uzinifu

Mandago

JF-Expert Member
Feb 8, 2008
238
99
Uasherati maana yake ni uzinifu baina ya watu wawili ambao hawakuoana kisheria. Madhara ya uzinifu ni makubwa ikiwa ni pamoja na kuleta fitina, ugomvi na hata kuuwana. Maradhi yanayoletwa na uzinifu ni makubwa na ambayo hayaponeki. Madhara katika jamii ni makubwa na mabaya ambayo inafikia kiwango cha kaka kumuoa dada kwa kutokujua baba zao au asili yao. Uzinzi unampelekea mtu kuingia Motoni. Kama ilivyokuja katika Qur-ani, Mwenyezi Mungu S.W.T. kasema katika Suratil Israa (Bani Israil) aya ya 32, "

"Wala msikaribie zina. Hakika hiyo ni uchafu (mkubwa) na ni njia mbaya (kabisa)."

Na pia imetajwa adhabu ya zina duniani na Akhera kwa kauli ya Mwenyezi Mungu S.W.T. katika Suratil Furqaan aya ya 68 mpaka 70, "

"Na wale wasiomuomba mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu, wala hawaui nafsi aliyoiharimisha Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa haki, wala hawazini; na atakaefanya hayo atapata madhara (papa hapa ulimwenguni kabla ya Akhera). Na atazidishiwa adhabu siku ya Kiyama na atakaa humo kwa kufedheheka (muda mrefu kabisa) milele. Ila yule atakayetubia na kuamini na kufanya vitendo vizuri..."

Na Mwenyezi Mungu S.W.T. kasema katika Suratin Nuur aya ya 2, "

"Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamume, mtandikeni kila mmoja katika wao mijeledi (bakora) mia. Wala isiwashikeni huruma kwa ajili yao katika (kupitisha) hukumu hii ya Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi mnamuamini Mwenyezi Mungu na siku ya Mwisho. Na lishuhudie adhabu yao (hii) kundi la Waislamu."

Wanavyuoni wamesema kwamba aya hii iliyotajwa juu (Surat Nuur aya ya 2) ni ile adhabu ya duniani kwa mwasherati (mzinifu) ambaye hakuoa/hakuolewa. Ikiwa mtu aliwahi kuoa/kuolewa kabla, akazini, kwa sheria iliyotolewa na Mtume S.A.W. adhabu ya duniani ya yule mzinifu mwanaume au mwanamke ni kupigwa mawe mpaka afe, hii adhabu kali huamrishwa baada ya mashahidi wanne kutoa ushahidi wao ya kwamba wameona kitendo cha kweli cha zina, au baada ya kukiri mmoja wao kati ya wawili waliozini kuwa kweli katenda kile kitendo. Kama ilivyokuja katika Hadithi iliyopokelewa na Jaabir bin Abdallah R.A.A. na kutolewa na Abu Daud Mtume S.A.W. kasema, "

"Hakika mwanaume alimzini mwanamke. Mtume S.A.W. akaamrisha aadabishwe kisheria akapigwa mijeledi (mia). Kisha akaambiwa kuwa yeye kaoa. Akaamrisha apigwe mawe mpaka afe."

Ikiwa hawataadhibiwa hapa duniani na wakafa bila kutubia, wataadhibiwa katika Moto wa Jahannam kwa kupigwa mijeledi ya moto. Na hatari ya Mwislamu wakati wa kufanya kile kitendo, Mwenyezi Mungu Mtukufu humnyang`anya Uislamu wake. Kwani hakiwi kitu kizuri na kibaya kukutanika pamoja sehemu moja wakati mmoja. Mtume S.A.W. kasema katika Hadithi iliyopokelewa na Abu Huraira R.A.A. na kutolewa na L-Bukhari na Muslim, "
"
"Hazini mzinifu wakati anapozini naye ni Mwislamu, wala haibi mwizi wakati wa kuiba naye ni Mwislamu, wala hanywi ulevi wakati wa kuunywa naye ni Mwislamu. Lakini toba inarejesha imani."

Na katika Hadithi iliyopokelewa na Abu Huraira R.A.A. na kutolewa na Ttirmidhi na Abu Daud na Baihaqi, Mtume S.A.W. kasema, "

"Atakaezini au kunywa ulevi (naye ni Mwislamu) Mwenyezi Mungu anamnyang`anya imani kama anavyovua shati kutoka kwenye kichwa chake."

Tukirejea wakati wa zama za Mtume S.A.W., alikuwa akiwaapisha na kuchukua ahadi kutoka kwa wanawake na wanaume kabla ya kuingia katika Uislamu. Na hicho kiapo cha ushahidi wa kutokuuwa au kuiba au kuzini kinachukuliwa kuwa ni ahadi ya kweli kwamba haya mambo yameharamishwa katika Uislamu. Mwenyezi Mungu S.W.T. kasema katika Suratil Mumtahinah aya ya 12, "

"Ewe Nabii! Watakapokujia wanawake walioamini wanakuahidi ya kwamba hawatamshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote, wala hawataiba, wala hawatazini, wala hawatawaua watoto wao, wala hawataleta uzushi wanaozusha tu wenyewe baina ya mikono yao na miguu yao, wala hawatakuasi katika jambo jema, basi peana ahadi nao na uwatakie msamaha kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, Mwingi wa rehema."

Na adhabu ya mzee mzinifu siku ya Kiyama Mwenyezi Mungu S.W.T. hatasema naye wala kumtazama (kwa jicho la rehema) na wala kumtakasa (madhambi yake) na atakuwa na adhabu kali. Kama alivyosema Mtume S.A.W. katika Hadithi iliyopokelewa na Abu Huraira R.A.A. na kutolewa na Muslim na Nnasaai, "

(Aina ya watu) watatu Mwenyezi Mungu hatasema nao siku ya Kiyama wala hatawatazama na wala kuwatakasa na watakuwa na adhabu kali: Mzee mzinifu, na mfalme mwongo, na maskini anayejivuna."

Na sababu kubwa ya Uislamu kuharamisha kuzini na mke wa jirani kwani dhambi yake ni mara kumi kuliko kuzini na mwanamke asiyekuwa wa jirani. Kama ilvyokuja katika Hadithi iliyopokelewa na Ibn Masoud R.A.A. na kutolewa na L-Bukhari na Muslim kasema, alimuuliza Mtume S.A.W., "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Jee, ipi dhambi kubwa? Mtume S.A.W. akamjibu kama ifuatavyo, "

"Usijaalie kitu chochote sawa na Mwenyezi Mungu, na hali Yeye kakuumba." Nikasema: "Hakika hiyo ni kubwa." Nikauliza: "Ipi nyingine?" Akajibu: "Usimwue mtoto wako kwa khofu atakula na wewe." Nikauliza: "Ipi nyingine?" Akajibu: "Usimzini mke wa jirani yako." Kasema: Ndipo Mwenyezi Mungu alipoteremsha Suratil Furqaan tokeya aya ya 68 hadi 70 kusadikisha ukweli wa kauli ya Mtume S.A.W., "

"Na wale wasiomuomba mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu, wala hawaui nafsi aliyoiharamisha Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa haki, wala hawazini; na atakaefanya hayo atapata madhara (papa hapa ulimwenguni kabla ya Akhera). Na atazidishiwa adhabu siku ya Kiyama na atakaa humo kwa kufedheheka (muda mrefu kabisa) milele. Ila yule atakaetubia na kuamini na kufanya vitendo vizuri..."

Kama inavyojulikana Iblisi daima ni adui wa binadamu, anamkimbilia kumpoteza na kumwangamiza na bila mtu yule kuhisi kuwa anayoyafanya yote hayo mabaya Iblisi ndiye anayemchochea na kumshangilia na kumpambia uovu na kuona huo uovu ni mambo mazuri wala hayana kitu akiyafanya. Iblisi pia anayafumba macho ya binadamu na huwa mtu yule haoni na kumtumainisha kuwa wewe utaishi miaka mingi wala usijali tumia uhai wako. Ukifikia umri wa uzee hapo ndipo unaweza kutubu. Jee! Kuna mtu anaejua ataishi miaka mingapi hapa duniani?" Mtume S.A.W. kasema katika Hadithi iliyopokelewa na Jaabir bin Abdallah R.A.A. na kutolewa na Muslim, "

"Hakika Iblisi anatuma askari wake (wa Kijini) katika ardhi na kuwapa ahadi kuwa yeyote yule atakayempoteza Mwislamu atavikwa taji. Kwa mfanyaji fitina mkubwa kabisa kati yao ni karibu naye huyo Ibisi katika cheo. Kisha (Shetani) mmoja wao akirejea baada ya kazi yake kwa Iblisi husema: "Sikumwacha fulani mpaka amemwacha mkewe. Iblisi anajibu; "Hukufanya kitu; ataoa mwingine!" Shetani mwingine humsogelea Iblisi na kumwambia: "Sikumwacha fulani mpaka yeye na kaka yake wakawa maadui." Ibisi anajibu " Hukufanya kitu; watapatanishwa." Mwingine anakuja kwake na kumwambia: "Sikumwacha fulani mpaka amezini." Iblisi husema (kumwambiya huyo Shetani): "Naam. (Ama wewe, naam) umefanya kazi nzuri!" Kisha humkalisha karibu yake na kumvika taji. Mwenyezi Mungu atuepushe na shari za Shetani na askari wake."

Pia Hadithi iliyopokelewa na Abdallah bin Haarith R.A.A. na kutolewa na Ahmad na Tabarani, Mtume S.A.W. kasema, "

"Hakuna dhambi kubwa baada ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu mbele ya Mwenyezi Mungu kama mwanamume kuweka mbegu ya uzazi (manii) katika utupu usio halali yake."

Kwa sababu anaemzini mke wa mtu anakuwa kamfanyia dhulma mumewe, na ikiwa kashika mimba basi mtoto anaezaliwa huwa si miongoni mwao. Na ikiwa kamzini msichana hajaolewa akizaa mtoto wa haramu huwa kamwangamiza maisha yake na mustakbali wake. Na pia kamvunjia heshima yake na ya wazazi wake. Na zina imefananishwa na kumshirikisha Mwenyezi Mungu S.W.T. kwa sababu SHIRKI ni dhulma kubwa.
 
Basi ikimbieni zinaa kwa kufanya TOBA YA KWELI na kumrudia Mwenyezi Mungu. Acheni usanii MOTO UKO ATTIIII!!!
 
Ahsante Mshiiri kwa ujumbe mzuri sana huu!
Binadamu huwa yuko tayari kupoteza hata maisha yake kwa ajili ya kulinda vitu kama vile
"uhuru", "demokrasia", "utu", "heshima". lakini cha ajabu inakuwa ngumu kweli kweli kupigana ili kulinda kitu kinachoitwa "uhai", wakati bila uhai hakuna uhuru wala demokrasia wala utu wala heshima, sasa pointi yangu ni hii, hivi watu wakiacha zinaa si tutalishinda hili janga la Ukimwi na hivyo kulinda uhai ambao huondolewa kwa sababu ya maradhi hayo?
 
Mtu Mzinifu hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.

Ikimbieni zinaa; Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwemyewe.

Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo nanayofanana na hayo; katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambao ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
 
Asante sana ndugu Mandago kwa post yako hii muhimu sana, kweli kabisa Uzinifu ni uchafu mkubwa na dhuluma kubwa sana.
 
Ahsante Mshiiri kwa ujumbe mzuri sana huu!
Binadamu huwa yuko tayari kupoteza hata maisha yake kwa ajili ya kulinda vitu kama vile
"uhuru", "demokrasia", "utu", "heshima". lakini cha ajabu inakuwa ngumu kweli kweli kupigana ili kulinda kitu kinachoitwa "uhai", wakati bila uhai hakuna uhuru wala demokrasia wala utu wala heshima, sasa pointi yangu ni hii, hivi watu wakiacha zinaa si tutalishinda hili janga la Ukimwi na hivyo kulinda uhai ambao huondolewa kwa sababu ya maradhi hayo?

Asante Mkuu
 
ni dhahiri hakuna dhambi nyepesi wala dhambi nzito,na hakuna haja ya kuchagua dhambi fulani ivaliwe kibwaya kwa vile tu hisia na mapenzi binafsi na tamaa ya jamii inaelekea huko.Kwa tamaa na matamanio ya binadamu jamii fulani imeona kama uzinifu ni dhambi mbaya kuliko hata kuua,je ipi mbaya na athari kubwa zaidi kati ya hizo? Ni kama vile wengine wanaona kula nyamafu ni dhambi mbaya na wako tayari kumhukumu kifo mtu kuliko kutoa uhai wa watu kadhaa kwa kujilipua mabomu au uchawi na kuwapongeza wanaofanya hivyo.Dhambi ni dhambi haijalishi ina ladha gani na kila atendaye dhambi atakwenda jehanam
 
Mtu Mzinifu hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.

Ikimbieni zinaa; Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwemyewe.

Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo nanayofanana na hayo; katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambao ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.

Mkuu ahsante kwa haya maandiko ingekuwa vyema nawe ukaweka milango na aya ya haya maandiko.
 
ni dhahiri hakuna dhambi nyepesi wala dhambi nzito,na hakuna haja ya kuchagua dhambi fulani ivaliwe kibwaya kwa vile tu hisia na mapenzi binafsi na tamaa ya jamii inaelekea huko.Kwa tamaa na matamanio ya binadamu jamii fulani imeona kama uzinifu ni dhambi mbaya kuliko hata kuua,je ipi mbaya na athari kubwa zaidi kati ya hizo? Ni kama vile wengine wanaona kula nyamafu ni dhambi mbaya na wako tayari kumhukumu kifo mtu kuliko kutoa uhai wa watu kadhaa kwa kujilipua mabomu au uchawi na kuwapongeza wanaofanya hivyo.Dhambi ni dhambi haijalishi ina ladha gani na kila atendaye dhambi atakwenda jehanam

Kujiua, uchawi au uzinifu ni katika madhambi makubwa sana ambayo waislamu wamekatazwa kabisa na dini yao kuyatenda.
 
And too pitty, kwamba dhambi hii ndiyo inayoongoza kukua kwa sasa.

Kwahiyo ndugu Mandago umefanya la maana sana kutukumbushia jambo hili.

Inaweza isionyeshe umuhimu sana mtu anapoisoma hapa, lakini at least AMEKUMBUSHWA HILO!

BWANA YESU AKUBARIKI!
 
Aaaaaamen!
 
Back
Top Bottom