Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,534
- 51,263
Mnapoteza muda kufikiria kwamba huyu wa sasa ataishi kwa huruma ya ajaye.
Jana ijumaa yamemalizika mafunzo maalum ya viongozi wa juu 60 pale bahari beach jeshini.
JPM analiandaa vyema kiuongozi kundi lake litakalokuwa na nguvu kuanzia 2020 - 25, na kwa taarifa yako marais wamekuwa wakishindwa kuwaweka viongozi chaguo lao kwa sababu wao wenyewe wamekuwa hawaaminiki.
JPM anaaminika kwa wananchi, na wananchi wanawakubali wale ambao ni chaguo lake la moja kwa moja, rejea Kassim Majaliwa Majaliwa.
Usishangae 2025 JPM akaweka mtu wake na akaungwa mkono na chama.
mwaka 2025 aweke mtu wake asiweke mtu wake haimsaidii, ataendelea kuishi kwa huruma ya huyo atakayemuweka. Na Uraisi huwa hauna ubia, ukishakizoea kiti ukajua chaneli zinavyokwenda basi hata yule aliyekuweka asije kujifanya kuingia kwenye 18 zako unaweza kumshughulikia!.
Hata Mwalimu Nyerere alikuja kuujua ukweli huu baadae sana kwenye maisha yake pale mtu aliyempigania kwa nguvu na akili zake zote BWM alipoamua kuuza NBC na mashirika mengineyo bila kujali JKN anaumia au haumii, sasa hilo ni dogo, kama JKN angechonga kama alivyokuwa akichonga kipindi cha mstaarabu AHM naye angejua tu ni nini nguvu ya kiti alichowahi kukikalia yeye mwenyewe