myoyambendi
JF-Expert Member
- Sep 13, 2013
- 150,961
- 668,078
✔️✔️Nchini Tanzania kuna chama cha wakunga, kinachowatambua wakunga na kutumika kama chombo cha kuwasemea wakunga nchini humo
✔️✔️Nchini Tanzania kuna chama cha wakunga, kinachowatambua wakunga na kutumika kama chombo cha kuwasemea wakunga nchini humo
✔️✔️✔️Umoja wa Mataifa unawatambua wakunga wa aina hii ya Issa Mbaga, na kupitia shirika lake la afya (WHO), limekua likiadhimisha mpaka siku maalumu kwa ajili yao. Mbaga anasema kutambulika kwa wakunga kunampa faraja kuendelea kutoa huduma hiyo kwa akina mama.
📌📌Matamanio ya mkunga huyu kijana ni kuona anafanya shughuli hiyo kisasa zaidi kuliko ilivyo sasa.
Tayari amepata kompyuta kutoka kwa mmoja wa wanawake aliowasaidia, na ameanza kutumia mitandao ya kijamii kuwafikia wanawake wengi nchini Tanzania. Lengo lake ni kufikia wanawake 200 kwa mwaka.
✅️Mkewe Issa Mbaga anasema hilo linamtatiza ila hana jinsi, anakubaliana nalo kwa vile anampenda mume
'Kuna wakati, kama anafanya kazi hiyo mchana sina shida, ila ikiwa usiku wa manane, napata mashaka na namuuliza'. Anasema Rahma Waziri, mke wa Issa huku akicheka.
✅️✅️✅️Wakati nasoma kuna eneo nilikuwa napita, kila siku nakuta akina mama wengi wamekaa, nilikua najiuliza kuna msiba? Marehemu mama yangu mkubwa akaniambia ni akina mama hao wanasubiri kuhudumiwa na mkunga, kuanzia hapo nikashawishika, kwa hiyo nimekua mkunga kwa kuchagua sio kuchaguliwa'.
SawaVijana wengi wa umri wa Mbaga unaweza kuwakuta kwenye shughuli nyingine kama Bodaboda, kilimo ama biashara nyingine, lakini kwake, yuko tayari kuamka usiku wa manane kusaidia wanawake wanaotaka huduma za ukunga.
Afya njema...Wanaponiona sasa huwa wanashindwa kuamini, wanasema wewe ndo muhudumu wewe ndo mkunga? Wanashangaa, lakini wakipata huduma yangu wanafurahia'
Hata hivyo furaha yake ni kuona wanawake na watoto anaozalisha wakiwa na afya njema.
✅️✅️Najua kuna zahanati, lakini wakati mwingine unapatwa na shida usiku na zahanati ni mbali, hapo Issa anakusaidia. Huduma anazotoa ni nzuri, yuko tayari muda wote, anaweza kukuangalia anajua namna gani ya kukusaidia, nashukuru amenisaidia.
📌📌Lakini kwa nini anafanya kazi ya ukunga bure?
'Afya ya uzazi ya mama na mtoto ndiyo masuala yanayopigiwa chapuo na mataifa mengi. Mama ama mtoto kufa na wewe unaweza kusaidia, ni ukatili, sitaki kuwa sehemu ya ukatili huo'.
📌Kazi hii kwa muda mrefu nimefanya kwa kujitolea tu, wakati mwingine wengine wanasema asante (kutoa kiasi cha pesa), nashukuru lakini huwa najitolea tu silipwi chochote.
AiseeKazi hii ya ukunga kwake ni ya kujitolea tu halipwi hata shilingi moja. Anasema kuifanya kazi hiyo kuna gharama maana yake mama akishindwa kulipa unampa wakati mgumu na wakati mwingine ni sawa na kumuhatarishia maisha yake.
Jino kwa jino..
Bado ni hatariMvua zinaendeleaje kwenu