Uzinduzi wa Uwanja uliokarabatiwa wa Amani Zanzibar wakumbusha juhudi za ujenzi za Wachina

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
1704356039884.png

Mwishoni mwa mwaka 2023 ambayo ilikuwa Disema 27, rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi alifanya sherehe kubwa katika uwanja wa Amani, ikiwa ni moja ya mafanikio yake mengi makubwa tangu aingie madarakani mwaka 2020.

Sherehe hiyo ambayo ilikuwa ni mahsusi kwa ajili ya uzinduzi wa Uwanja wa Amani na kuwakutanisha Wazanzibari wengi waliokuwa na shauku, hamasa na imani kubwa kwa rais wao, ilifanyika baada ya uwanja huo kufanyiwa ukarabati mkubwa ambao umeweza kuupandisha hadhi na kuwa wa kimataifa, na sasa unatarajiwa kuwa miongoni mwa viwanja vitakavyoandaa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, mashindano yanayoandaliwa kwa pamoja na Tanzania, Kenya na Uganda.

Hata hivyo unapotaja uwanja wa Amani Zanzibar basi na China nayo haitakuwa mbali sana kwa kuwa inahusika pakubwa katika ujenzi wake. Tarehe 26 Machi Mwaka 1968, rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere alikwenda visiwani Zanzibar kuweka jiwe la msingi wa Uwanja wa Michezo wa Taifa huko Sebuleni, akipokelewa na wajumbe mbalimbali wa Baraza la Mapinduzi pamoja na Makamo wa kwanza wa rais Sheikh Amani Abeid Karume.

Baada ya shughuli za kuweka jiwe la msingi, Uwanja wa Amani ukajengwa kwa msaada wa serikali ya China na kufunguliwa mwaka 1970. Huu ulikuwa ndio mradi wa kwanza kwa China wa uwanja wa michezo barani Afrika, ambao uliashiria mwanzo wa diplomasia yake ya ujenzi wa uwanja kwa miongo kadhaa.

Katika kipindi hicho cha mwaka 1968, ambapo China ilijenga uwanja huo uliogharimu kiasi cha shilingi milioni sita kwa wakati huo na kuchukua miaka miwili tu hadi kukamilika kwake, uwanja huo ulikuwa na uwezo wa kubeba watu elfu kumi na tano, huku ukiwa na hoteli moja kubwa ya ghorofa tatu, vilevile kukiwa na viwanja vingine vya majaribio ndani ya uwanja huo.

Katika sherehe za kuweka jiwe la msingi aliyekuwa Naibu Balozi wa China nchini Tanzania Pao Ping alisema kwenye hotuba yake kwamba rais Nyerere na makamo wake wa kwanza Sheikh Karume sio kama wanapendezwa na shughuli za michezo tu, bali pia wanathamini sana urafiki uliopo baina ya China na Tanzania. Balozi Pao aliendelea kusema kwamba uhusiano na urafiki huo ulianza zamani na kila siku unazidi kuendelea, na ujenzi wa uwanja huo unazidi kuonesha wazi uhusiano wao wa mapenzi baina ya watu na nchi hizi mbili.

China ilianza kushirikiana bega kwa bega na Zanzibar kabla hata visiwa hivi kufanya mapinduzi yake. Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964, yaliongeza ushawishi mkubwa wa Wachina kisiwani humo ambapo China iliutambua utawala huo mpya mara moja na kutoa misaada ya kijeshi na misaada ya maendeleo ukiwemo ujenzi wa Uwanja huu wa Amani.

Baada ya ufunguzi wake uwanja huu ukawa unatumika kufanyia shughuli kubwa mbalimbali huko visiwani Zanzibar, yakiwemo maadhimisho ya kitaifa ya kila mwaka ya Siku ya Mapinduzi. Hata hivyo China haikuishia kwenye ujenzi tu, bali hata kwenye kazi ya kuufanyia ukarabati uwanja huo pia ilihusika. Uwanja huo ulifanyiwa ukarabati tena kwa usaidizi wa Wachina, na kufunguliwa tena mwaka 2010.

Zikitupia macho nyuma na kuona mafanikio makubwa yaliyopatikana, China na Tanzania sasa zimekuwa na faraja kubwa kuona mbegu iliyopandwa na waasisi wa nchi hizi mbili imeota na kuwa mti mkubwa ambao umekuwa ukiengwaengwa na kutunzwa na pande zote. Awali ilikuwa ni urafiki wa kawaida tu, lakini sasa nchini hizi mbili zimekuwa ndugu wa karibu wakisaidiana na kuungana mkono kwa kila hali.

Mbali na uwanja wa Amani Zanzibar, katika miaka hiyo ya 70 China pia iliacha alama nyingine kubwa Tanzania ambayo inaendelea kuonekana na kukumbukwa hadi leo na Watanzania na Waafrika kwa ujumla “Reli ya TAZARA”. Kwa maana hiyo ni sawa tu kusema kuwa China ilianza kunyoosha mkono wake wa misaada kwa Tanzania tangu zamani sana, na uzuri ni kwamba hadi leo bado inaendelea, hasa katika ujenzi wa miundo mbinu kupitia Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, FOCAC, na Pendekezo la Ukanda Mmoja Njia Moja (BRI).
 
Urafiki wa Tanzania na China ni wa miaka mingi sana, tangu enzi za kina Mao na Nyerere waliokuwa Wajamaa...maswahiba wa kiitikadi
 
View attachment 2861546

Huu nao je, CCM hawajaupora?
 
Naomba kujua ni miradi gani mikubwa imefanywa na wakandarasi wetu wa ndani?!!
 
Back
Top Bottom