MmasaiHalisi
Senior Member
- Jan 15, 2009
- 192
- 23
Imeandikwa na Maulid Ahmed; Tarehe: 1st May 2009
Viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM wa Mkoa wa Tabora, wamemtaka Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi, kuacha kutukana viongozi wa chama hicho na kama anataka siasa aingie kwenye chama chochote na kupambana na wanasiasa majukwaani. Sambamba na hilo, wamemtaka kuwaomba radhi wana CCM wa Tabora kwa walichadai ni kumkashifu na kumdhalilisha Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz kuwa miongoni mwa mafisadi papa watano aliowataja.
Tunahoji nafasi yake ni nini kwenye CCM Mengi ana historia ya kulumbana kwa kashfa na mawaziri wengi nchini, tunamtaka aache mara moja na kama anataka siasa aingie kwenye ulingo wa siasa na tutakutana naye kwenye majukwaa ya kisiasa, alisema Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa, Patrick Kabaye, aliyesoma tamko la viongozi hao wa UVCCM Tabora mbele ya waandishi wa habari Dar es Salaam.
Kabaye aliyefuatana na Mwenyekiti wa UVCCM wa Mkoa wa Tabora, Robert Kamoga na wenyeviti wa UVCCM wa wilaya zote za mkoa huo, alisema wanalaani kitendo cha Mengi kumkashifu kiongozi wao ambaye wananchi wake wana imani naye.
Tumefuatilia kwa karibu mwenendo wa ziara za Mengi akiwa na msafara wa wabunge, huku akitoa misaada mbalimbali na tumepata taarifa anakuja Wilaya ya Tabora, UVCCM inatoa angalizo kama misaada yake inaendana na kutukana na kuwaundia majina mabaya viongozi wetu, hatutavumilia hilo, wananchi wa Tabora wana matatizo, lakini wanaheshimu utu na viongozi wetu tuliowachagua kidemokrasia, alisema.
Viongozi hao waliitaka serikali kuchunguza kauli za Mengi na kumchukulia hatua kali za kisheria ili iwe funzo na watu waheshimu utawala wa sheria. Tunaiomba serikali iangalie upya sheria na matumizi haya mabaya ya vyombo vya habari ambayo yanaweza kuleta mtikisiko kwenye nchi na serikali ipige marufuku tabia hii ya Mengi kutumia umasikini wa Watanzania kupandikizia chuki watu wengine, alisema Kabaye kwa niaba ya wenzake.
Walisema vijana hawatakuwa tayari kuwabeba wabunge mwaka 2010 wanaoshiriki katika ziara za Mengi ambazo wameziita zinakichafua chama na serikali kupitia kivuli cha kusaidia wanyonge. Viongozi hao wameeleza kumuunga mkono Rostam na kutokuwa tayari kuona anadhalilishwa bila kuwa na ushahidi wa jambo lolote na imani ya serikali haitaruhusu tabia ya watu kujitafutia umaarufu kwa gharama za kuchafua wengine.
Rostam ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mjumbe wa NEC wa Mkoa wa Tabora na Kamanda wa UVCCM Wilaya ya Igunga. Kauli hiyo ya vijana hao ni mfululizo wa watu waliopingana na Mengi tangu kutoa tamko lake la kuwataja mafisadi papa watano kati ya 10. Wengine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Sophia Simba, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na watuhumiwa wenyewe akiwamo Yusuph Manji waliodai kauli hiyo inaleta uchochezi kwa jamii na kuonyesha ubaguzi wa rangi.