Uwezekano wa kutoka Form Four kwenda Diploma

Janja PORI

JF-Expert Member
Jul 31, 2011
825
246
Wadau wa Elimu salamu,
Napenda kuuliza kama na kijana afaulu form 4 labda division two na staki aende advance school kuna uwezekano wa kuunga diploma bila certificate ??
 
Wadau wa Elimu salamu,
Napenda kuuliza kama na kijana afaulu form 4 labda division two na staki aende advance school kuna uwezekano wa kuunga diploma bila certificate ??

Wekaaa matokeoi yakee mbonasioo mchanganuajii wa mamboo na alisoma masomo ganii tumsaidiee mbona maelezo yakoo hayajitoshelezii
 
Uwezekano upo lakini endapo tu huyu mtahiniwa ataamua kujiunga na masomo katika fani za uuguzi na ufamasia au fani zote za uhandisi,na tofauti na Diploma za course nyingine hizi huchukua miaka mitatu badala ya miwili.
 
Wadau wa Elimu salamu,
Napenda kuuliza kama na kijana afaulu form 4 labda division two na staki aende advance school kuna uwezekano wa kuunga diploma bila certificate ??

mkuu Janja PORI hapa mjini. na wenyewe wanasema mjini shule.. Hebu toa hiyo labda kwenye maelezo yako upate jibu sawia. Amesoma masomo gani na anataka kusomea fani gani ni la msingi zaidi.

Utaelekezwa hadi pa kwenda au kumpeleka kama ni kweli ulichoandika. manake hiyo LABDA yako ni kama unatupima ufahamu wetu juu ya hili. Na mi nnaamini hili ni jukwaa la kisomi. Wanaelewa meengi juu ya masomo.
 
Wadau wa Elimu salamu,
Napenda kuuliza kama na kijana afaulu form 4 labda division two na staki aende advance school kuna uwezekano wa kuunga diploma bila certificate ??

Hataweza labda awe alikuwa anasomea science so itabidi aendelee na masomo yake ya science huko chuo but bado hajafanya ujanja coz diploma ya science ni miaka 3 ni sawa tu na yule aliyeanza cerficate ambapo mwaka mmoja wa cerficate na wa miwili ya diploma,namtakia masomo mema ya chuo
 
Wadau wa Elimu salamu,
Napenda kuuliza kama na kijana afaulu form 4 labda division two na staki aende advance school kuna uwezekano wa kuunga diploma bila certificate ??

Inategemea anataka kufanya nini yaani Degree gani anataka kuchukua..kuna baadhi inakubali kuenda kwenye diploma!
 
pHx baadhi kama zipi? Comp.sc je

Aise Comp degree tena ndio rahisi zaidi. Kuna colleges nyingi sana hapa bongo ambazo zinakubali mtu kuingia kufanya Diploma..kuna baadhi zitakubali kufanya kwa mwaka nyingine kwa miaka miwili, na kuna ambazo pia zinauhusiano wa vyuo vikuu vya Nje kama UK, INDIA na USA.

Ambapo unaweza jiunga na advance diploma then ukamalizia na degree kwenye hicho chuo (1year - total ukipiga hesabu ni 4-5years una degree).

Ila kabla hujajiunga hakikisha hiyo college imesajiliwa na NACTE na hiyo diploma inatambulika maana kuna college kadhaa ni wasanii. Hii ni nuhimu ili ukienda kuhakiki hicho cheti cha degree TCU wakikubali.
 
Wadau wa Elimu salamu,
Napenda kuuliza kama na kijana afaulu form 4 labda division two na staki aende advance school kuna uwezekano wa kuunga diploma bila certificate ??
Sasa skia dogo nikuambie kitu, siku hizi kunavyuo vimerahisisha sana. Open University kuna kitu kinaitwa Foundation course hiyo unaingia ukiwa na form.

Unasoma mwaka mmoja tu na ukifaulu una apply degree au diploma kulingana na kozi unayotaka kusoma. Mfano yupo mke wa waziri mkuu ameanza na hiyo foundation na sasa anafanya masters, wapo viongozi wakubwa serikalini wamepitia hiyo hatua,

waziri wa sasa aliyekabidhiwa wizara ngumu ya nishati na madini amaesoma hapo katika mlolongo huo huo na sasa anakula bata
 
Nenda DIT, ATC au MIST ukitoka hapo unaingia kazini, na mshahara wako unafanana na mwenye degree. Kama ulisoma sayansi.
 
Nenda DIT, ATC au MIST ukitoka hapo unaingia kazini, na mshahara wako unafanana na mwenye degree. Kama ulisoma sayansi.

Hapo ndipo huwa sikubaliani napo. Tena hapo ndio huwa sipapendi, huwa napinga!

Ni umbumbumbu kumshauri mtoto/kijana kwenda kusoma ili aajiriwe. Tanzania tunahitaji Wajasiriamali. Tunahitaji watu wenye nia na uwezo wa kujiajiri, sio watu wa kukimbilia kuajiriwa. Hivyo Kijana anatakiwa ashauriwe kusoma ili ajiajiri mwenyewe.

Nirudi kunako Mada. Binafsi, kama walivyosema wengine, sijui kama linawezekana kwa Kijana kutoka CSEE kwenda Diploma moja kwa moja kwa Masomo ya Sayansi Jamii (Arts/Social Science/etc). Kwa Masomo ya Sayansi linawezekana na linafanyika. Tunavyoandika hapa, DIT, St. Joseph na MUST tayari wameshatoa Matangazo na wanapokea Maombi ya Kozi za Diploma!
 
Back
Top Bottom