya uhamisho kwa watumishi wa umma

JOSE KASANO

Senior Member
Apr 23, 2013
120
93
VIBALI VYA UHAMISHO KWA WATUMISHI WA UMMA

E Mungu Muumba mbingu na nchi,umeiwekea Dunia vitu vyote wakiwemo Wanadamu.Umewapa wanadamu uwezo wa kuongoza na kutawala viumbe wengine. Twakuomba katika kuongoza na kutawala, uwajalie viongozi wetu wa Tanzania afya njema, Hekima na Busara ili pamoja na mambo mengine waweze kufanya maamuzi ya haki kuhusu watu maskini waliooko chini yao ili wewe MUNGU wa Kweli uweze kupata UTUKUFU na KUINULIWA. AMINA.

Nawasalimuni kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania:

Bila shaka mmeitikia. KAZI IENDELEE NA MAMA SAMIA

Ndugu viongozi wetu;

Rais Dr.Samia Suluhu Hassani, Mwanamke wa Kwanza kuongoza Taifa letu pendwa la Tanzania na mama mlezi wa familia, ndoa unaijua umeiishi na unaiishi na unalea ndoa zote za Watanzania.

Mh. Dr. Philipo Mpango; Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wewe ni kiongozi pekee,kwa muonekano wako ni kama Kasisi wa Dini Fulani, baba, mpole na mnyenyekevu kweli.Ni baba wa familia,unaishi na ndoa yako, unajua umuhimu na nafasi ya ndoa kwa mtumishi wa Umma.

Waziri Mkuu;Mh.Kassimu Majaliwa Majaliwa; Baba mtendaji kazi,mcheshi na mchangamfu,unaijua ndoa na umuhimu wa watumishi wanandoa kuishi kwa pamoja katika kuleta tija na ufanisi wa utendaji kazi.
Mh.Simbachawene, Waziri wa Utumishi wa Umma Tanzania;unaijua ndoa na unafahamu kabisa kuwa watumishi wanandoa kuishi pamoja kuna tija na maslahi kwa Taifa.

Mh. Angela Kairuki, mama wa kazi usiyekuwa na mawaa unayeweza kufanya yoyote kwa ufanisi pindi unapopewa. Mama Angela unalea watumishi wa umma wote, unafahamu Raha na namna watumishi wanandoa wanaoishi kwa pamoja wanavyofanya kazi kwa furaha Amani na utulivu.

Dr. Tulia Akson, Mh. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,unaijua na unafahamu namna watumishi wanandoa wanaoishi pamoja walivyo na tija katika kutenda kazi kwa ufanisi akili zao zikiwa zimetulia.

TUNAWAOMBA, muwapatie vibali vya UHAMISHO watumishi walioomba kuhama kwa sababu mbalimbali. Lakini leo ninaeleza hasa juu ya Uhamisho wa watumishi wanandoa.

Nimetaja viongozi wetu wachache wa Kitaifa kwa umuhimu wao na kwa madaraka waliyopewa ili kuweza kuondoa mkwamo wa vibali vya UHAMISHO kwa watumishi walioomba vibali TAMISEMI:-

Ni jambo la muhimu sana kuwapa uhamisho watumishi walioomba kuhamia maeneo ambayo WENZA wao na FAMILIA zao zipo ili kuwategenezea utulivu wa kiakili katika kutimiza majukumu yao ya kiutumishi.

Ikumbukwe hivi sasa kutokana na majukumu mbalimbali ya serikali na kwa sababu awamu ya tano ilizuia kabisa watumishi kuhama, mtumishi na mwanandoa mmoja anaishi Mtwara halafu mwingine anaishi Mara.Ili watumishiwa wanandoa hawa waweze kukutana ni lazima mmoja aidha awe na likizo, aombe ruhusu za mara kwa mara ama awe anatoroka kwenye majukumu yake ili walau familia iweze kumuona.

Katika zama hizi ambazo jamii imebadilika,tabia mbovu za ushoga,usagaji usaliti na matukio ya ajabuajabu yanatokea,ni kipndi ambacho wanandoa kuwa karibu na kujumuika kwa pamoja katika kutenngeneza malezi bora ya watoto ambao ndio viongozi wetu wa Taifa letu la Tanzania baadae.

Mtoto wa mtumishi ambaye amekua na amesoma bila kuexperience malezi ya wazazi wa pande zote mbili hakika hata baadaye akija kuwa kiongozi hawezi kulifaa Taifa kwa sababu ya muathiriko wa Kisaikolojia na mara nyingi hujikuta wanakuwa viongozi katili kwenye jamii ambao hajali ustawi wa watu wengine maana hawakuexperince exposure ya wazazi.

Wizara ya TAMISEMI na Utumishi ndizo wizara nyeti na mama katika kutengeneza msawazo na kulisaidia Taifa kwa hili.Wapo watumishi wa Umma wameomba uhamisho kitambo na wengine wanendelea kuleta maombi wizarani LAKINI hatima yao haijulikani.Imo mikononi mwenu. Saidia kutegua kitendawili hiki cha watumishi,wako kwenye ombwe la ajabu mno la kiakili,ni wagonjwa mno kuliko mnavyokiria.Mtumishi unapomwambia atafute wa kubadilishana naye,umempa adhabu kubwa na nzito na ambayo kwa kweli madhaa yake yamekuwa makubwa kama nitakavyoyaainisha baadaye.

MADHARA YA UHAMISHO WA KUBADILISHANA
Mtumishi kutumia muda mwingi kuzunguka kutafuta mtumishi mwingine wa kubadilishana naye badala ya kutumia muda mwingi kutoa huduma wa wananchi.

Watumishi kujikuta kwenye vitendo vya rushwa za fedha na ngono.

Mickahato mirefu sana isiyoakisi utendaji kazi wa serikali kwa watumishi katika kusainisha barua na kuzituma.
Mfadhaiko wa kisaikolojia kwa watumishi kwani baadhi yao baadaye michakato yao hukwama njiani bila kupata sababu.

MADHARA YA MTUMISHI MWANADOA KUISHI MBALI NA MWENZA WAKE

- UFANISI WA KAZI HUWA NI MDOGO kwa sababu ya utumia muda mwingi kufuatilia familia yake iliyoko mbali naye. Kupiga simu,facebook, Whastap, Instagram, Bluetooth ndizo zimekuwa zinalea familia hizo.

- AFYA ZA AKILI kwa watumishi wanandoa wanaoishi mbali hazio salama.Usishangae kumkuta mtu ofisini na mfadhaiko mkubwa hayuko katika hali ya kutoa huduma.

- USALITI wa kupindua miongoni mwao. Hawa ni wanadamu huduma ya ndoa ni muhimu na ina nafasi yake katika kumjenga mtu na kumletea masawazo wa akili.Anapoiosa wa mwenza wake basi kama hana Rehema na Neema ya Mwenyezi Mungu lazima atafute mbadala wa kupata tendo la ndoa. Usaliti huu umeleta maangamizi wa watumishi wengi katika ndoa zao. Wapo waliotekeleza amilia zao Jumla hususani wababa. Nashikiliwa Jumla na mchepuko hadi anasahau kuwa ana mke na watoto. Baada ya hapo serikali inaanza kukimbizana na watoto wa mtaani wakati wametengenezwa na kutowaruhusu hawa watumishi waishi kwa pamoja.

- MAGONJWA kwa sababu ya kutoishi pamoja na baadhi yao kutoweza kuzuia hisisa za miili yao,wamejikuta wanaambuizwa magonjwa kama UKIMWI,KASWENDE na KISONONO na wao kuwambukiz wenza wao bila kujua.Ikumbukwe baada ya watumishi kuumwa serikali hutumia gharama kuwatunza lakini baada ya wao kuondoka Duniani watoto wao ambao ni tegemeo la Taia huwa katika wakati mgumu na mzigo kwa jamii na Taia wa ujumla wakati ustawi wao ungezuiwa kwa kuwaruus wazazi wao kuishi pamoja.

- GHARAMA KUBWA ZA UENDESHAJI FAMILIA. Jamani Serikali tuoneeni huruma sana,vipato vya mishahara yetu mnavijua na hali ya uchumi mnaijua kwa watumishi wenu,gharama tunazotumia ni kubwa mno katika kuendesha familia zetu hali inayopelekea umaskini miononi mwetu kuwa mkubwa mno.

- VIFO VYA MAPEMA. Kutokana na kuathirika kisaikolojia wengi hupoteza maisha mapema kwa kushambuliwa na magonjwa ya akili.

- KUFANYA MAAMUZI YANAYOILETEA HASARA SERIKALI. utafiti tu kiongozi ambaye you mbali na familia yake maamuzi yake siku zote huwa si mazuri.Kwanza watu anaowaongoza hutakana wao waishi kama yeye hususani kwenye nafasi za maamuzi.Huwa wakali hata mahali ambapo hapastahili.Hili ni tatizo,utawakuta watumishi walioko chini yao wanaliakwa sababu ya kutosikilizwa na kutendewa mambo mema.

KWA HAYO MACHACHE TUNAOMBA SERIKALI KUPITIA TAMISEMI JAMANI MTUMISHI KUHAMA NI HAKI YAKE KUTOKANA NA SABABU ALIZOAINISHA. TOA VIBALI VYA UHAMISHO KWA WATUMISHI WOTE BILA KUBAGUA SIJUI HUYU ANABADILISHANA HUYU KAFANYEJE. VIBALI VINAVYOOMBWA TAMISEMI TAYARI MTUMISHI ANAKUWA AMESHAPATA NAFASI HUKO ANAKOTAKA KUHAMIA.

AHSANTENI SANA NA BWANA AWABARIKI MKILIFANYIA KAZI OMBI HILI MUHIMU.
 

Attachments

  • KUHUSU UHAMISHO WA WATUMISHI WA UMMA WANANDOA.pdf
    144.7 KB · Views: 32
Mtanzania ni kama mnyama tu! Hakuna mtu wa hovyo kama mtanzania...

Hizi mentality za kijamaa za kutukuza wenye mamlaka ili mle ilihali hayo mamlaka yanatoka kwenu ndo yanawafanya muonekane daraja duni na dhalili sana hata dawamu...

Umetia kinyaa sana.
 
Hapo mwanzo umeweka maelezo meengi kupitiliza. All in all, ushauri wangu wa watumishi wa serikali.

Ukiona vikwazo vya kuhama ni vingi, kaa chini tafakari. Kama vipi, unawaachia kazi yao! Halafu unaenda zako kufanya ishu zako nyingine. No wa out.
Kumbe Kuna mda una akili we boya
 
Nilimwambia mkurugenzi naomba kuhama akanambia nisubir nikaandika barua nikaona anaiangalia kama mafi ya kuku nikakabidhi ofisi nikamfuata ofisini nikamuaga kwa nyodo akanijibu utarudi tu nikasepa baada ya miezi sita akanipigia (nilikuwa HQ) akisema nirudi ili niandike barua ya kuhama sikumjibu na huu mwaka karibu 7 nipo kitaa na maisha yanasonga yaani ukiwaendekeza hawa watu utakufa kabla ya siku zako
 
Back
Top Bottom