Uzuri wa mwanamke...

Kidudu Mtu

Member
Nov 7, 2009
64
0
Utasikia mtu anasema "mwanamke yule mzuri" lakini unaweza usiuone huo uzuri anaousifia. Hivi uzuri wa mwanamke ni nini? Vigezo vipi mwanamke awe navyo ili wengi wamuone mzuri?
 
Uzuri wa mwanamke ni tabia sio sura ..
Baada ya hapo kila mtu ana uzuri wake wa asili ..mwingine ana macho mazuri ,nywele ,masikio ,pua,midomo au hata anatembea vizuri ,wengine watasema colour yake ina mvuto.
Lakini kinachobeba yote ni tabia yake
 
tabia, usafi, heshima, upendo, utii. sura au maumbile yanafuata baadae! Usisahau 'utundu' awapo kitandani!
 
tabia ya mwanamke huwezi iona mara moja kwani hakuna mwenye uwezo wa kuuchunguza moya wa mtu, tunachokiona kwa nje hutubashiria ya ndani.
 
...lakini unaweza usiuone huo uzuri anaousifia....

...tafsiri yake unatofautiana baina ya mtu na mtu kutokana na malezi, makuzi na uzoefu baina ya mtu na mtu. Kitachokuwa kizuri kwangu sio lazima kifanane na uzuri utaouona wewe.

...Uzuri upo wa aina mbili, ...unaoonekana kwa nje (ambao unaonekana kwa wataovutiwa naye) i.e Sura nzuri, Umbile zuri, etc.

...na ambao umejificha moyoni. (utapomjua/fahamu au kumuelewa), i.e tabia, maadili, etc
 
...
...na ambao umejificha moyoni. (utapomjua/fahamu au kumuelewa), i.e tabia, maadili, etc

Karibu sana mpwa Mosquito tumekumiss kweli kweli karibu mwana mpotevu.
Naona mlikuwa njia moja na Nyani Ngabu nae karejea.
Kwangu uzuri wa mwanamke ni al-batar
 
Ni kweli mkuu,

Hakuna kigezo rasmi cha uzuri. Uzuri anaujua anayeutafuta. Lakini kwa ujumla, maumbile ya nje yanakuwa na nafasi ya juu pale unapomwona binti mara ya kwanza (spot siting).Baada ya hapo ndipo uzuri wenyewe kama wanavyosema wadau wengine unapokuja, ikiwemo tabia katika ujumla wake na pia kuutunza huo uzuri wa nje. Ndiyo maana kila mtu anapata mwenzake hata kama watu wengine wanashangaa.

Na katika utafutaji, mtu anaweza kuanza na mvuto wa nje ndo asonge mbele. Ila mahusiano yanayotokea baada ya kuzoeana hayaangalii sura ya nje. Ndo maana unaweza kukuta watu wa sura, haiba, elimu na kila kitu kinachooneka kiko tofauti lakini wenyewe wamependana hadi watu wanaowatazama hawaamini kama inawezekana!
 
Karibu sana mpwa Mosquito tumekumiss kweli kweli karibu mwana mpotevu.
Naona mlikuwa njia moja na Nyani Ngabu nae karejea.
Kwangu uzuri wa mwanamke ni al-batar

...Shukran ndugu yangu, tupo pamoja! :D
 
Uzuri wa mwanamke ni macho ya anayemtizama,sio kitu kingine chochote wala tusijidangaye!!!
 
Uzuri wa mtu ni subjective, inategemea na mtu anayeona huo uzuri. ndo maana utakuta mtu anamsifia mwanamke/ mwanaume fulani wakati wewe hata huoni huo uzuri anaousifia. so, inategemea unapenda nini katika mwili wa unayemuona mzuri.
 
Naona wakuu wote ni kama mnakubaliana ya kwamba uzuri wa mwanamke ni machoni kwa mtu,lakini kuna wakati ni kama jamii yote inakubaliana kwamba fulani ni mzuri.Hapa vipi,una maana hapa binti atakuwa ametimiza vigezo vya kila mtu?
 
Uzuri wa mwanamke ni macho ya anayemtizama,sio kitu kingine chochote wala tusijidangaye!!!

Na kipofu hajui uzuri?...is more than that Man, na ndo mana wengi wakaishia kusema tabia lakini hata kama atakuwa na tabia nzuri, sura mzuri maumbile mazuri bado tafsiri huwa inaishia kwa kile kinachomfanya yeye aitwe "Mwanamke" .

Yote mengine ni nadharia tu na maono na hisia za kimtazamo wa kila Mwana wa adamu.
 
Uzuri wa Mwanamke unaanza kwenye umbo lake na sura yake..tabia hufuata baada ya kukubali umbo lake...

Kama umbo choka mbaya tabia wala huwezi anza kujisumbua...inaitwa NOT MY TYPE!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom