Varangati: Mbunge Msigwa na DC Kasesela nusura ngumi zichapwe

hii ni too low kwa ccm. yaani wanajipa hata haki miliki ya kutoa misaada?
Mkuu ukisikia kuishiwa mipango ndio huko watahangaika sana hao ma dc maana mbunge ni chaguo la wananchi wenyewe
 
''Mimi nimechaguliwa na wananchi, wewe umeletwa na Rais''-Msigwa.

''Manispaa niya kwetu, huyu ameletwa tu-Msigwa

''Leo ninakutolea uvivu na waandishi wa habari wanachukua-Msigwa.

''Kila kwenye kikao cha CCM unanisema, acha mambo ya kishamba shamba-Msigwa.

''Sasa hivi nitapambana na wewe serially''-Msigwa

''Maafa sio ya kwako, maafa niya Watanzania wote''-Msigwa

''Si una power ya kuniweka ndani, kaniweke basi ndani''-Msigwa

''Sina shida ya kukuweka ndani''-Kasesera

''Sikiliza, mimi ninakuheshimu sana ndio maana sina shida ya kubishana na wewe''-Kasesera.

Politicians and politics at its best!

Wanasiasa wetu wanataka kutwangana ngumi, kisa nani anakuwa mbele mbele katika kutoa misaada ya wahanga wa mvua ya el nino!
Huyo kasesera anajitafutia kufa njaa
 
Kasesela amezoea kuishi kwa kujipendekeza na kubebwa, Hawezi kujisimamia mwenyewe!!
 
Kuwa mpinzani ktk nchi ambayo watendaji wa serikali ni makada wa chama dola na wanatenda ili kuangusha juhudi za mbunge wa upinzani ktk maeneo waliyopo,unahitaji kuwa "fyatu" kidogo ili uendano nao..Vinginevyo utahujumiwa mpaka upoteze muelekeo.Mambo mengine tujadili kama vile ndio tumevaa viatu vya Mbunge Peter Msigwa....U sometimes need to be "crazy" to cope with Tanzania multi-Party Politics....Hakuna cha msalie mtume na kujirinda hata kwa kutandika mtu makofi...A Traditional principle of "lesser of two evils" is applied,Yaani unachagua njia moja ambayo ni "kali" lakn haina madhara....Kuliko Msigwa kujificha na kumsimanga (backbite) DC au kumtandika ngumi....bora kachagua hii njia ya "makavu laivu".....Tatizo tumelelewa kwa njia ya "unafiki" ...kukaa na vitu kifuani!!Fumua uwe huru...hata DC mwenyewe kaonekana kukiri na kusema "basi yaishe"......Ila nimecheka,Ka-Msigwa kana mkwaraaaaaaaaa(Credit:Copy and Paste from Msigwa's Fb Account)
 
Ndiyo maana wengine wanenda kwenye maafa wanawabeba waandishi wa habari badala ya kubeba waathirika hahahahahahaaaa ili mwenye nchi amuone
 
Vurumai hizo zilizotokea baada ya Msigwa kukasirishwa na kitengo cha DC kutaka kumuengua ili asionekane anatoa msaada kwa watu wa jimbo lake

Huyu anayejiita Mchungaji Msingwa sio mchungaji ni lipagani fulani hivi lililojivika kola ya uchungaji

Biblia katika MATHAYO 6:2-5 unasema "Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni. Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu. Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume; sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

Hivi kama mchungaji hadi anataka kupigana ili aonekane akitoa msaada? dini hizi hatari.Hivi ni mchungaji wa kanisa gani?
 
Inaelekea hawa maDC wanafikiria njia ya kupata attention ya Magufuli na kuonekana wanafanya kazi ni kuwakorofisha wabunge wa wilaya zao na wao kuonekana kwenye luninga wanapogombana ; naamini Rais hataingia kwenye huu mtego kuwa wale wanaojionesha kwenye luninga na kugombana na wabunge ndio watabaki kuwa maDc au kupandishwa kuwa ma RC kama alivyoahidiwa Makonda !!!

Labda Makonda Kawashauri Ukitaka Chapuo kwa Rais Mtukane Mbunge hivi, au Mzuie Kuongea, Au Mseme Mbunge kwenye vyombo ya habari, Mr. Kasesela Stay Away From Makonda, Dishonest is not a good shortcut to success and honor.
 
Kwa mtu anayemjua huyo DC ataelewa Msigwa anamaanisha nn. huyo dc ameshagombea ubunge zaidi ya mara 4 na zote anabwagwa mbali so chuki ni kawaida kuwepo, anapenda kuonenaka sana publicity kama wema sepetu vile
 
Miaka miwili iliyopita, Watz hawakumwelewa Polepole ni mtu wa aina gani. Yule ni mtu wa aina ya "popoma". Always anaamini kwamba kile anachokiwaza na kukifanya basi jamii inakihitaji, wakati siyo.
 
Kazi kwel
View attachment 324104

View attachment 324105

View attachment 324106

Kumetokea mabishano makali sana kati ya Mbunge Msigwa na DC Kasesera eneo la Iringa Mjini baada kuwa wamewatembelea wahanga wa nyumba zilizoezuliwa na mvua kubwa na kusababisha baadhi ya watu ktk Tarafa ya Nduli

Vurumai hizo zilizotokea baada ya Msigwa kukasirishwa na kitengo cha DC kutaka kumuengua ili asionekane anatoa msaada kwa watu wa jimbo lake bali DC ndio ionekane anajali wananchi.Shutuma zilienda mbali baada ya Msigwa kumueleza DC kuwa anajuwa anamhujumu na amekuwa anapanga mikakati ya siri ya kumfanyia hujuma ili aonekane hafanyi kazi jimboni kwake.

Juhudi hizo zimefanyika week iliyopita ambapo DC kwa kushirikiana na Humphley Polepole waliandaa "mdahalo" na wanafunzi wa vyu vikuu mkoani Iringa na kuanza kumsema vibaya Mbunge Msigwa,katika mdahalo huo Polepole amerekodiwa akisema Iringa awalikosea sana kumchagua Msigwa sbb alikuwa anamuunga mkono "fisadi" Lowassa

Wakati DC Kasesera alimshutumu Mb Msigwa kutokwenda Tarafa ya Pawaga kusaidia wahanga wa mafuriko na Msigwa akamjibu kuwa aanze kumwambia Lukuvi kwanini hajaenda maana Tarafa ya Pawaga ipo ndani ya Jimbo la Isimani,na hata yeye akienda sio lazima DC ajue,kama ambavyo yeye anaenda na kupiga picha na kurusha Facebook akimbeba mpiga picha ambaye haitaji msaada wa kubebwa.

Vurugu hizo ziliamuliwa na diwani na Meya wa Mji. Mwishoni Msigwa akamwambia DC awaite polisi wamuweke ndani maana katika viako vya CCM DC Kasesera amekuwa akisema lazima amuweke ndani Msigwa kumtia adabu
Kazi kweli kweli......
 
Ha ha ha. Cheki Msigwa anavyovua koti lake. Eti "...everywhere, in Facebook sijui wapi...I use strategies..." Huyu mchungaji aache kupanic. Mwisho wa siku yeye ndio ataonekana kichaa. Kasesera kamseti na yeye kaingia kichwa kichwa.
Kasesera ni mpita njia huyo,msigwa ndiye chaguo la wana wa iringa
 
H

hakuna cha kichwa kichwa hapo Mkuu wa wilaya alimkosea Mbunge kwa kutaka kumdhalilisha ni vyema wakuu wa wilaya wakawaheshimu wabunge pasipo kuweka itikadi za Vyama vyao mbele.
Mkuu minyoo hilo tatizo la wakuu wa wilaya nafikiri wanakuwa wanatekeleza maagizo ya wakubwa zao kutoka juu
 
Fanya vyote ila usitake kutafuta sifa au kujitolea kwenye jimbo la CDM..Yani upate sifa bila yeye kuwepooo??Muulizeni Mary Mwanjelwa alifanywa nini na sugu
 
Kamchana live huo ndiyo ukweli, lazima tufike mahali tuachane na kasumba za kuendekeza Majungu na itikadi za ccm kwenye shida zinazowahusu wananchi wote.
Upo sahihi mkuu na huo ndio uawala bora tunategemea kuona kutoka kwa viongozi wetu
 
Safi sana Mchungaji Msigwa. Siku nyingine akileta tena ungese ungese mchape kibao. Hilo kuu la wilaya jinga kabisa
Nashindwa kujua hawa wakuu wa wilaya wanakuwa wanatumia busara zipi hadi kupelekea kutaka kumdharau mbunge wa sehemu husika wakati huyo mbunge ndiye chaguo la wananchi wa hapo
 
Ni kweli.
Ila naona alishindwa kudhibiti hasira zake mpaka ameshindwa kutoa maneno kwa ufasaha. Huyu kasesera anaonekana ni mtu mwenye dharau au nyodo tuseme kwahiyo mtu unapaswa uwe technical kidogo kumvaa. Hapo mbunge kaonekana kama amepanick au analalamika, jambo ambalo DC kalichukulia poa tu.
Kwani kupanic ni dhambi?
 
Huyo mkuu wa wilaya kabla ya kuteuliwa alikuwa ni mtu mngwana sana tokea akiwa shuleni Azania hadi akiwa kwenye harakati zingine nimeshangaa kumwona kaaza ukorofi kwa kuwaiga akina Polepole ambao ni Watumishi wa Benard Membe adui namba moja wa Lowasa.
Inasikitisha sana kwa kiongozi kuwa na mambo ya ajabu kama haya
 
Back
Top Bottom