Nikupateje
JF-Expert Member
- Dec 22, 2009
- 1,334
- 988
Wote tumeiangusha CHADEMA kwa uzembe ambao hampendi ujadiliwe kwa kina kila unapoletwa kama si makusudi.
Tume ilitangaza matokeo ya urais, ubunge na udiwani vituoni kote kwa kuyabandika hukohuko hata kabla ya saa 06:00 usiku siku ya uchaguzi.
Wagombea uraisi waliopigiwa kura ni sita akiwemo Kikwete, Slaa na Lipumba. Kila wakala ali-sign matokeo na kisha Tume ikampa kila mmoja kopi ajue atakavyoitumia. Kitendo cha Tume kumpa kila wakala kopi ya matokeo kituoni ni aina nyingine ya kutangaza maana baadhi ya kopi zile ndizo Slaa alizotumia kama ushahidi alipoongea na wanahabari juzi.
Ukijumlisa idadi ya fomu za matokeo zilizotolewa na tume pale kituoni ni saba. Yaani ile iliyobandikwa kituoni na zilizogawiwa kwa mawakala. Kwa lugha nyingine ni kwamba Tume ilitangaza matokeo kituoni mara saba!
Mara ya kwanza ni pale ilipobandika kituoni na mara sita ni zile ilizowapa mawakala kuondoka nazo wakajichagulie jinsi ya kuzitumia.
Kituo kutopata watizamaji wengi wa matokeo ya pale haiondoi ukweli kwamba matokeo ya pale yameshatangazwa publically. Labda tu kwa wenye ugonjwa wa kudhani kutangazwa kwa jambo ni pale linaposikika duniani kote.
Kutangaza ni pale unapoweka jambo lako hadharani kwa public consumption kama unavyobadika matokeo kituoni.
Turudi kwenye hoja yangu ya uvivu .
Hivyo basi hatukuhitaji kabisa matokeo mengine zaidi ya yale yaliyotangazwa kituoni. Kama jimbo lilikuwa na vituo 300 ilibidi kila apendaye ajumlishe kila kituo ili kujua kwa jimbo zima Kikwete kapata kura ngapi na Slaa na wenzake wamepata ngapi.
Kama wapo wavivu wa kujumlisha basi hilo ni tatizo lao lakini binafsi sikuhitaji professa wa dunia hii kuja kunisaidia kujumlisha hata kama jimbo lingekuwa na vituo elfu kumi.
Sikuamini macho na masikio yangu nilipoona hakuna pressure inayoshabikiwa ya kushinikiza matokeo ya kila kituo. Ni kweli vituo vilikuwa 52,000 na hivyo gazeti maalumu lingechukua siku nne kuyachapisha matokeo ya nchi nzima kituo kwa kituo.
Ingefanyika hivyo basi leo hii kila mmoja angekuwa na haki ya kusema jimbo fulani SLAA kachakachulliwa kura kadhaa na KIKWETE kaongezewa kura kadhaa.
Narudia utaratibu. TUme ilitoa kopi ya matokeo kituoni na kwa mawakala zaidi ya sita. Hivyo kulikuwa na source zaidi ya sita kupata matokeo ya kituo kwa kituo. Kama gazeti lingehitaji usahihi lingekaa jimboni ambako mawakala walikuwa wamekusanyika kuwapelekea matokeo wenzao waliokuwa wanajumlisha matokeo ya vyama vyao.
Kumbe waandishi wa habari hawakuhitaji kupoteza petroli kwenda kituo kwa kituo kupata matokeo ya huko na kuyachapisha magazetini. Je, inawezekana na waandishi walikuwa wavivu wa kujumlisha hadi wasubiri yaliyojumishwa na Tume pale jimboni?
Lakini waandishi wangejitosaje kwenye biashara hiyo ambayo nyinyi wote hamkuionyesha kama ni habari ya muhimu na badala yake mkawa mnasubiri kujumlishiwa na Tume pale jimboni?
Mimi naona hiki ndicho kilichomuangusha kila mtanzania. Hata mwana-CCM aliyeshinda hawezi kujivunia ushindi na kumsuta mwana-CHADEMA kwa kuchanganua kituo kwa kituo. Sanasana mwana-CCM huyo ataishia kusema aliamua kujenga imani na Tume kama muumini anavyojenga imani kwa mchungaji wake.
Namalizia kwa kuweka thread zilizosisitiza matokeo ya kituo kwa kituo na muone jinsi tulivyoisua hiyo mada kila ilipoletwa:
Tulionyana hivi: { https://www.jamiiforums.com/matukio/83944-tumekataa-matokeo-kituo-kwa-kituo-uvivu-wetu.html}
Kisha ikawa hivi: {www.jamiiforums.com/results-matokeo/83377-kujumlisha-matokeo-kunatushinda-tuweze-nini-duniani.html}
Na baadaye hivi: {www.jamiiforums.com/results-matokeo/83558-poor-media-houses-and-journalists.html}